Hivi Tanzania daima wana uhusiano na Gazeti la Hoja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Tanzania daima wana uhusiano na Gazeti la Hoja?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TUMBIRI, Dec 20, 2011.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimesoma habari kuu ya leo kutoka Tanzania daima nimeona kuna mahala imeandikwa kwamba Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo Ndugu Absalom Kibanda jana alidhaminiwa na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Hoja Ndugu Yasin Sadiq.

  Sehemu ya gazeti inasomeka hivi "Hata hivyo, katika hatua isiyo ya kawaida, huku wakijua kwamba bado ana dhamana, polisi walimzuia tena Kibanda akiwa na mawakili wake Nyaronyo Kicheere na Juma Thomas, wakamlazimisha awe na mdhamini mwingine kwa kiasi cha sh milioni tano. Mhariri Mtendaji wa gazeti la Hoja, Yasin Sadiq, alimdhamini ". Binafsi nimekuwa nikiyasoma magazeti yote mawili na nilichogundua ni kuwa kila gazeti lina itikadi zake zinazopinganza na lenzake. Hoja siku zote wanawatetea watuhumiwa wa Ufisadi na limekuwa likiponda hata Makala zinazochapishwa na Tanzania daima.

  Mfano kuna kipindi Naibua Mhariri Mtendaji wa Tanzania daima ndugu Ansbert Ngurumo akiwa Uingereza (Hull University) kimasoma alichafuliwa na Gazeti la Hoja kwamba anaiponda serikali ya JK kwa kuwa alitoswa kwenye uteuzi wa Ukuu wa Wilaya. Lakini nimeshangaa sana kusoma kuwa Jana Mhariri Mtendaji wa Hoja amemdhamini Mhariri wa Gazeti pinzani lake katika kesi yake ya Uchochezi inayomkabili.

  Source:
  Siri yafichuka kukamatwa kwa Kibanda
   
 2. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Na Saeed Kubenea alivyomdhamini juzi nalo linauhusiano na Tz Daima? Jitizame upya tena
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Mbona hushangai JK kumteuwa Samuel Sitta kuwa Waziri!!?
   
 4. Y

  Yetuwote Senior Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna tofauti kubwa kati ya "Kibanda vs Sadiq" na Tanzania Daima vs Hoja.
   
 5. m

  mob JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  ndugu zangu tuache kudiscuss watu ila tuweke utaifa juu
   
Loading...