Hivi SUMATRA wapo kazini au likizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi SUMATRA wapo kazini au likizo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kashaija, Apr 24, 2009.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Miezi kadhaa iliyopita SUMATRA walitangaza kushuka kwa nauli za mabasi zikiwamo daladala ambapo safari zilizonyingi ndani ya Dar ni Tsh. 250/=.

  Madreva wa daladala kwa kujua kwamba SUMATRA ni viongozi tu wa maofisini ambao hawatoki nje kuangalia hali ikoje wakaanza kutumia mwanya huo kujinufaisha zaidi, sasa wanachofanya ni hiki kifuatacho:

  Mfano, safari ya kutoka Mwenge kwenda Tabata kwa mujibu wa SUMATRA inatakiwa kuwa Ths 250/= lakini kwa sasa ni Tsh. 600/= au zaidi. Maana kuanzia saa 11 jioni na kuendelea huwezi kupata gari la moja kwa moja (Mwenge - Tabata). Kinachofanyika ni kukatiza route, (Mwenge - Ubungo) Tsh. 200/=, gari hilo hilo likishashusha, linasogea mbele kidogo tu linaanza kupakia (Ubungo - Tabata dampo) Tsh. 200/=, baada ya kushusha linasogea mbele kidogo linaanza kupakia (Tabata dampo - Segerea/Kimanga) Ths. 250/=.

  Hivyo abiria huyu aliyetoka Mwenge kwenda Tabata anajikuta ameshalipa Tsh. 650/= badala ya Tsh. 250/=. Vile vile mtu huyu anapata adha zaidi ya kutembea umbali mrefu kidogo ambao siyo wa lazima kufuata gari hilo hilo lililomshusha muda mfupi uliopita. Na pia tatizo hili limechangia kuongeza msongamano wa watu kwenye baadhi ya maeneo kama vile Ubungo, ikifika saa moja eneo la Ubungo linakuwa na watu wengi sana kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

  Nasema sasa wakati wa SUMATRA kutoka maofisini kwenda site umefika.
   
 2. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2009
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Ni hali ya kusikitisha kuona, kwamba hali ya usafiri katika jiji la DAR-ES-SALAAM inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

  Leo hii wananchi wanaotumia usafiri wa daladala wanatumia masaa mawili hadi matatu njiani kwa safari ya dakika ishirini hadi arobaini na tano .

  ni vigumu kuamini kuwa katika nchi masikini kama ya kwetu muda unakuwa hauthaminiwi. jiulize ni kiasi gani cha pesa serikali imepoteza kutokana na watu kutowahi makazini kutokana na usafiri duni katika jiji la DAR-ES-SALAAM .

  Watu wanapoteza muda kusubiri magari, muda ambao wangeutumia kufanya shughuli nyingine za muhimu kama kusimamia homework za watoto wao, ama hata kuimarisha familia zao kwa kupata muda extra wa kuspend nazo, ama kuongeza kipato cha ziada, au hata kufanya mazoezi ya kuimarisha afya zao.

  Ni jambo la ajabu kuona Sumatra wanashindwa kusimamia vitu vidogo kama kuhakikisha wenye daladala wanafuata route zao.

  KITENDO CHA KUONDOA VIPANYA KATIKATI YA JIJI BILA YA KUWA NA ALTERNATIVE SOLUTION YA USAFIRI NI MISTAKE KUBWA SANA.so far tatizo la msongamano wa magari bado lipo, ila wasio na magari binafsi ndo sasa tunzaidi kusuffer.

  kitendo cha kuondoa vipanya ili eti kupunguza msongamano wa magari, kilikuwa ni kitendo cha kuwasaidia wenye magari wachache bila kujali adha ya wasio na magari walalahoi ambao ndio wengi.

  katika msongamano wa magari, gari mbili saizi ya mark two ambazo mara nyingi huwa na mtu mmoja au wawili ndani, zinaoccupy nafasi ya hiace(kipanya) kimoja chenye kubeba watu kumi na tano ndani. sasa watu wanne wanaziba nafasi ya watu kumi na tano, then unaona solution ya msongamano wa magari ni kuondoa hii yenye kuchukua watu wengi na kuacha ile yenye watu wachache.

