Sijui ni umeme umejizima wenyewe au mmekata makusudi au mnafanya ukarabati, ila umeme umekatika na kurudi mara ya tano kuanzia saa nane usiku hadi sasa saa kumi usiku. Jamani mtasababisha watu wafeli mitihani mtu ameamsha anapiga msuli wake usiku mnamkatia umeme ovyo ovyo. Na hapa ninapoongea ni giza balaa. Huu ni uzembe usio na mfano.
Haiwezekani umeme mnatumia vifaa kutoka Ulaya, Marekani, Japan nk, power stations mnazotumia, sub stations, grid lines, transformers ni zilezile zinazotumika Ulaya na Marekani inakuwaje wao umeme wao haukatiki ila nyinyi kila saa unakatika au mnashindwa kuvitumia vifaa mlivyouziwa? Wenzetu wakikata umeme ujue kuna janga maalum kama vile California juzi walikata baadhi ya maeneo kwa sababu kulikuwa na bush fires, ila wao suala la umeme kukatika kizembezembe haiwezekani, nyie wenzetu mkijiskia tu mnakata bila kujua athari mnazotupa sisi watumiaji ambao tunaathirika kiuchumi na kisaikolojia kutokana na kukaa gizani. Imagine nimekaa macho usiku huu wa manane naandika hapa niko gizani nimezungukwa na wachawi athari ninazo pata kisaikolojia mngejua tu.
Kuna haja Rais kuliangalia hili shirika upya. Alafu unakuta mtu eti kasoma Marekani alafu viswitch vidogo vinamshinda ku operate. Mmejazana mandugu humo kwa kujuana shirika hamliwezi kuliendesha. Haiwezekani vifaa vile vile mnavyoagiza Ulaya kwetu viwe vibovu kila siku wakati wao huko kwao hawajui umeme kukatika. Tatizo lenu ni utaalamu mdogo wa ku operate hivyo vifaa hamna excuses.