Communist
JF-Expert Member
- Jun 1, 2012
- 5,400
- 1,181
Kwa mujibu wa Mwananchi (2013), Maoni hayo yanatolewa wakati juzi Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt alitaja sababu za Obama kuja Tanzania kwamba ni kutokana na sifa nzuri za Tanzania. Sifa hizo zilizomvuta Rais Obama ni utawala bora, demokrasia na mazingira bora ya uwekezaji yanayosabisha kukua kwa uchumi.
Balozi wa Marekani alisema Tanzania ni nchi ya mfano linapokuja suala la uongozi bora na ndiyo maana imekuwa na amani, utulivu kwa muda mrefu ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Napata wasi wasi sana na hizi sifa za kutuvimbisha vichwa ili tuibiwe vizuri. Yaani hayo, maePa, Meremeta, Rada, Mauswisi ndio huyu jamaa anatusifia?
Yaani aache kwenda Rwanda kwa sifa hizi aje hapa kwa wezi wakura. Bado namkumbuka jamaa aliekuwa anakimbia na box la kura kule Segerea. (Utawala Bora?)