Hivi Tanzania tuna muziki ama copy za muziki wa wengine?

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Yaani inakera sana kuona media zinavyosifia eti muziki wetu umekua wakati hatuna muziki wa kujivunia hadi leo. Wasanii wetu wenye majina makubwa karibu wote kazi yao ni kuangalia muziki unaotrend sehemu nyingine za Africa na kuuleta kwetu kuuwekea maneno ya kiswahili, yaani wanatambaa na upepo.

Mara waige wanaija, mara masebene, na sasa hivi ndo kero kabisa karibu kila msanii anataka aimbe Amapiano. Ukiacha muziki hata dance hawajiangaishi kucreate zao, kazi yao kucopy wanigeria na wasouth.

Tumeshindwa hata kuikuza Singeli uwe muziki wetu?

Ni aibu kujilinganisha na watu tunaowacopy, kwa style hii tutaendelea kusubiri sana

S
 
Mziki wetu upo mkuu, taarabu ni yetu na singeli pia imetoholewa kwenye mchiriku,
Tunao mziki wetu ila hatujawekeza vya kutosha
 
Tumalize hili kwanza
JamiiForums114553076.jpg
 
Kiba alikuwa nawaponda sana wanao imba nyimbo zenye beat za kineija, ila yy mwenyewe kaanguka huku huku kishanogewa nyimbo tatu DODO,JELOUS, SALUTE ni beat za Kinejeria.

Huku Wasafi labda Mbosso na upwani wake.
 
Yes Mbosso kajitahidi kukomaa na muziki wake, walau tungestick na hizi ladha za kipwani tungeonekana tuna mziki wetu

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kiba alikuwa nawaponda sana wanao imba nyimbo zenye beat za kineija, ila yy mwenyewe kaanguka huku huku kishanogewa nyimbo tatu DODO,JELOUS, SALUTE ni beat za Kinejeria.

Huku Wasafi labda Mbosso na upwani wake.
Usisahau kibamia ameshusha na NDOMBOLO, muziki ni biashara ukizubaa utaishia kuwa kama akina Barnaba ambao wanaishia kusifiwa kwa talent lakini muziki wao hausongi mbele.
 
Wanaimba usenge Tu hamna kitu....! Mbosso fundi , somehow Zuchu walau ....
 
HATA NAMI HILI NILILIONA NA LINANIKERA SANA.SIJUI KAMA KENYA, UGANDA, ZAMBIA. BURUNDI NA RWANDA WANAIGA HUO MZIKI? SIJUI UNAITWA AMAPIANO. AU NI TZ PEKEE NDIYO TUNAUSHOBOKEA
 
Wasanii hawana ubunifu na ukitoa maoni basi mahsabiki wao watakujia juu kuwa huu ndo mziki wa biashara, lakini wanasahau kuwa biashara ikibebwa na ubunifu inakuwa na maisha marefu na ina chance kubwa ya kuwa na maisha marefu
 
Yaani inakera sana kuona media zinavyosifia eti muziki wetu umekua wakati hatuna muziki wa kujivunia hadi leo. Wasanii wetu wenye majina makubwa karibu wote kazi yao ni kuangalia muziki unaotrend sehemu nyingine za Africa na kuuleta kwetu kuuwekea maneno ya kiswahili, yaani wanatambaa na upepo.

Mara waige wanaija, mara masebene, na sasa hivi ndo kero kabisa karibu kila msanii anataka aimbe Amapiano. Ukiacha muziki hata dance hawajiangaishi kucreate zao, kazi yao kucopy wanigeria na wasouth.

Tumeshindwa hata kuikuza Singeli uwe muziki wetu?

Ni aibu kujilinganisha na watu tunaowacopy, kwa style hii tutaendelea kusubiri sana

S
Singeli ikuze wewe mkuu
 
Mziki wetu upo mkuu, taarabu ni yetu na singeli pia imetoholewa kwenye mchiriku,
Tunao mziki wetu ila hatujawekeza vya kutosha
SIYO KWELI KWMB SINGELI IMETOHOLEWA KWENYE MCHIRIKU. SINGELI IMETOHOLEWA KWENYE TAARABU. WAKINA MSAGA SUMU WALIKUWA WANAIMBA AU KUCHOMBEZA VIJIMISTARI VYAO NDANI YA MDUNDO WA TAARABU. HADIJA KOPA ANAIMBA, HALAFU WANAITIKIA, HALAF KIZAZI KIPYA WANACHOMEKEA MISTARI YAO. MCHIRIKU NA SINGELI HAWAJUANI HAAAATA
 
Wewe unamjua Msaga sumu tuu? Juma Mpogo unamjua? Dogo Jack Simera unamjua? Hao akina msaga sumu walitafuta namna ya kutoka wakatoka ila wasanii wa mchiriku wapo kitambo sana
 
Wakina Dulla Makabila, Man Fongo wakiulizwa kuhusu Singeli wanakwambia bila Msagasumu wasingefika pale. Msagasumu wanamheshimu sana. Kiukweli jamaa alicheza na taarab tu hatimae ikazalishwa Singeli kitu ambacho hata yeye Msagasumu hakujua kama ingefika huko kwakuwa lengo lake lilikuwa kusherehesha kwenye shughuli hasa harusi za Wazaramo, wandengereko and the likes.
 
Wewe unamjua Msaga sumu tuu? Juma Mpogo unamjua? Dogo Jack Simera unamjua? Hao akina msaga sumu walitafuta namna ya kutoka wakatoka ila wasanii wa mchiriku wapo kitambo sana
MIMI SIJAPINGA UWEPO WA MCHIRIKU. NINACHOPINGA NI ILE DHANA KWAMBA SINGELI IMETOKANA NA MCHIRIKU. SINGELI IMEZALIWA NA TAARABU. NIMEANZA KUUJUA MCHIRIKU MIAKA YA 80's. BENDI KAMA TOPAZ, URAIBU, GARI KUBWA, ATOMIC, ENZI HIZO JAKI SIMELA NA DOGO MFAUME HAWAJAZALIWA. MPOGO ALIKUWA ANAIMBA VANGA. MDUNDIKO NA MIGOMA MINGINE YA KIUTAMADUNI
 
Mzee Chaka shikamoo
 
Nilikua nasikiliza amapiano ya Mmakonde, eti anajiita Ticha, wakti wimbo ni copy!
 
Kwa akili zangu ndogo nmeona hv...

Muziki ni sanaa. Sanaa hii imekuwa ni njia kubwa ya kuingiza kipato kwa wasanii wa muziki. Hivyo muziki ni biashara kama zilivyo biashara zingine.

Sifa mojawapo ya biashara n kukidhi mahitaji ya wateja ambapo hapa ni mashabiki wa muziki. Sidhani kama ni akili kukomaa na visingeli ikiwa mashabiki wanashobokea amapiano.

Hii inamfanya msanii kuangalia n mziki upi una soko kwa kipindi husika.
Sioni kama ni tatizo, maana huwezi kuuza viazi vitamu hotelini kisa n chakula cha asili kwako wakati wateja wanahitaji pizza na baga.

So point kubwa hapa muziki umekuwa biashara.
 
Back
Top Bottom