Nimekuwa nikifuatilia matangazo ya TBC1 wamekuwa wapenzi sana wa wa kutumia neno habari mpasuko. Sijui wamepata wapi kiswahili hiki? Nionavyo kuna makosa. Ilipaswa watumie 'Habari motomoto'. Hawapaswi kutumia tafsiri sisi kwa neno hilo.
Kuita habari mpya sio sawa sana kwa vile siyo kila habari mpya itakuwa na mvuto kwa jamii. Mfano. Diwani/mbunge hata yeyote kuhudhuria mahafali sio 'breaking news' kwa tafsiri yangu siyo habari motomotoMimi nadhani wangetumia neno "Habari mpya!!" tatizo lao wameona wanatafsiri neno moja moja.
breaking news ni "HABARI TIKISO".mia
Mimi nafikiri wangesema habari mpya kwani breaking news ni ile ambayo haikupangiliwa ila imetokea kama tukio la ghafla na lina umuhimu kwa jamii
Habari zilizojiri peke yake haitatosha labda iwe 'habari zilizojiri punde'
Tafsiri nzuri mimi naona ni 'habari zinazoingia sasa hivi'. Kusema habari mpasuko ni kutafsiri neno kwa neno kitu ambacho wakati mwingine hupotosha maana.
Nina mashaka na hao wataalamu wao wa lugha hapo TBC. Siyo kila kitu lazima kitafsiriwe neno kwa neno.