MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Wakuu sitaki niseme sana lakini juu ya hili siachi kutamka neno!
Wengi tumeshuhudia upangaji wa kamati za bunge na viongozi wake, kwakweli kwa mtu yeyote mpenda maendeleo na anayelipenda taifa lake hawezi katu kufurahia upangaji huu usiozingatia weledi, muktadha, aina ya bunge lililopo na hata kauli mbiu ya Mh Rais ya hapa kazi tu.
Sidhani kama hata kwa kamati ambazo viongozi wake hawajapatikana kunweza kuleta changes zozote!
Ninachokisema hapa ni kwamba binafsi naamini huenda kuna wapo watu wazuri zaidi ndani walioachwa au wale ambao tayari wameshapangiwa kamati zao tayari. Ni dhahiri kabisa kwa kuangalia taswira halisi ya kamati ambazo nadhani kwa 95% wajumbe na wenyeviti wake wameshapatikana utagundua kabisa hakuna weledi wowote hapo, hakuna vigezo vilivyotumika kuteua wajumbe hao na kama kuna vigezo vilitumika basi ni kwa asilimia ndogo sana!
Binafsi nilifikiri uteuzi wa wanakamati hao ukengejikita zaidi kwa kuangalia zaidi taaluma zao na wala sio hisia za kisiasa,chuki,ubinafsi na visasi, nilitegemea kwa kuzingatia bungeni kuna kila aina ya wanataaluma basi hicho kingekua ni kigezo kizuri kama walivyofanya watangulizi wa Ndungai ili kupata washauri wazuri ndani ya bunge kila wanapotaka kufanya maamuzi ya kuidhauri serikali.
Inashangaza kuona watu ambao wana tuhuma lukuki za rushwa na hata mikono yao inanuka rushwa wanapewa kamati muhimu, hawa hawakutakiwa kupewa nafasi ya aina yeyote kutokana na tuhuma zao hata kama nao pia ni wazuri kwa taaluma zao maana hawataweza kuisimamia serikali zaidi ya kuulea na kuficha mambo.
Ikumbukwe kwamba siku za nyuma iliyokua kamati ya Mwakyembe aliyokua ikichunguza sakata la Richmond ilivyoficha Ripoti ya uchunguzi wake, pia tunakumbuka jinsi ambavyo wenyeviti wengi na baadhi ya wajumbe wa kamati mbali mbali walivyokua wakisemwa sana kwa tuhuma za rushwa.
Wameachwa watu ambao kwa hakika wanao uwezo wà kuisimamia vizuri serikali wakiwa viongozi wa kamati hizo na kwa kuzingatia taaluma zao. Sitaki niwataje kwa majina wabunge hao walioachwa lakini ukweli ndio huo! Hapa tutabaki kuendelea kuyaficha madudu ya baadi ya watendaji wa serikali na baadhi ya watu watabaki kunufaika na nafasi zao kama viongozi wa kamati.
Nchi hii maigizo hayaishi na tutaendelea na ngonjera zile zile, drama zile zile hata kwenye mambo ambayo si ya kusimamiwa na serikali.