Hivi Tanzania wanayo zungumzia CHADEMA ni Tanzania ipi?

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,780
2,000
Kwa wiki hizi chache niliamua kusitisha shughuli zangu za kuuza mikate stand ya Ubungo na kuanza kuzunguka mikoa mbalimbali kukusanya maoni ya raia mbalimbali kuhusu mwenendo wa nchi hususan katika awamu hii ya tano.

Niliwahoji kwenye daladala, bodaboda, vijiwe vya story, wafanya biashara wa kati, wakulima na raia wengine, ki ukweli Magufuli anakubalika kila kona ya nchi hii, nikaona ngoja niende mikoa ya kusini ambapo mpaka leo hii bado nipo huku na nimeshuka kwenye daladala muda mfupi ulio pita, huku kusini mwamba wanamkubali balaa.

Sioni kabisa future kwa CHADEMA, sioni future kwa Membe, narudia tena sioni. Na ziara hii imefanya nijiulize hivi hiyo Tanzania wanayozungumzia CHADEMA na hao wapiga kelele wengine ni hii hii au ni ile ya Kigogo2014 ambayo kuna miili kila kona imetapakaa kwa COVID-19? Nafikiri kuna Tanzania nyingine ipo Twitter na JF lakini kwa Tanzania hii ninayoishi na uhakika wapinzani hawatapata hata 10% ya kura zote zitakazopigwa.

Pole sana Lissu, umedunguliwa na risasi na unadunguliwa tena na Watanzania kwenye uchaguzi 2020
 

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
8,227
2,000
Tanzania mnayosema imefikia uchumi wa kati kabla ya 2025 ni Tanzania ipi ?

Au nyie manyani hamuoni m@cunduye ?
 

umusuntiwawe

Member
Jul 9, 2020
61
150
sasa ulitaka wasemeje wakati wapinzani walipigwa pini kufanya siasa miaka mitano.ngoja mikutano ianze uone watakapoweka uozo wa jpm kama wananchi hawatamgeuka within a minute na nina uhakika hata we utamchukia. Kwanza swala la ajira ndo litamfanya jpm azomewe jukwaani
 

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,398
2,000
Yaani kwa taarifa tu ni kuwa siku mkutano wa chadema ukaitishwa mji wa daressalaam utasimama. Nakuhakikishia Lissu akipanda jukwaani akaonyesha maovu na madhaifu ya mwenyekiti wenu ni dakika sifuri tu JPM akipita miji ya wakereketwa kama Mbeya anweza pigwa mawe.
1.Kodi zote zimepelekwa chato
2. Ajira zipo kwa wana ccm tu
3. Watu wana tekwa na kupotea
4. Mauwaji kila kona ya nchi
5. Vyama vingine kufunguliwa mashitaka

Yaani mwenyekiti wenu atabaki na wapiga tarumbeta tu
 

Mwakinyo

Member
Jul 29, 2020
38
75
TANZANIA sio Mali ya CCM ata Roman Empire ilikuwa na Mambo ya kipuuzi ivi ivi kama CCM lakini ili collapse
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,392
2,000
1. dodoso la utafiti wako lipo wapi

2. Umeenda mikowa ipi itaje? Ilitukuhoji vizuri,

3. Umehoji wangapi kwa ushahidi gani?

4. Nani anadhamini utafiti wako
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,154
2,000
Subiri kampeni zianze mzee.. Nyie si mlifanya kampeni miaka mtano? Sasa wao mezi miwilinita wafunika..
Watanzania sio malifa.
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
6,221
2,000
Kwa bao la mkono ndio lakini kwa haki CDM wanashinda asubuhi asubuhi tu.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,550
2,000
Mkuu, inawezekana umeaminishwa na hata kufikia hitimisho kwa hayo uliyoyaandika kupitia "sample size" ambayo umeitumia, pasipo kujaji uhalisia wala uwakilishi wake kwa jumuiya nzima ya taifa la Tanzania. Nachelea kusema kuwa hukuwa na mtandao mpana wa kukupa taarifa sahihi kwa kadiri ambavyo wewe pia ulihitaji kuzipata.

Mapungufu ya wazi ambayo nayaona ktk mada yako, kwanza kuwa "preconceived idea" ili ikapate kuhitimisha lile ambalo ulikwisha kulikusudia. Pili upo "biased" kwa kuwa inaonyesha upo kimkakati kulinda itikadi ya chama unachokipenda na kuonyesha mapungufu ya vyama vya upinzani.

Lakini jambo la tatu, unapelekeshwa na mihemuko ya "prejudices" ambayo inakufanya uwe "perception errors" kwa yale ambayo unayaamini. Fungua macho yako ili ukapate kuuona vyema nje ya kasha la ufahamu.
 

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,650
2,000
Mkuu chadema wanazubgumzia Tanzania ya twitter na Jf....

Chadema huwa wana jidanganya sana humu
 

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,780
2,000
Mkuu huo ndo uhalisia, Ila tegemea matusi. Wenyewe wanatestigi mitambo kwa kupiga kura Jamii Forums wakiamini ndo hali halisi. Ukiishi mitandaoni waweza kudhani JPM hatakiwi na wananchi kabisa, Ila mtaani ni hali tofauti.
Hahahahahaa
 

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,780
2,000
sasa ulitaka wasemeje wakati wapinzani walipigwa pini kufanya siasa miaka mitano.ngoja mikutano ianze uone watakapoweka uozo wa jpm kama wananchi hawatamgeuka within a minute na nina uhakika hata we utamchukia. Kwanza swala la ajira ndo litamfanya jpm azomewe jukwaani
Sasa wataweka kitu gani tuwaelewe wakati sisi tunaona yaliyofanywa kwa macho yetu?
 

Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,199
2,000
Mkuu huo ndo uhalisia, Ila tegemea matusi. Wenyewe wanatestigi mitambo kwa kupiga kura Jamii Forums wakiamini ndo hali halisi. Ukiishi mitandaoni waweza kudhani JPM hatakiwi na wananchi kabisa, Ila mtaani ni hali tofauti.
Hata mapokezi ya Lissu na maandamano kuelekea makao makuu mlisema ni ya twitter, Facebook na JF.

Mmeona kilichofuata, endeleeni kujipa moyo fisiem.

Bila polisisiem na kubebwa na tume ninyi ni wepesi kama pamba, jiandaeni kukabidhi nchi Chama Cha Majambazi(CcM)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom