Hivi TRA waweza kamata gari ambayo nnunuzi wa gari hajafanya transfer?

Old-Timer

Member
Aug 9, 2011
76
15
Gari ya ndugu yangu imekamatwa leo huko Morogoro kwa kosa la kutofanyiwa ownership transfer. Jamaa alinunua hiyo gari miaka miwili iloyopita na hakubadili jina kwenye kadi. Leo amekamatwa na agent wa TRA, eti hajafanya transfer ya gari na alipaswa kufanya hivyo ndani ya siku 30 baada ya mauziano, Afisa huyo alisema mmiliki wa gari alikua na exemption hivyo inatakiwa kulipwa TZS 2,000,000/= .

Nachokifahamu ni iwapao jamaa angeenda TRA kufanya transfer ndio angetakiwa alipe exemption, vp akamatwe barabarani! Ndugu yangu ni mtumishi wa umma, je anaweza kunufaika na exemption ya gari hiyo?
 
Nijuavyo ni kuwa mkataba wa mauziano ni baina ya mnunuzi na muuzaji, Naombeni ushauri wanaJF
 
tra ni wezi sana, unawezaje nunua gari kwa shs milion mbili,ushuru ukawa milioni tatu
 
Aliyesamehewa kodi ni huyo aliyekuuzia gari na kamwe siyo wewe, kalipe kodi ya serikali.
TRA wanayo mamlaka ya kukusanya kodi kisheria ikiwa ni pamoja na kukamata na kuzuia na baadaye kupiga
mnada mali ambazo hazijalipiwa kodi ili kuipata kodi ya serikali. Mara unaponunua mali kama vile gari kabla hujaanza
matumizi yake ni lazima ulipie kodi.
Dola/ Taifa madhubuti haliwezi kujengwa na wakwepa kodi. Ukwepaji kodi ndiyo uliotufikisha kwenye umasikini wa kutupa.
Pamoja na madhaifu kadhaa ya TRA, lakini tujijengee tabia ya kupenda kulipa kodi ndipo tuwe na moral authority
ya kuilaumu serikali isipotupatia huduma muhimu.
 
Huo ni wizi.Maana kuuziana gari ni kitu kingine na kufanya transfer ni kitu kingine.Je wamejuae kama ameuziwa?Labda kama aliye muuzia ndo amekwenda TRA kuchongea ili wamkamate jaama yako.
 
Aliyesamehewa kodi ni huyo aliyekuuzia gari na kamwe siyo wewe, kalipe kodi ya serikali.
TRA wanayo mamlaka ya kukusanya kodi kisheria ikiwa ni pamoja na kukamata na kuzuia na baadaye kupiga
mnada mali ambazo hazijalipiwa kodi ili kuipata kodi ya serikali. Mara unaponunua mali kama vile gari kabla hujaanza
matumizi yake ni lazima ulipie kodi.
Dola/ Taifa madhubuti haliwezi kujengwa na wakwepa kodi. Ukwepaji kodi ndiyo uliotufikisha kwenye umasikini wa kutupa.
Pamoja na madhaifu kadhaa ya TRA, lakini tujijengee tabia ya kupenda kulipa kodi ndipo tuwe na moral authority
ya kuilaumu serikali isipotupatia huduma muhimu.

TRA bana ni wataaram wa kukusanya kodi kwa walala hoi,huku wakiwaacha wawekezaji na wafanya bishara wakubwa wakipeta tu.
 
hyo scenario yako iko hiv ukinunua gari lolote lenye exemption lazma u top up the excempted amount na hii iko kisheria refer motor vehicles(tax on registration and transfer) Act chapter 124 revised edition 2006 nazani hapo huto lalamika tna
 
Back
Top Bottom