Hivi tatizo hili la umeme kukatika litakwisha lini?

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,715
Ndugu zangu Watanzania, bila shaka hamjambo. Mimi kama Mtanzania mwenzenu nawasalimia!

Ndugu zangu nimekuwa nakwazwa sana na hili suala la kukatika kwa umeme kila wakati kama siyo kila siku. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana yasiyokuwa na majibu, na ningeomba mtu mwenye majibu anaifahamishe ni kwanini umeme unakatika kila wakati?

1. Je, ni nguzo huwa mbovu mvua zikinyesha hivyo zinaanguka na kusababisha shoti? Na kama ndivyo! Mbona hata kiangazi bado umeme unakatika?

2. Je, au Tanesco huwa wanafanya matengenezo kila siku, mwezi na mwaka?Je, kama ndivyo, ni lini haya matengenezo yatakwisha ili tusione umeme ukikatika katika Hovyo?

3. Je, au maji kwenye mabwawa yameisha hivyo kupelekea mgao? Lakini mbona mvua zinanyesha? Na kama ndivyo ya kwamba mabwawa yanapungua maji na kupelekea kukosa umeme nchini, ni kwanini viongozi wanakomaa kujenga tena bwawa kubwa la uzalishaji wa umeme kutumia maji kwa pesa kubwa? Hawaoni kama tutarudi kulekule endapo maji yakipungua?

Ndugu zangu naombeni mnifahamishe sababu hasa za umeme kukatika maana ninapata sana wakati mgumu kuwaza na kuwazua!

Hivi ni nini tatizo na tufanye nini ili hili hili tatizo liishe na libaki historia!

Hivi nchi ambazo umeme haukatiki wenzetu wamewezaje?

Mimi nashangaa sana leo Karne hii ya 21 yenye teknolojia ya kila namna lakini bado hapa nchini kwetu umeme ni tatizo, ni kwanini viongozi wetu wasipambane na hili suala la umeme tu hata kama litamaliza miaka kumi lakini liishe kabisa na iwe historia?

Ni kwamba viongozi wetu hawalioni tatizo au shida kubwa ni nini?

Yaani nina maumivu yameujaza moyo nashindwa hata kuandika!

NI NANI ATATUSAIDIA TANZANIA?

 
Back
Top Bottom