Hivi tbc wanafahamu umuhimu wa karibu travel and tourism fair kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi tbc wanafahamu umuhimu wa karibu travel and tourism fair kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanawao, Jun 7, 2011.

 1. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,983
  Likes Received: 1,640
  Trophy Points: 280
  HIVI TBC WANAFAHAMU UMUHIMU WA KARIBU TRAVEL AND TOURISM FAIR KWELI?
  Juzi tarehe 05/06/2011 ilikuwa siku ya mwisho ya maonesho ya Karibu Travel and Tourism Fair (KTTF) yaliyofanyika kwa siku tatu mfululizo ndani ya mji wa Arusha. KTTF ni maonesho yanayokutanisha wadau wa utalii kutoka sehemu mbalimbali za Afrika na hata nje ya Afrika. Lengo kubwa la maonesho haya likiwa ni kutengeza ushirikiano au mtandao mzuri wa kibiashara kati ya wadau waliopo ndani ya sekta hii. Pili inatoa nafasi nzuri kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake mbalimbali kwa wadau wanaotoka nchi nyingine barani Afrika na hata nje ya Afrika.
  Tanzania imekuwa ikijaribu kutangaza vivutio vyake vya utalii ingawa sio kwa ushindani mkubwa kama nchi nyingine. Naandika makala hii kutokana na jambo moja ambalo limenisikitisha kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokutilia maanani kilichokua kikiendelea kwenye Karibu Travel and Tourism Fair. Nilitegemea katika Dunia hii ya ushindani mkubwa wa kimasoko kuwa TBC wawe mstari wa mbele kuutangazia ulimwengu maonesho haya kila siku angalau kwa saa moja tu.
  TBC ina channel mbili ambazo ni TBC1 & TBC2 ambazo zote zipo kwenye Star Times. TBC2 inapatikana kwenye DSTV. Star Times na DSTV zinaonekana sehemu nyingi tu nje na ndani ya Afrika. Kwa mantiki hii kutangaza maonesho haya kungevuta wadau wengi wa utalii ndani na nje ya Afrika kuzidi kufahamu vivutio vya utalii Tanzania na kukuza soko letu la Utalii. Vivutio vyetu vikifahamika watalii wataongezeka, pato la Tanzania litaongezeka na kusaidia kupunguza utegemezi kwa nchi hisani.
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280

  hawakupata maelekezo ya kuitangaza hiyo exhibition toka kwa Mukama na Nape. TBC are trained dogs.....maximumly obey orders and directives from CCM dudes!!
   
Loading...