Hivi Tanzania tuna waandishi wachunguzi na wachambuzi huru?

kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,802
6,468
Nimekuwa nikifuatilia ishu zinazoibuliwa mara nyingi labda na top leaders ndio inakuwa mijadala rasmi ya media.

Mfano: leo gazeti la uhuru linazungumzia rushwa pale kariakoo, kuna gazeti moja nalo linazungumzia kuhusu aliyekua DC Hai. Yote ni baada ya viongozi kuibua taarifa wao ndio wanapatia pa kuanzia.

Imekuwa pia hata awamu ya 5, waandishi wanapata cha kuandika japo kabla ya kiongozi kusema wao hawakuona kama ni ishu ya kuandika. Ni kweli hatuna waandishi wa kiuchunguzi wenye kuleta hoja hadharani au media zao zimewa-limit au wanaangalia ugali wao?

lakini pia nimejaribu kufuatilia karibu studio nyingi hata zile kubwa nchini kuhusu kualika wachambuzi mfano Rais ameteua ama kuna ugeni nchini huoni kitu cha ajabu walichonacho kama wachambuzi (wa kidiplomasia, uchumi, jamii au wasomi), zaidi watateleza na uhalisia wa muda huo lakini mambo yakibadilika watabadili tena.

Mfano: uteuzi wa MaRAS niliona badala ya wachambuzi kuonesha pande mbili za wateuliwa kutokana na utumishi/uzoefu wao etc, sheria za kiuteuzi, kama kuna makosa ya kiuteuzi (mfano kwanini RAS achague kiongozi wa chama kuja kuwa RAS nk).

Ni kwamba wanaogopa kuudhi watawala au kutokana na maelekezo ya media au wenyewe haiba zao?

Contents walizonazo binafsi sioni sababu ya wao kualikwa studio.
 
Walianza kufunguka kipindi cha Kikwete, Jiwe akaja kuwafinya kwa kutumia vitisho, akawarudisha nyuma hatua nyingi sana, kwa sasa at least wameanza kufufuka kutoka huko mafichoni, tuwape muda kidogo, soon watakamata mwendo mzuri.
 
Walianza kufunguka kipindi cha Kikwete, Jiwe akaja kuwafinya kwa kutumia vitisho, akawarudisha nyuma hatua nyingi sana, kwa sasa at least wameanza kufufuka kutoka huko mafichoni, tuwape muda kidogo, soon watakamata mwendo mzuri
Chombo pekee cha habari kilichokuwa huru Awamu ya 5 ni "Mwahaharakatihuru" Musiba na vijarida vyake kwa hisani ya bwanayule !
 
Wapo wachache kutokana na historia ya nchi yetu, lakini tatizo kubwa ni chombo kipi kitapokea habari hizo za uchunguzi?
 
Naunga mkono hoja, Tanzania tuna tatizo la ukosefu wa wachambuzi mahiri. Waandishi wa uchunguzi wapo, na wachambuzi mahiri pia wapo, tatizo ni

Sasa utashuhudia, habari za uchunguzi kama kinachoendelea Raia Mwema, na utashuhudia wachambuzi mahiri.

P
 
Tanzania huna Journalists bali kuna High Table, PR and Brown Enveloped Journalists.

Journalists wapo Kenya, Uganda, Algeria, Misri, South Africa, Burkina Faso Ghana hapa Afrika.

Nasisitiza hakuna Journalists Tanzania.
Mda mwingine huwa nakuelewa mkuu, ila ukishakunywa ulanzi loooh unakuwa chizi.
 
Naunga mkono hoja, Tanzania tuna tatizo la ukosefu wa wachambuzi mahiri. Waandishi wa uchunguzi wapo, na wachambuzi mahiri pia wapo, tatizo ni ...
Sasa utashuhudia, habari za uchunguzi kama kinachoendelea Raia Mwema, na utashuhudia wachambuzi mahiri.

P
Shikamoo baba, Hata wewe pia unaweza ukawa mchambuzi Bora zaidi kuliko tunavyokutazama leo, ila kinachokuvunjia heshima ya taaluma yako na umahiri wako ni siasa na hasa kutaka kuwa kiongozi wa kisiasa badala ya kutumia ile nafasi ya utaalamu aliokupa Mungu.

Ukweli mkuu unaulewa wa Mambo mengi na tena pengine huenda ukawa mchambuzi Bora kuliko hata tunaowafikiria ila umeamua kujitwisha beseni la takataka kichwani na kutuonyesha kuwa wewe huna uelewa na Mambo, ukweli unaujua mwenyewe kwanini umeamua kuwa hivi ulivyo.
Mungu akusaidie uelewe na utambue karama na nafasi aliokupa Mungu uitumikie badala ya kuwa bendera fuata upepo.

Nisamehe sana maana kwa umri wako sikutakiwa niseme haya ila msema kweli ni mpenzi wa Mungu jaribu kujiangalia baba angu umevaa shati kwa kuligeuza alafu unatuambia upo sawa.
 
Hii inaitwa point blank, na the jf spirit, where we dare talk openly. Nimeipokea hoja yako, maneno yako japo ni makali, lakini ndio ukweli wenyewe, na mtu unapoambiwa ukweli, hata kama ukweli huo utakuuma vipi, inakubidi, uupokee na uukubali. Hivyo nimepokea na nimekubali.

P.
 
Ahsante sana Mkuu nami nilijua kuwa ni maneno makali ndio maana niliomba msamaha mapema na sikuwa na jinsi ya kukwambia ukweli ili moyoni mwangu niwe na amani
 
Ahsante sana Mkuu nami nilijua kuwa ni maneno makali ndio maana niliomba msamaha mapema na sikuwa na jinsi ya kukwambia ukweli ili moyoni mwangu niwe na amani
Uwe na amani kabisa, ukweli wako ni ukweli wa ukweli, mtu mwenye akili akiambiwa ukweli, huwa anauchukulia very positive.
P
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom