Hivi Tigo na Tanesco wameniibia au tupo wengi??

Snipes

JF-Expert Member
Jul 2, 2013
9,109
16,681
Habari Gani wakuu

juzi(ijumaa) nimenunua umeme mida saa 12 jioni kupitia Tigo Pesa, kama ilivyo kawaida ukinunua umeme unaletewa ujumbe kwamba muamala wako umekamilika na majibu yakirudi unaletewa umeme(token)

maajabu nimepata juzi mpaka sasa bado yanaendelea kwanza waliniletea ujumbe ambao hawakuwahi kuniletea hata siku moja, ulisomeka hivi "Transaction successful" na manamba kibao bila token(namba za luku)

baada ya masaa 6 nilipiga simu huduma kwa wateja wakanambia kuna tatizo nikawaelewa, nililala kiza nikajua mpaka kufika asubuhi ya jana watakuwa washanitumia umeme, asubuhi kuamka hakuna kitu...nilivyowapigia bado wakanambia bado kuna tatizo, hivi mpaka sasa pesa yangu haijarudishwa na si kawaida yao kama kuna matatizo hurudisha pesa kama ilivyo.

maajabu zaidi yametokea leo baadhi ya watu wananunua umeme na baada ya sekunde 45 tu umeme wanapata.

sasa hapa nawauliza ndugu zangu na nyie pia iliwatokea au ndio nimelipia kodi bila kujua??

nimejiandaa na kila aina ya jibu

nawasilisha
 
Mimi siwezi kununua umeme au chochote kutumia tigo pesa. Sijui ni line yangu tu au kuna issue ya kiufundi huko tigo.
 
Mimi nimefanya muamala kutoka CRDB Simbanking kwenda TigoPesa leo siku ya tatu hakuna kitu. Niliwapigia wanasema eti mpaka J3 coz of sikukuu na weekend...
 
Bora wewe tigo .mimi ilikuwa vodacom two years mpk sasa ni kaamua kusamehe tu
 
nilinunua umeme jmosi hadi leo hawajanitumia hyo token elf 50 yangu nimewahifadhi tu hao tigo ngoja kesho naenda tcra
 
Habari Gani wakuu

juzi(ijumaa) nimenunua umeme mida saa 12 jioni kupitia Tigo Pesa, kama ilivyo kawaida ukinunua umeme unaletewa ujumbe kwamba muamala wako umekamilika na majibu yakirudi unaletewa umeme(token)

maajabu nimepata juzi mpaka sasa bado yanaendelea kwanza waliniletea ujumbe ambao hawakuwahi kuniletea hata siku moja, ulisomeka hivi "Transaction successful" na manamba kibao bila token(namba za luku)

baada ya masaa 6 nilipiga simu huduma kwa wateja wakanambia kuna tatizo nikawaelewa, nililala kiza nikajua mpaka kufika asubuhi ya jana watakuwa washanitumia umeme, asubuhi kuamka hakuna kitu...nilivyowapigia bado wakanambia bado kuna tatizo, hivi mpaka sasa pesa yangu haijarudishwa na si kawaida yao kama kuna matatizo hurudisha pesa kama ilivyo.

maajabu zaidi yametokea leo baadhi ya watu wananunua umeme na baada ya sekunde 45 tu umeme wanapata.

sasa hapa nawauliza ndugu zangu na nyie pia iliwatokea au ndio nimelipia kodi bila kujua??

nimejiandaa na kila aina ya jibu

nawasilisha
Mm kama ww nlipata msg hiyohiyo na mpk leo j2 ucku cjalata umeme
 
nimetoka kuongea nao muda si mrefu wanasema bado kuna tatizo
cha ajabu watu wamenunua nimewashuhudia leo
 
Labda kuna tatizo upande wako mm tigo nikinunua luku dk5 nying nakua nimepata umeme itakua tatizo la kiufundi ila usichoke kuwapigia
 
Leo mchana nilinunua Luku lakini sikuparudishiwa message yenye token baada ya kama nusu saa nikawatafuta hewani wakaniambia tatizo lipo na linashughulikiwa, baada ya kama dakika 10-15 nikatumiwa message yenye token na message nyingine ilikuwa "Ahsante kwa kuwasiliana na Tigo huduma kwa wateja.Ombi lako limeshughulikiwa, Kumbukumbu namba*****
 
Nazani kulikua na tatizo hiyo Siku ila niliwapigia Siku ya Pili wakanitajia Token namba mimi. Hebu wapigie waambie wakutajie.
 
Back
Top Bottom