Hivi TANROAD mikoani mnafanya kazi gani?

kasanga70

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
212
489
Hakuna kitu mnanikera kama mashimo yaliyoko lami ambayo yanadumu mwaka mzima.

Mashimo yanaharibu gari, yanasababisha ajali mbaya Sana na kupunguza uzalishaji na nguvu kazi ya Taifa. Juzi nimepita njia ya Iringa Dodoma.

Mashimo yaleyale niliopita mwaka juzi nimekuta yameongezeka hasa hasa mkoa wa Iringa kuanzia Njiapanda ya Tosa hadi Mtera; kagueni kuna mishimo kibao humo mnataka hadi waziri apate ajali ndio mje myazibe siyo?

Mnaudhi sana kwa kweli.
 
Mimi napendekeza issue ya ukaguzi wa barabara wa-subcontract kwa Wachina. Those people are hard workers, serious, and cheap. Kitengo cha inspection kiondolewe na wafanyakazi wake wawe redundant.
 
Mimi napendekeza issue ya ukaguzi wa barabara wa-subcontract kwa Wachina. Those people are hard workers, serious, and cheap. Kitengo cha inspection kiondolewe na wafanyakazi wake wawe redundant.
Wakapewe majukumu mengine hivi unakaaje na shimo katikati ya lami miaka 2? Na sheria zilivyokuwa za ajabu....ukikutwa unaziba au kulifukia hilo shimo unakamatwa.

Dunia ngumu sana
 
Hadi Rais aseme ndo wataamka sahizi yanalipwa bure tu.
 
Hadi Rais aseme ndo wataamka sahizi yanalipwa bure tu.
Waziri aliepita hakwenda na speed ya Jiwe Sasa huyu nae ni kama amelala usingizi wa pono. Ngoja tuirecord hiyo mishimo tuitume kunako majambos....hizo mbio zakeee
 
Nilitembelea Mkoa wa Mbeya. Kwa kweli Mkoa unatia huruma. Barabara ni moja tu! On the way to Zambia! Sasa hiyo congestion ya magari utacheka.
 
Back
Top Bottom