Hivi tatizo letu ni mabeberu au ni CCM na uongozi wake wa miaka yote toka uhuru?

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,087
2,000
Wanajamvi,

Jana wakati wa yale mahojiano baina ya Tundu Lissu, Masilingi pamoja na muendeshaji ama host wa kipindi cha Straight Talk Africa, Shaka Salli. Nilipata kujifunza mambo kadhaa, ambayo nayo yalinifanya kujiuliza maswali kadhaa wa kadha.

Pia niseme kuwa, itakuwa ni jambo la msingi kabisa endapo tutafanikiwa kuanzisha cheche ya mabadiliko chanya, ambayo itatufungua kama Taifa.

Kwa kifupi, niligunduwa hoja mbili za msingi, ambazo kimsingi ni kuhusu maendeleo yetu vs ccm vs mabeberu!

Yani hapo ina maana kwamba ccm mara zote wanasema kuwa kikwazo cha maendeleo yetu, ni hao mabeberu. Yani toka uhuru wamekuwa wanadai wanatupatia maendeleo, lakini kikwazo cha kupata maendeleo makubwa zaidi na kuufuta umasikini,ni mabeberu. Mabeberu ambao wameingia nao mikataba ambayo imewafukarisha wananchi na Taifa na kuwafaidisha cronies wachache wa ccm. Hapo alumiwe Lissu au chadema kivipi?Wengi kupitia ten percent nk. Ni mawaziri wa ccm.

Lakini pia Lissu alizungumzia ile sheria ya kikoloni/mabeberu ya mwaka 1953, ambayo ilitumika kumuweka mwalimu ndani wakati wa harakati za kuwaondoa hao mabeberu!Sheria hiyo hiyo imetumika kumweka Mbowe ndani. Je hapo beberu ni nani? Au ni rangi tuseme imebadilika? Certainly kuna mabeberu weusi. Ni levels tu, lakini ubeberu ni ubeberu.

Propaganda hii hii ya mabeberu, ndiyo iliyopelekea Lissu kutaka kuuwawa, Lissu ambaye naye alishaswekwa ndani mara kadhaa kabla ya jaribio la kumuuwa, kwa sheria hizo hizo kandamizi za mabeberu walizoziacha! Je ccm party “is eating a cake and have it too”? Unapotumia sheria za kibeberu kukandamiza wananchi, halafu unasema beberu ndo mbaya, utaeleweka vipi? Au ni sisi wananchi hatujielewi?

Hilo limenifanya nikajiuliuliza sana maswali mengi. Pia nikafahamu ni kwanini Lissu aliwahi kuyasema yale aliyoyasema kule bungeni kuhusu Mwalimu! Kweli kuna mazuri na mabaya yake. Baya kubwa kabisa, ni kuirithisha ccm yake na “Taifa lake”, sera kandamizi za kibeberu dhidi ya wananchi, huku ikitumia propaganda dhidi ya mabeberu hao ambao ni marafiki zao kwa upande mwingine, dhidi yetu sisi wananchi! Na wananchi tunabaki kuchanganyikiwa, Kwani hata huko kwa mabeberu, hakuna sheria kandamizi kama huku kwetu.

Labda wakati huu tutamtambua adui yetu vyema, na Taifa letu litasonga mbele!

Tamaa za madaraka za viongozi hao wa ccm, ndizo zimetufikisha hapa! Kama ccm ingekuwa na mapenzi ya dhati kwa Taifa, isingeedelea kutudanganya kuwa maadui zetu ni “imperialists” peke yao! I think it is a combination of factors! I think the ccm leadership has failed us. Mmeshindwa kuja na jipya toka uhuru?
 
Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
6,270
2,000
Tatizo kubwa la nchi hii ni ccm ,kwa wao ndio waliipora Mali za nchi hii na kujimilikisha ,kuingia mikataba ya kimangungo kwa kutambua hayo wameamua kugoma kutoka madarakani ,wakiogopa kuulizwa Mali waluzojikimbikizia wamezipata wapi?
 
makinikia halisi

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
559
1,000
Kuna vitu ukifikiria kuhusu hii nchi vinatia hasira. Mfano tu prezda anashinda anangalia shilawadu badala ya kujifunza maswala ya kiuchumi na teknolojia ya dunia ya kwanza,Msukuma mbunge anatunga sheria za kisaidia nchi,mtoto wa shangaz anapewa kazi hazina, kwa kigezo cha undugu wakat hana sifa wala utalamu wa maswala ya fedha. Tatizo la Tz sio mabeberu n ccm,kama tatizo lingekuwa wao sirikali ya ccm isingeliwapigia magoti na kutembeza kabuli. ...ccm ilishindwa kuendwsha nchi wanakuja na visingizio visivyokuwa na fizi wala meno...
 
Umesema vyema kabisa!👍🏽

Nadhani pia ccm wanaichafua nchi yetu sana.
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,087
2,000
Tatizo kubwa la nchi hii ni ccm ,kwa wao ndio waliipora Mali za nchi hii na kujimilikisha ,kuingia mikataba ya kimangungo kwa kutambua hayo wameamua kugoma kutoka madarakani ,wakiogopa kuulizwa Mali waluzojikimbikizia wamezipata wapi?
Ni sawa na mwizi anayekimbizwa na yeye anajidai kukimbiza mwizi na kudai kuwa yuko mbele yake kumbe ndo yeye mwenyewe, lengo ni kuzuga ama kupoteza maboya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom