Hivi suala la usaili wa utumishi kufanyika kikanda liliishia wapi?

KimpaGhasha

JF-Expert Member
Jun 21, 2020
327
448
Habari wanaJf,

Najiuliza saana kuhusiana na usaili wa utumishi kufanyikia dodoma.
Yaani sijafahamu kabisa kigezo kikubwa kilichochukuliwa mpaka wakaamua saili zao zote kufanyikia pale,

Yaani naona Kama ni mbinu inayotumika kunyima fursa/nafasi kwa baadhi ya watu kutoshiriki usaili kwasababu ya gharama zake na ukiangalia gharama za maisha kwa sasa ziko juu.

Lakini pia nikama vile mtu unaenda kubahatisha kutokana na mazingira ya saili zenyewe zinavyofanyika.

Lakini nakumbuka mwaka 2017 Kama mwezi wa saba hivi kuna ajira za TRA zilitangazwa na baadae kwenye usaili nafikiri watu walifanya kikanda.

Baada ya hapo sijasikia kabisa kuhusu kuendelea kwa utaratibu huu.

Binafsi niliuona kam ni utaratibu mzuri kwani ulitoa fursa kwa washiriki wote wenye vigezo kuhudhuria kwenye saili kupambania bahati zao kutokana na unafuu wa gharama kwa namna moja au nyingine.

Ila saivi mtu unajikuta una shotlisted nyingi ila ukianza kufikiria suala la gharama yakwenda dodoma na kurudi, kula na malazi duh unajikuta unakata tamaa tu na usaili wenyewe.

Nauliza hivi utumishi pamoja na wadau wengine hamna anaeliona hili?? Au wamekaa kimya tu kuna manufaa yanapatikana kwao endapo usaili ukifanyika dodoma??

Wakati wanaendelea nahuu utaratibu wanajiuliza kuna watu wanashindwa kuja huku kwasababu ya gharama kubwa??

Kiukweli inauma saana kwasababu hawa utumishi pamoja mambo yao yote yanaendeshwa na kodi zetu ambazo kila mtanzania mwenye vigezo vya kulipa analipa Kodi bila kujali mahali alipo,
kwahyo linapotokea suala la umma Kama hili nivizuri kila mtu mwenye vigezo ashiriki kwa namna yake.

Sidhani kam inashindikana kuratibu hili zoezi la usaili likaendeshwa walau kikanda.

Mkiendelea na utaratibu huo wakufanyia dodoma kuna watu watasikia tu kuhusu ajira za serikali,

Tafadhalini jamaniiiiii fikirieni na hili,,
 
Back
Top Bottom