Hivi Tanzania inahitaji kununua umeme toka Ethiopia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Tanzania inahitaji kununua umeme toka Ethiopia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kamkoda, Oct 19, 2012.

 1. k

  kamkoda JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 396
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [h=2]Mameneja 29 Tanesco wasimamishwa kazi kwa hujuma[/h]


  Na John Ngunge  19th October 2012
  Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud


  Mameneja 29 wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wameshimamishwa kazi baada ya kuhusishwa kuhujumu utendaji wa shirika hilo kwa kuunganisha umeme kinyume cha utaratibu, wizi wa mafuta ya transfoma na nyaya za umeme.

  Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema hayo jana jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati yao ya kutoa huduma bora kwa wananchi na operesheni inayoendelea nchini kote ya kuwasaka watu wanaojiunganishia umeme kinyemela.

  “Tanesco ya sasa siyo ile ya zamani. Tunajisafisha na tayari wapo waliochukuliwa hatua na wengine kusimamishwa,” alisema lakini akakataa kutaja majina ya vigogo waliosimamishwa.

  Alisema waliosimamishwa kazi ni wenye vyeo vya umeneja na maofisa.

  Akizungumzia hali ya umeme nchini, Badra alisema hakutakuwa na mgawo wa umeme kwa sababu sasa hivi Tanesco haitegemei zaidi umeme wa maji, isipokuwa wanatumia umeme wa mafuta na gesi.

  “Hakuna mgawo na hatutarajii kuwa na mgawo. Sasa hivi tunatumia umeme wa mafuta na gesi,” alisisitiza.

  Kuhusu kukatika kwa umeme katika baadhi ya mikoa, alisema hiyo inatokana na sababu za kupanga wenyewe ili kuruhusu kufanya marekebisho katika njia za umeme au wakati mwingine inatokana na sababu tofauti kama vile mvua za radi, upepo, kukatika kwa miti kunakosababisha kuharibu mfumo wa usambazaji umeme au hata gridi ya taifa kupata matatizo ya kiufundi.

  Katika hatua nyingine, Badra alisema Tanzania inafanya mazungumzo na serikali ya Ethiopia ili kuangalia uwezekano wa kununua umeme kutoka nchi hiyo.

  “Njia kuu za kusafirisha umeme zitakapounganishwa na kukamilika, nchi yetu itaweza kununua umeme unaozalishwa kwa njia ya maji na unaouzwa kwa bei nafuu moja kwa moja kutoka nchi kama Ethiopia,” alisema na kuongeza:

  “Ethiopia wanazalisha nishati ya umeme megawati 10,000 na kubakiwa na ziada ya megawati 8,000.”

  Alikuwa akizungumzia mkutano wa mawaziri wa nishati wa nchi za Afrika Mashariki na Kati kuhusu mtandao wa usambazaji wa nishati hiyo unaojulikana kama Eastern Africa Power Pool (EAPP) unaozihusisha nchi 11 za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Djibout, Ethiopia, Libya, Jamhuri ya Sudan na Misri.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Dhuks

  Dhuks JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 1,471
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 180
  Kama umeme unaozalishwa Tz haukidhi mahitaji yote sioni kosa kununua toka nje.
   
Loading...