  ni lazima tukubali ukweli kwamba kwa Umasikini wetu tuna limited resources ya vitu vingi sana zikiwemo bara bara. kutokana na tatizo hili inapasa resources zetu zitumike kuwafaa walio wengi zaidi. kama tukikubali ukweli huu PUBLIC TRANSPORT IPEWE KIPAUMBELE ZAIDI KABLA YA MAGARI YA WATU BINAFSI.

  kutokana na msongamano wa magari kuwa mengi katika jiji la beijing nchini China, serikali iliamua kwamba Magari yabadirishane siku za kuingia barabarani. iliweka utaratibu kwamba kama ukiendesha gari mathalan siku ya jumatatu basi jumanne wewe huendeshi mpaka jumatano, hivyo hivyo katika mtindo wa mbadirishano wa siku moja moja. siku ambayo mtu haruhusiwi kuendesha gari lake basi anakuwa anatumia public transport.

  sasa hivi kila mtu Dar-es-salaam mwenye kuingia kwenye Middle class anawaza kununua gari, jambo ambalo ni zuri sana na la maendeleo, lakini ukweli ni kwamba barabara zetu hapa Dar ni nyembamba, nyingine hazina viwango bora,na cha kusikitisha zaidi barabara hizi ni chache, hivi ni kweli katika hali ya namna serikali inashindwa kuipa priority PUBLIC TRANSPORT yenye kuhudumia watu wengi?.

  Juzi Serikali imetangaza kwamba mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi hauwezi kutekelezwa mwakani. kwa maana hii sisi Wakazi wa Mkoa wa dar-es-salaam tutaendelea kuumia tu kwa muda usiojulikana, yawezekana ni makumi ya miaka megine tena, who knows!

  SUMATRA inabidi wawe na short term solution zifuatazo:
  1: punguzeni magari binafsi yanaoyoingia city centre(hata kama jiji litakosa hizo pesa za parking, so far kwanaza hatujui huo mradi wenyewe wa parking unatunufaisha vipi sisi walalahoi wa mkoa wa dar-es-salaam) na badala yake incourage public transport zinazoingia katika sehemu hizo, kwa maana hii rudisheni VIPANYA.

  2:shirikianeni na jeshi la polisi kuwathibiti wenye madaladala wanaokatiza route au wanaokataa kuwabeba abiria wanaokwenda katika sehemu walizoruhusiwa kwa mujibu wa leseni zao.kila afande awaye kituoni kusubiri usafiri wake pindi akiona gari linakiuka sheria na kanuni aweze kuliripoti gari kwa vyombo husika

  3:Anzisheni huduma ya wananchi kuziripoti gari zinazogoma kuwapeleka ama kutoa huduma kwa abiria kwa mujibu wa leseni. na isiishie hapo tu, bali tuone kweli mnatekeleza majukumu ya kuzichukulia hatua gari hizi

  4: Sumatra ishirikane na vyombo vinavyohusika na kodi kuvishauri ili kodi ya kuingiza magari makubwa ipunguzwae watu walete magari makubwa na yanayofaa.

  Pamoja na Short term Solutions Sumatra lazima wawe na Longterm Solutions.

  ILA KUSEMA KWELI WANANCHI WA MKOA WA DAR-ES-SALAAM TUNAUMIA SANA KUTOKANA NA USAFIRI NA KUSEMA KWELI TUNATAKA MAJIBU KUTOKA SERIKALINI JUU YA TATIZO HILI.
   
 3. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2009

 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1. Serikali ihamie Dodoma

  2. Watu wakome kuhamia Dar..wabaki huko2 shamba! ha ha ha!

  3. Kwani ni lazima ufanyie kazi Dar? Kuna miji poa tu hakuna stress kama Iringa, Moshi, Tanga n.k
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Aug 16, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  well said
   
Loading...