Hivi Tanzania tulipoteza wanajeshi wangapi vita vya Tanzania na Uganda

Ninaukumbuka sana huu wimbo by Zahir Ally Zorro.

Wazazi, wazazi wetu eee
Mashujaa tuliorudi, tumerudi kishujaa
Mashujaa walokufa wamekufa kishujaa
Lengo na nia yetu wazazi lilikuwa moja
Kuilinda hadhi yetu eeh

Kama kuna mwenye hii audio tafadhari naiomba, natamani sana nizikumbuke siku zile.
 
Mkuu, kuna fidia zozote walilipwa familia za wanajeshi waliopoteza maisha vitani?

Hilo la familia sina uhakika, lakini kwa wale waliokuwa mstari wa mbele, Nyerere aliwapa mkono wa shukrani 40,000 Tshs. Zilikuwa nyingin sana ukizingatia kima cha chini kilikuwa kati ya 200-400.
Wengi walirudi na vitu kutoka Uganda. Jeshi halikuweza kuajiri wote na Nyerere alisema tunataka tuwe na jeshi dogo la kitaalamu.
 
Benedict Kiloloma (Ben Kiko) home boy, ndio aliekuwa akitangaza vita vya Uganda, wakati mwingine alikuwa mtangazaji Seleiman Kumchaya pamoja na Dunstan Tido Mhando
Du! Vita ilikuwa inatangazwa kama mechi ya Simba na Yanga!!
 
Vitani sirahisi kupata takwimu sahihi za waliokufa japo wapo wanakufa wakahesabika lakini wengine wakifo hawaonekani japo wengine hukimbilia kusikojulikana.Hata hvyo wanajeshi wetu walirudi wachache walikimbilia ng'ambo kukwepa mapigano na wengine walitekwa.
 
Mkuu, basi hamna ata maiti ziloitambulika na zikahesabiwa wananchi wakatangaziwa?
 
Me pia nimejiuliza ni wanajesh wangapi wa tz walipoteza maisha. Halaf wengine walikuwa vijana wadogo sana walikusanywa na kupewa short time training wakaingia vitani . Kweli nch ilikuwa na uzalendo wa hali za juu.[/QUOTE
Uliza Google utapata idadi teh!!
 
ule uzalendo niliouona jana kwenye ile vita sijui kama utarudi,..leo tz ikivamiwa afu uniambie niende mstari wa mbele sikubali,sanasana nitaside na maadui...
NDIYO MAANA YAKE! Wenye madaraka wameshajimegea nchi,hata akitokea adui wao watatanguliza familia zao nje,Nyerere alifanya kwa vitendo,mwanae nae aliingia vitani.
 
Du! Vita ilikuwa inatangazwa kama mechi ya Simba na Yanga!!
Kijana, nadhani ulikuwa bado ujazaliwa, bahati nzuri ID yako unaonekana mtu wa Kagera, jaribu kumuuliza mzee wako nadhani atakufahamisha
 
Idai ya watanzania waliokufa vitani uganda ilifikia askari 600 waliozikwa katika kambi ya Kaboya. Idadi inaweza kuwa ni zaidi ya hapo maana wengine walizikwa walikozaliwa. Ili kujua idadi kamili ya askari walioathirika kwa kufa katika vita hii inatakiwa kutofautisha kama ifuatavyo:

1. Waliokufa katika mapigano halisi (Died in action)
2. Waliokufa kwa ajali (za magari kupinduka huko vitani)
3. Waliokufa kwa mashambulizi rafiki (Friendly fire) mashambulizi yasiyotoka kwa adui bali nyie wenyewe
4. Wasiojulikana kama wamekufa au wako hai (Missing in action)
5. Waliochukuliwa mateka na kufahamika (POW)
6. Waliotoroka vitani (Desserters)
7. Waliokufa kama adhabu za kijeshi vitani (Marshal court death penalty)

etc.
 
Wanajeshi wa Tanzania pamoja na uzalendo walikuwa nao walivyofika Jinja walipora vitu vingi sana vya raia wa Uganda, pamoja na kuiba magari na vitu mbalimbali na kuja navyo Tanzania

Una ushahidi? Vitu walivyokuja navyo nadhani walinunua kwa allowance walizolipwa huko. JW halijawahi kukosa uzalendo, si unajua tena limeundwa na kukomazwa na makada wa CCM !! Jeshi hili linaweza kuharibika tu pale ikitokea likawa chini ya Rais aliyetoka chama kama CDM.
 
Sidhani kama umetumia Ubongo kufikiria hicho ulichokiandika hapo. Bila shaka Umetumia Uti wa Mgongo, kwa wale wanaoelewa biology kidogo. Napenda kujua elimu yako ni ya kiwango gani tafadhali!!?

Form 6 PCB, halafu mafunzo ya itikadi kutoka Chuo cha Chama Kivukoni, halafu shahada ya pili ya uhamasishaji umma na propaganda za kisiasa kutoka Bucharest Romani. Pia nimehudhuria warsha mbali mbali katika miji ya Pyong yang, Havana, East Berlin, Odessa, Peking, Belgrade na Leningrad. Kwa hiyo siyo tu nafikiri kwa kutumia ubongo, bali natumia ubongo ulio makini.
 
Una ushahidi? Vitu walivyokuja navyo nadhani walinunua kwa allowance walizolipwa huko. JW halijawahi kukosa uzalendo, si unajua tena limeundwa na kukomazwa na makada wa CCM !! Jeshi hili linaweza kuharibika tu pale ikitokea likawa chini ya Rais aliyetoka chama kama CDM.
Mkuu. ushahidi upo mimi binafsi niliona wanajeshi wakipokelewa Mwanza wakiwa na vitu mbalimbali, vilevile walikuja na magari na pikipiki zina namba za Uganda, wakigawa biskuti kwa wanafunzi walikwenda kuwapokea
 
Pikipiki, magari, radio...etc walinunua kutoka kwa Waganda. Kama vingekuwa vya wizi visingeruhusiwa kuletwa.
Wapo wachache waliojaribu kupora, waliadhibiwa vikali na vitu walivyokutwa navyo vikarudishwa kwa wenyewe.
 
Uzalendo uliooneshwa kipindi hicho haijapata kutokea watu waliipenda nchi yao haswa.
 
Uzalendo uliooneshwa kipindi hicho haijapata kutokea watu waliipenda nchi yao haswa.
Mkuu huyu mwenye bandiko anauliza idadi ya askari mashujaa wetu waliokufa katika hii vita. Naona muda umepita lakini jibu bado hajalipata.
 
Back
Top Bottom