Hivi tafsiri ya 'Breaking news' ni 'Habari mpasuko'?

Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
660
298
Nimekuwa nikifuatilia matangazo ya TBC1 wamekuwa wapenzi sana wa wa kutumia neno habari mpasuko. Sijui wamepata wapi kiswahili hiki? Nionavyo kuna makosa. Ilipaswa watumie 'Habari motomoto'. Hawapaswi kutumia tafsiri sisi kwa neno hilo.
 
umoto moto wake ni nini, tetea hoja yako..kwanini moto moto??
 
umoto moto wake ni nini, tetea hoja yako..kwanini moto moto??

umoto wake ni kwamba hiyo habari itakuwa na msisimko kwa jamii na kila mtu atapenda kuiona au kuisikia. Ni kama vile ukisikia kikao kilikuwa cha moto.
 
Mimi nadhani wangetumia neno "Habari mpya!!" tatizo lao wameona wanatafsiri neno moja moja.
Kuita habari mpya sio sawa sana kwa vile siyo kila habari mpya itakuwa na mvuto kwa jamii. Mfano. Diwani/mbunge hata yeyote kuhudhuria mahafali sio 'breaking news' kwa tafsiri yangu siyo habari motomoto
 
breaking news ni "HABARI TIKISO".mia

Ni kweli tunakaribia kupata maana kuliko ule ukakakasi wa TBC1 mpaka unajiuliza hz tafsiri za shule ya msingi wamezipata wapi! 'HABARI TIKISO' nakubaliana na wewe kabisa. Labda ungefafanua kdg ili kuelewa msingi wake.
 
Mimi nafikiri wangesema habari mpya kwani breaking news ni ile ambayo haikupangiliwa ila imetokea kama tukio la ghafla na lina umuhimu kwa jamii
 
Mimi nafikiri wangesema habari mpya kwani breaking news ni ile ambayo haikupangiliwa ila imetokea kama tukio la ghafla na lina umuhimu kwa jamii

Mfianchi namie hasa nilitaka kujua kama habari imetokea ghafla na haikupangiliwa itaitwa vipi? Kwa vile wenzetu wa TBC1 ndin huitwa habari mpasuko
 
kuna media moja hupenda kusema "Habari zilizotufikia hivi punde" binafsi ningesema habari zilizotufikia ghafla!
 
Tafsiri nzuri mimi naona ni 'habari zinazoingia sasa hivi'. Kusema habari mpasuko ni kutafsiri neno kwa neno kitu ambacho wakati mwingine hupotosha maana.

Nina mashaka na hao wataalamu wao wa lugha hapo TBC. Siyo kila kitu lazima kitafsiriwe neno kwa neno.
 
upo sahihi.
 
Back
Top Bottom