Hivi tbc wanafahamu umuhimu wa karibu travel and tourism fair kweli?

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
3,140
5,629
Juzi tarehe 05/06/2011 ilikuwa siku ya mwisho ya maonesho ya Karibu Travel and Tourism Fair (KTTF) yaliyofanyika kwa siku tatu mfululizo ndani ya mji wa Arusha. KTTF ni maonesho yanayokutanisha wadau wa utalii kutoka sehemu mbalimbali za Afrika na hata nje ya Afrika. Lengo kubwa la maonesho haya likiwa ni kutengeza ushirikiano au mtandao mzuri wa kibiashara kati ya wadau waliopo ndani ya sekta hii. Pili inatoa nafasi nzuri kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake mbalimbali kwa wadau wanaotoka nchi nyingine barani Afrika na hata nje ya Afrika.
Tanzania imekuwa ikijaribu kutangaza vivutio vyake vya utalii ingawa sio kwa ushindani mkubwa kama nchi nyingine. Naandika makala hii kutokana na jambo moja ambalo limenisikitisha kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokutilia maanani kilichokua kikiendelea kwenye Karibu Travel and Tourism Fair. Nilitegemea katika Dunia hii ya ushindani mkubwa wa kimasoko kuwa TBC wawe mstari wa mbele kuutangazia ulimwengu maonesho haya kila siku angalau kwa saa moja tu.
TBC ina channel mbili ambazo ni TBC1 & TBC2 ambazo zote zipo kwenye Star Times. TBC2 inapatikana kwenye DSTV. Star Times na DSTV zinaonekana sehemu nyingi tu nje na ndani ya Afrika. Kwa mantiki hii kutangaza maonesho haya kungevuta wadau wengi wa utalii ndani na nje ya Afrika kuzidi kufahamu vivutio vya utalii Tanzania na kukuza soko letu la Utalii. Vivutio vyetu vikifahamika watalii wataongezeka, pato la Tanzania litaongezeka na kusaidia kupunguza utegemezi kwa nchi hisani.
 
wakenya tukisema kilimanjaro yetu mnalia mlia.....tbc2 inapatikana chanel no ngapi dstv?
 
Kwa ujumla serikali haijui umuhimu wa hayo maonyesho hata kidogo ndo maana kama yamwaka ajana hakukuwa na kiongozi aliyekuja kuyafungua.

Pongezi kwa waasisi wa Karibu travel fair Damian Bell, Victor Mollel these were the key persons. Mwaka huu pia ilikuwa hamna kiongozi wa kufungua sijui walimkamatia wapi Nyalandu ndo akapitia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom