Hivi tatizo ni wabunge au wanaokikalia kiti cha Spika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi tatizo ni wabunge au wanaokikalia kiti cha Spika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mazoko, Jul 28, 2011.

 1. Mazoko

  Mazoko JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 676
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wadau kuna jambo linaendelea katika bunge letu ambalo wao wanaliita bunge tukufu. Leo hii wakati wa maswali kwa waziri mkuu naibu spika kamkemea Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali kwa kugoma kukaa kimya wakati naibu spika akizungumza.Jana tena hali hii ilitokea leo wanamziki wa bongo fleva wameimba bunge kariakoo .Ila linalonisikitisha nikuwa naona kama wanaoongoza kikao wanatumia nguvu na ubabe mfano waleo kabla ya swali lazima maelezo japo kidogo yatolewe ili swali lieleweke kwa waziri mkuu naibu spika anasema uliza swali je swali bila miguu au kichwa litaelewekaje.Au jana mbunge wa kasulu Moses Machali analalamika kuwa wabunge wa CCM wanamzomea wakati akitaka kutoa maelezo badala ya mwenyekiti kuwakemea wabunge wa CCM watulie yeye anasema kuwa Machali yeye aendelee kuongea asiwajali hao inamaana wabunge wa CCM wao wanaruhusiwa kupiga kelele wenzao wa upinzani wakiwa wanatoa hoja zao??na jambo hilo lakuikosea adabu bunge wameanzisha CCM toka siku wabunge wa CHADEMA kutoka nje wakati RAIS akitaka kutoa hotuba bungeni.Mimi kwa mtizamo wangu nilitegemea kuwa kwa kuwa wenzao wa CHADEMA wakati wakutoka hawakuzomea wala kupiga kelele wao wangewaacha watoke kimya kimya ili kuonyesha ustaarabu.Pia wanaokikalia kiti naona kimewashinda wao wanatanguliza fikra zao zaidi ya kutumia hekima na busara
   
 2. Mazoko

  Mazoko JF-Expert Member

  #2

 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,369
  Likes Received: 3,687
  Trophy Points: 280
  Tatizo si wabunge bali wanaoendesha bunge. Kile kiti hakita mtu wa kupendelea chama fulani wa watu fulani kwa sababu yoyote ile. Na vile kanuni za bunge baadhi zina kasoro.............. Kanuni yoyote inayobeba neno hili................ ITAFANYIKA KWA JINSI SPIKA AU MWENYEKITI ATAKAAVYOONA INAFAA........ Kwa maana nyingine uwezo woooooteeeee wa bunge anakabidhiwa mtu mmoja.

  Mfano mwingine............ yule aliyeamuru Machali atoke nje alitumia kanuni gani kumruhusu kurudi ndani...??? Kwangu mimi naona baada ya kujihisi kachemka akaona abadili uamuzi. Vinginevyo Machali asingehudhuria siku nzima.
   
 4. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kiti kile hakina tatizo ila tatizo ni kwa Wabunge wanaokalia kiti hicho kwani wamebase saaana upande mmoja yaaani means wote wanatoka Chama Kimoja
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  unamaanisha wenje au?? Sorry sijakuelewa kwani kunamwingine alitolewa??
   
 6. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Leo wabunge watatu wa cdm, lisu, lema na msigwa nao wametolewa nje pia.
   
 7. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kiongozi akielekeza vibaya wafuasi hupotea.
  Spika na wenyeviti wanaongozwa na wabunge wa chama kimoja hivyo wao kukosa muelekeo wao na wadhifa wao kama waongozaji , ila wanageuka waongozwao.
  Miluzi ikiwa mingi mbwa hupotea.
  Spika na mwenyekiti wanapotezwa na matashi mengi ya wanamagamba.
   
 8. Kibuja

  Kibuja JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 510
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani Bunge la sasa limekosa mvuto kabisa, yaani itikadi za vyama zimetawala badala ya maslahi ya taifa, hasira, ghadhabu, utovu wa nidhamu, zomea zomea n.k. Shame on you. Hivi wapiga kura wenu mnafikiri tunafurahi mnavyo shout kama walevi?? kila mtu apewe muda wa kuwasilisha hoja yake bila kukatizwa kwa zomea zomea. Upendeleo wa wazi wazi kwa baadhi ya vyama haufurahishi hata kidogo. Kumbuka bunge hili si kama lile la miaka ya 47 sasa hivi runinga zimetapakaa kila mahali na wapigakura wenu tunawaangalia tu na hukumu yenu si mbali!!! mshindwe
   
 9. L

  Lugeye JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 1,065
  Likes Received: 1,361
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni makada wa ccm wanaleta ushabiki wa kivyama ktk Bunge,hao wenyeviti wote ni makada wa ccm so lazma wapendelee uccm!na pia siasa za makundi coz kila anaeongaza Bunge yupo kundi la watu fulani wanaotaka urais 2015,kingine ni kwamba kama mnakumbuka Spika aliyepita alitolewa ktk uspika baaada ya kuonekana anatenda haki kwa wabunge wote bila kujali chama chake,kwa iyo na hawa wanaopata nafasi kuongoza Bunge wanaogopa kuiga uongozi wa mh.SITTA,wasije wakatolewa kafara ya kutoteuliwa kugombea tena ubunge 2015,angalieni wabunge wa upinzani hasa CDM na NCCR,CUF.wakiomba mwongozo hata kama atakuwa yeye ndo wa kwanza kuomba na akafatiwa na mbunge wa ccm aliyeomba mwongozo, cha kustaabisha atakaepewa nafasi ya kwanza ni wa ccm japo wa cdm ndo aliyetangulia kuomba,hiki kitu kimetokea wiki hii tu alipokuwa mh Simbachawene anaongoza Bunge,alimnyima mh TINDU LISSU,akamruhusu mh fulani hv kutoka ccm,Tunaomba hawa viongozi wanaongoza Bunge wawe FAIR.
   
 10. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tusilalamike hata kidogo tusubiri kuwapa hukumu yao ya haki wale wote wasiotenda haki kwani wao ndio chanzo cha nchi kuendeshwa kihuni.
   
Loading...