Blackafrica
Senior Member
- Jun 26, 2021
- 141
- 401
Nimejikuta najiuliza hilo swali, swali ambalo naamini wananchi wengi wafanyabiashara na wakulima wamekuwa wakijiuliza. Baada ya kumaliza chuo kwa msaada fulani niliopata, niliamua kujihusisha na shughuli za kilimo kununua na kuuza mazao lakini vile vile kulima.
Haya mambo ya kilimo, ukisimuliwa ni rahisi kudhani yana faida, lakini ukweli ni kwamba kilimo cha Bongo ni kilimo cha kijanja janja, kuanzia kwa mkulima mpaka mfanyabiashara. Haya makundi mawili kila kundi lina wakati wake wa kulia lakini wakati mwingine makundi yote hulia kwa pamoja.
Najua unashangaa lakini ndio ukweli wa mambo ulivyo wakati mkulima analima kwa shida shambani, mfanyabiashara anakuja kulangua mazao kwa bei ya chini hapo ni kilio cha mkulima. Wakati mwingine kukiwa na uhaba mfano kwa sasa alizeti ipo juu hapo mkulima anapeta, lakini maajabu ni wakati mwingine mkulima kuuza mazao yake kwa bei ya chini na mfanyabiashara kukosa soko la kuuza mazao yake mfano kwa sasa mpunga na mahindi yako bei chini soko la kuuza hakuna, hapo makundi yote mawili yanateseka kuanzia mkulima mpaka mfanyabiashara.
Swali je Wizara ya kilimo ipo? Na kama ipo kazi yake nini? Kweli inashindwa kutafuta masoko ya wakulima? Kweli hii wizara inashinda kutengeneza mazingira ambayo yatamsaidia mkulima kupata faida lakini pia mfanyabiashara kuuza kwa soko la uhakika lenye faida.
Katika utafiti wangu nimegundua asilimia kubwa ya wakulima Tanzania hutegemea soko la ndani, hili soko la ndani limeshikwa na watu wachache ambao ndio wanafaidika nalo na mkulima hufaidi kidogo sana, leo hii ukijitutumua wewe mkulima au mfanyabiashara ukatafuta soko la nje ya nchi utakwama tu na itafika mahari utajiuliza hivi hii nchi ya Tanzania ina Wizara ya kilimo kweli?
Kwa taarifa tu Wakulima wengi wa Tanzania tunashindwa kuuza mazao yetu nje ya nchi kwa sababu hatuna mikakati au mbinu ya kushindania bei ya kimataifa (international price) leo hii ukitaka kuuza zao lolote la kilimo nje ya nchi kitu cha kwanza cha kuzingatia lazima upange bei ambayo inaendana na bei ya kimataifa, yaani kama mahindi katika soko la dunia yanauzwa sh 100 kwa kg basi itakulazimu na wewe kuuza kwa kg mahindi yako kwa sh 100
Hili ndio tatizo lako ambalo linahusiana na bei ya kimataifa tatizo la pili ni uwingi quanitity mara zote ukitaka kuuza mazao nje ya nchi lazima uwe na msuri wa kutosha wa kuwa na mzigo wa kutosha, yaani kama ulizoea soko la ndani kuuza tone mia tano au elfu moja ya mchele usijidanganye kulitaka soko la kimataifa huko wanaanziaga tone ya chini sana ni tone elfu kumi kuendeleaaaaa!
Sasa najiuliza sana Wizara ya kilimo ipo? Na kama ipo kazi yake ni nini? Maana mapungufu makubwa yanayotokea kwenye sekta ya kilimo yanasababishwa na hii wizara kutoshiriki ipasavyo katika kuinua kilimo, ambapo kilimo pekee tu kama hii serikali yetu ingekuwa serious kingetosha kujenga uchumi wa nchi hii, kwa mwananchi mmoja mmoja mpaka Taifa nzima.
Tunakwama kwa sababu tuna kilimo cha hovyo mikakati ya hovyo sera za kilimo za hovyo, lakini vile vile tumeruhusu watu wachache wanufaike na mfumo wa hovyo wa kilimo uliopo sasa na ndio maana unaona mara mkulima analia mara mfanyabiashara analia wakati mwingine wanalia wote je wizara haiyaoni haya? Je wizara haiyajui haya? Lakini je wizara haina uwezo wa kuyatatua haya? Ukijiuliza yote hayo itafika sehemu utajiuliza wizara ya kilimo kazi yake ni nini? Tutafakari kwanza haya afu nitaludi tena.
Kila jambo lina mwisho wake mwambie na mwenzako.