Hivi swala la umeme watanzania tumelogwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi swala la umeme watanzania tumelogwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumishi Wetu, Oct 17, 2011.

 1. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Natumaini wadau wote wa JF hamjambo!!!!!!!

  Jana jumapili nilifuatilia mdahalo wa umeme Star TV Dar, nikagundua kumbe si TANESCO wala Serikali yaanai wizara yenye mkakati wa kudumu kuondoa kero za umeme!!!!!!!!!!! Mipango iliyopo ni ya zima moto tena kwa gharama kubwa yaanai umeme wa mafuta!!!!!!!!!!!!! Sasa wanasiasa kama Mheshimiwa January Makamba na mwenzake Zito Kabwe pamoja na lawama zao kwa Serikali lakini hawakuonyesha msisitizo wowote wa kujikwamua swala la umeme!!!!!!!!!!

  Nilishawahi kutoa thread hapa ingawa watu hawakuchangia kuhusu umeme wa maji!! Inaonyesha kabisa hawa wanasiasa na wataalamu wetu hawana nia ya kufunga mitambo ya maji Hydro Eletric Power Generating systems.Chukua mifano ya Uganda wamefunga mitambo eneo la Bujagari falls, hiyo ni new venture mbali na Jinja Hydro Power Station!

  Maji ya Jinja ni ziwa Vctoria source yake ni mto Kagera, huo mto unategemea utakauka lini waache kuzalisha umeme wa maji? Tuna mto Kagera, Mto Rufiji ambao unaunganishwa na Kilombero na Kihansi maji mengi tuu!

  Hawa wanasiasa na wataalamu wetu wamelishwa uongo wa mafisadi, eti mito yetu itakuka, kweli mito mikubwa ikauke hivi hivi bila environmental disaster?

  Mafisadi na wawekezaji uchwala wengi ni wa hapa nchi kwetu wameona Tanzania ni shamba la bibi, hivyo wanaona ni bora watumie kiini macho cha utafiti njaa ili waendelee kuuza umeme wa mafuta unaofilisi nchi yetu kiuchumi!

  Hivi tumelogwa sote hatuoni hilo, gharama za kufunga hydro power na uzalishaji wake ni ndogo lakini wanataka waendelee kuuza umeme wa majenerator sijui Syimbion Power, IPTL, Agreco na wengine wanaokuja kwa bei kubwa ili kufilisi nchi kwa umeme wa mafuta!!!!!!! Kwa njia hii kweli nchi itajikwamua kiuchumi?
   
 2. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Swala kubwa hapa ni jinsi gani tutaepukana na umeme wa mafuta (magenerator) maana umeisha onekana kuwa ni wa aghari na ni mzigo kwa uchumi wa nchi yetu?
   
 3. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wa bongo wanaangalia only 10%
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Ndugu zanguni mambo yanayohusu UMEME mimi sijui hata naona kama imekuwa kama jambo la kawaida kwa Watanzania na Mi naona kuna muda kapo ya Watanzania wazelenndo wakichafukwa na mioyo mimi nadhani serikali tawala itakuwa katika wakati mgumu sana. Na katika mtiririko wote huu wa uzalishaji umeme wa maji, hawataki hata kuona wala kusikia kwani wameona si wazalendo tumekuwa lala lakini siku si nyingi wataja shangaa na roho zao.
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kimsingi, watanzania tunapaswa kuachana na hawa mavuvuzela. Hawana mipango yoyote. Tunapaswa kuangalia vyanzo vingine vya nishati na kwangu mimi naona nishati rahishi ni windi generators na solar powers. Tukiwa na vyanzo hivi vya nishati, TANESCO automatically itakufa kwani itakosa wateja. Kwani mteja mkubwa atakuwa serikali na migodi. Wateja hawa kwa kawaida hawailipi TANESCO hivyo itakufa tu. Hebu tuwe smart. Jua tunalo la kutosha na upepo upo wa kutosha kwa nini tunahangaika namna hii. SIDO wanatengeneza windi generators kwa hiyo si kwamba hatuna nishati mbadala bali ni mazoea tu.
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,811
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Wewe mtoa HOJA, ungekuwa kwenye kamati ya kutafuta mwekezaji wa Umeme Tanzania, je ungeikataa 10% ambayo inafikia karibia 5 billon juu ya meza kaka? cha msingi sote tujichunguze -- tumekosa uzalendo. Na nchi inayopoteza uzalendo miongoni mwa wananchi wake ni nchi ambayo ni mfu, nchi ambayo wananchi wake wamekata tamaa - ndiyo sisi Watanganyika.

  Waliotufikisha hapa lazima tuwalaani vikali yaani tumekuwa Taifa la Wachuuzi, Taifa Tegemezi, Ubinafsi -- umimi ndiyo umetawala. Si kwenye sekta ya umeme tu, kote kote hali ni mbaya sana.
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,811
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  kaka Tanesco ipo chini ya Wizara ya nishati na Madini, hata ukikwepa vipi lazima mbele ya safari kuna Politics ndugu yangu. Siasa ndizo zinaua uchumi wa nchi hii.
   
 8. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280

  hawa watu wana makampuni ya kuagiza mafuta sasa watengeneze hydro wale wapi na vizazi vyao. Umesahau reli ya kati walivyoiua!!! Sasa malori tele tele. Mungu awalaani wote ukimwondoa Nyerere, basi.
   
 9. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mafaili ya utafiti yamekaliwa mkuu, hawataki kabisa kusikia, kama maji yatakwisha kwani gesi au mkaa wa mawe hauishi?????????
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Nashukuru ndg yangu FUSO,ila mimi binafsi najua kuchukua rushwa ni laana hivyo nimwiko kuchukua rushwa!!!!!!!!Hiyo laana itageukia hadi kizazi chako chooote!!!!!!! Ndio maana tunasema katiba mpya iunde kitengo cha maadili cha kitaifa, integrity center itakayo vet kuanzia viongozi kama wabunge hadi watawala wote!!!!! Ili tupate watu wenye maadili mazuri, mbona wenzetu Kenya wameweza waliofanya maovu wanapelekwa mahakamani!!!!!!! Tukianza kujiheshimu tutaheshimu nafasi zetu kuepuka aibu ya kufungwa na kufilisiwa!!!!!!!
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kama tunajua hilo sasa ni wakati wa kuamka tutetee taifa letu through dialog!!!!!! Kama ni hivyo hawa watu wa serikali hii wanakitu wanaficha kuhusu umeme ILI WAENDELEE KUIBIA TAIFA LETU!!!!
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mtumishi Wetu! Hawa magamba walioko hewani hapa Inchini hawaoni wala hawasikii. Wao wameona kula na kunywa ndiyo mwisho wa haya maisha. Wanajilimbikiza matrilion ya Tsh ikiwa ni majasho ya walipa kodi lakini hakika kufa itawakuta tu kama ilivyoada ya kifo na matrlioni ya Tsh wanaojiwekea kwa ajili ya watoto wao hakika nao hawataifaidi kamwe na watakuwa wamewaachia laana. Ila iko siku na haiko mbali UKOMBOZI utakuja.
   
 13. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kweli Bwn LiverpoolFc watajuta maana siku za mafisadi zinahesabiwa, Watanzania walio wengi wameshachukia huovu!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...