Hivi tatizo ni watendaji au mamlaka za uteuzi? Tukisema tuko kwenye mkwamo mkubwa ni kosa?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Watendaji wetu wameshindwa kabisa kulisaidia Taifa letu, wameshindwa kua wabunifu kumsaidia Mkuu wa nchi walao kuwe na tofauti kubwa kati ya awamu zilizopita na awanu ya 5. Tofauti iliyopo ni makosa makubwa yanayofanywa na watendaji wa sasa kuliko hata wa serikali zilizopita kabisa.

Inawezekanaje waziri mzima uliyepewa dhamana ya kutatua shida za wananchi umepewa na usafiri, unalipwa posho kwa pesa za umma unafika mahali unakuta wananchi wamebeba madumu ya Maji kwenye mikokoteni na baiskeli wanahemea,l maji,badala ya wewe kukaa nao uwazikilize shida zao matokeo yake wewe unapanda baiskeli iliyobeba madumu ta maji naranda nayo unaendesha? Hiyo kitaalam ina msaada gani kwenye utatatuzi wa shida za wananchi?

Eti mkuu wa mkoa unaacha shughuli za kulijenga taifa unaavaa sare za chama unaenda kupiga kampeni ili iweje? Hivi viongozi wa chama kuanzia ngazi ya mkoa mpaka shina wana kazi gani? Unapamda gari ya umma, unatumia pesa za umma kujilipa posho kwenda kufanya kazi ya siasa?this is only in Tanzania.Huu kwanini tusiite kua ni ushamba wa madaraka? Kwa sababu kama unafanya kitu usichokijua tafsiri yake ni ushamba huo.

Mkurugenzi mzima wa halmashauri/manispaa unavaa T-shirt na kofia unaingia kwenye mkutano wa chama mchana kweupe, kwa sheria ipi? Nani kasema?Hii imewahi kutokea katika awamu ipi ya serikali tangu yetu nchi ipate Uhuru?Mimi sijui labda wakati wa chama kimoja kwa sababu kipindi hicho hakukua na tofauti kubwa sana kati ya shughuli za chama na serikali. Unashindwaje kutumia muda ule kukaa mizani na kuchora ramani za mipango yako ili mkeshe na watendaji wako wa chini kutatua matatizo ya wananchi?

Lazima tukubali kwamba huku ni kutokuelewa watendaji wetu wanafanya nini, hawajui majukumu yao kua ni makubwa sana hasa kwenye kulivusha taifa hapa tulipo kwenda mbele.Huenda ndio wakati wa kampeni CCM walikua na sera nzuri sana za kutuvusha, lakini tatizo watendaji wa serikali wameshindwa kabisa kua wabunifu,wameshindwa kutambua wajibu wao kwa majukumu waliyovikwa. Mtu anafurahia tuu shangingi na viyoyonzi yake kutwa nzima pasipo kutambua kua lile shangingi ni mzigo mkubwa sana kwao kwa majukumu wanayotakiwa kuyatekeleza.

Watendaji wa serikali badilikeni tulivushe taifa hili, kama hamjawa mfano kwa walio chini yenu msifikiri kua kuna muujiza wa kuwabeba.
 
Tatizo hapo kwa wakurugenzi wa halmashauri za miji na wilaya kuchanganya shughuli za Chama na za serikali. Ni tatizo la kikatiba na kimazoea la kuifanya Chama kama dini (imani kali). Na hili hufanywa kuanzia ngazi ya taifa!! Unakuta ziara za viongozi wakuu watatu wa nchi, zinabebwa kichama na hawaonyi wala kutofautisha shughuli hizi. Na hii imekuwa tatizo ambalo wakurugenzi hawawezi kuliepuka na hivyo hujikuta budget ya serikali kufanya shughuli za Chama!!
 
Kwa wakurugenzi hicho kitu kwenye katiba hakipo kabisa, May be kwenye mamlaka za uteuzi katiba ndio tatizo mkuu
 
Hawana la kufanya!! Je wajua hata kabla kugawana miradi ya maendeleo ktk halmashauri husika. Huwa wanaitwa kwanza kwenye kamati ya madiwani ndani ya Chama na miradi hugawiwa huko kabla baraza la madiwani halijakaa!!!

Wakurugenzi hujiona waajiriwa wa Chama zaidi, kwa sababu ya mashinikizo ya idara za uteuzi.
 
Watendaji wetu wameshindwa kabisa kulisaidia Taifa letu, wameshindwa kua wabunifu kumsaidia Mkuu wa nchi walao kuwe na tofauti kubwa kati ya awamu zilizopita na awanu ya 5. Tofauti iliyopo ni makosa makubwa yanayofanywa na watendaji wa sasa kuliko hata wa serikali zilizopita kabisa.

Inawezekanaje waziri mzima uliyepewa dhamana ya kutatua shida za wananchi umepewa na usafiri, unalipwa posho kwa pesa za umma unafika mahali unakuta wananchi wamebeba madumu ya Maji kwenye mikokoteni na baiskeli wanahemea,l maji,badala ya wewe kukaa nao uwazikilize shida zao matokeo yake wewe unapanda baiskeli iliyobeba madumu ta maji naranda nayo unaendesha? Hiyo kitaalam ina msaada gani kwenye utatatuzi wa shida za wananchi?

Eti mkuu wa mkoa unaacha shughuli za kulijenga taifa unaavaa sare za chama unaenda kupiga kampeni ili iweje? Hivi viongozi wa chama kuanzia ngazi ya mkoa mpaka shina wana kazi gani? Unapamda gari ya umma, unatumia pesa za umma kujilipa posho kwenda kufanya kazi ya siasa?this is only in Tanzania.Huu kwanini tusiite kua ni ushamba wa madaraka? Kwa sababu kama unafanya kitu usichokijua tafsiri yake ni ushamba huo.

Mkurugenzi mzima wa halmashauri/manispaa unavaa T-shirt na kofia unaingia kwenye mkutano wa chama mchana kweupe, kwa sheria ipi? Nani kasema?Hii imewahi kutokea katika awamu ipi ya serikali tangu yetu nchi ipate Uhuru?Mimi sijui labda wakati wa chama kimoja kwa sababu kipindi hicho hakukua na tofauti kubwa sana kati ya shughuli za chama na serikali. Unashindwaje kutumia muda ule kukaa mizani na kuchora ramani za mipango yako ili mkeshe na watendaji wako wa chini kutatua matatizo ya wananchi?

Lazima tukubali kwamba huku ni kutokuelewa watendaji wetu wanafanya nini, hawajui majukumu yao kua ni makubwa sana hasa kwenye kulivusha taifa hapa tulipo kwenda mbele.Huenda ndio wakati wa kampeni CCM walikua na sera nzuri sana za kutuvusha, lakini tatizo watendaji wa serikali wameshindwa kabisa kua wabunifu,wameshindwa kutambua wajibu wao kwa majukumu waliyovikwa. Mtu anafurahia tuu shangingi na viyoyonzi yake kutwa nzima pasipo kutambua kua lile shangingi ni mzigo mkubwa sana kwao kwa majukumu wanayotakiwa kuyatekeleza.

Watendaji wa serikali badilikeni tulivushe taifa hili, kama hamjawa mfano kwa walio chini yenu msifikiri kua kuna muujiza wa kuwabeba.
Pole Sana, ukiendelea kufuatilia haya, utapata stroke bure.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom