Hivi Tanzania One wako wapi, wale walioongoza kitaifa Form Six na Form Four?

yuda75

JF-Expert Member
Aug 16, 2020
520
1,377
Wako wapi vijana waliojichukulia ujiko wa zawadi na headlines magazetini na vyombo vya habari wako wapi kaka zetu na dada zetu waliotesa kwa ufaulu wa kutisha?

Wako wapi jamani? Tusaidiane.

Je, wapo chimbo wanajifua kuvunja record zao wenyewe?

Je, wako wanasoma na kujiendelezakimataifa?

Je, serekali imewatupa mkono kimasomo au vyomba vya habari vimewasahau?
 
Wote walipata skolashipu kwenda nje ya Tanzania kusoma. Wamebakia hukohuko wanajiendeleza kielimu.

Wengine waliorudi nchini wanakeep low profile wako na wake/waume na watoto wao wanaingiza kipato kinachowatosha kumudu gharama za maisha na kutoa sadaka kanisani na misikitini.

Hii ni kwa ambao nna taarifa nao, ambao sina taarifa zao ukienda TAMISEMI utapata kila hatua waliyopitia.

Alamsiki.
 
au na wewe umo
Ni matani tu mkuu. Tucheke na kufurahi!

Tanzania One wote hawa walipaswa kuangaliwa na kuendelezwa kwenye fani zao walizochagua mpaka wafikie mafanikio yao ya kitaaluma. Sitashangaa kuona kama wengi wao huishia kwenda kusoma nje na kupotelea huko. Hawa wangefaa sana hata kuwa maprofesa kwenye vyuo vyetu watunolee kizazi kijacho!
 
Wote walipata skolashipu kwenda nje ya Tanzania kusoma. Wamebakia hukohuko wanajiendeleza kielimu.
Tupo ndio tunawezesha maisha bora kwako na kwa wananchi wengine kufanya maisha yawe rahisi.
 
Wote walipata skolashipu kwenda nje ya Tanzania kusoma. Wamebakia hukohuko wanajiendeleza kielimu.

Wengine waliorudi nchini wanakeep low profile wako na wake/waume na watoto wao wanaingiza kipato kinachowatosha kumudu gharama za maisha na kutoa sadaka kanisani na misikitini.

Hii ni kwa ambao nna taarifa nao, ambao sina taarifa zao ukienda TAMISEMI utapata kila hatua waliyopitia.

Alamsiki.
Dolla_Mbili soma hapa Kasie alivyoandika!
 
Back
Top Bottom