Hivi spika Anna Makinda hana wigi la aina nyingine?

mawazoyangu

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
324
65
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana wigi analovaa huyu mama. kwa muda wote akiwa bungeni, nje ya nchi hata na wageni wake amekuwa akivaa wigi la aina moja tu ambalo kwanza halimpenezi bora hata angeacha nywele zake asuke mitindo mbalimbali au anunue mawigi ya aina mbalimbali ili alete mvuto wa kumuangalia. Kwa hilo alilonalo linachosha kuliangalia kila siku. Washauri wake au marafiki zake mtakaopita hapa JF hebu mpeni ushauri huu ili abadilike kidogo tumuone kwa muonekano mwingine tena unaweza ukampendezesha zaidi akawa wa kuvutia
 
Hivi ni wigi lile.....mimi nilidhania ni nywele zake!:lol::lol::lol:
 
Ni conservative, ni niwakizamani hataki kubadirika.
Ndio maana anaendesha bunge kama ni la chama kimoja. enzi zilee!
 
mmmmh huwa sipendi wanawake wanaovaa mawigi, sijui yanavaliwa au yanachomekwa hata sijui
 
Unataka aache kuvaa uone manvii yake??labda nywele zote nyeupeee...Hivi kwanza unataka abadilishe avae ipi?za rangi nyekundu au njano??
 
MAMA ANNA MAKINDA KWA NINI UMECHAGUA KUUDHALILISHA 'UBINADAMU, HAKI NA UTU WA MTANZANIA' KWA KUTUMIA USPIKA WAKO VIBAYA???:spy:

Hivi huyu mama alipokua amekaa pale mbele na kushinikiza saaana kupitishwa muswada huu ambao hivi sasa umebatizwa jina 'Muswada wa Makinda', alijibidisha hata kidogo tu kulifunua ndani akajionea jinsi ilivyo HATARI KWA USALAMA WA TAIFA letu kwa kukiuka mkataba wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kuvipa FURSA MPYA vyombo vya Zanzibar kutungia sheria mbalimbali Tanzania Bara na kuonekana mbuzi ndani ya gunia kiasi hicho?

Je, huyu mama anajua kweli tofauti kati ya marekebisho ya sheria ukilinganisha UUNDWAJI UPYA KWA KATIBA ya nchi kama ambavyo wananchi wa Tanzania tulivyoomba?

Je, mama Makinda anayo habari kwamba kwa Demokrasia ilivyoanza duniani kule Mesopotamia (Iraq ya leo) hali halisi ilikua ni ilikua ni kwa wananchi wote wa taifa hilo kujiendea bungeni (Direct Democracy) kujiamulia jinsi gani ardhi zenye rutuba za pale Ephrates na Tigris zingeweza kugawiwa uzuri kwa kila mwananchi akapata kulima. Je, anatambua ya kwamba ilikua tu ni baadaye sana tu ndipo mtaalam mmoja wa Hisabatia wa nchini Samos ajulikanaye kama Pythagorus alipoombwa tu NA BUNGE ZIMA LA WANANCHI WOTE ili aje kuwasaidia juu ya ugawaji ardhi kwa haki Pythagoras Theorem kutumika katika lengo hilo?

Je anayo habari kwamba yeye ni spika tu na yule ni mbunge tu kwa sababu siku hizi kutokana na idadi ya watu kuongezeka kukaonekana ni vema kutumia mfumo wa demokrasia ya uwakilishi (Representative Democracy) badala ya ile ya kila mtu kwenda bungeni?

Hali hii inamaana kwa hasa kwetu Tanzania kwa kukubali kufuata mfumo huu mpya ya uwakilishi bunge ni kwamba ni kweli wananchi TUMEAMUA KWA DHATI KABISA KUKASIMU MADARAKA yetu kwenu ili kila mlitendalo bungeni, mahakamani na huko serikali kuu ni SHARTI IENDESHWE KWA KUZINGATIA MATAKWA YETU na jinsi ambavyo tunawatumeni huko mkafanye. Mama Makinda iweje katika huu muswada nyeti na hatarishi wewe uamue tu kutuweka kando wananchi unafanya hivo kwa maelekezo na maslahi ya nani??

Mama spika, mbali na sisi kuhiari kukasimu madaraka yetu kwenu kutuwakilisha huko bungeni kwa kutunga sheria mbali mbali zinazotokana moja kwa moja na ndoto na matumaini zetu huku uraiani,
NANI KAKUAMBIA KWAMBA HATA MADARAKA YETU YA KUKALIA USHUKANI KUJIUNDIA KATIBA YA NCHI YETU NAYO TULIKASIMU KWA MTANZANIA MMOJA TU AITWAYE RAIS AU KWA WAKATI MWINGINE JAKAYA MRISHO KIKWETE na maswahiba wake?
:spy:
 
Hii mi siitaki kabisa kwa sababu huyo mama ytuko kwenye list yangu ya watu waliorudisha maendeleo ya nchi kwa kasi ya ajabu.
 
hana mvuto nje ya wigi na ndio maana hana mume akivaaa wigi angalau mvuto unakuja
 
Nashangazwa sana na tabia za wanaume kuwa wambea kuliko wake zao. Asubuhi ya leo mmojawetu humu kaanzisha mada ya kuwa ukitaka kuona mambo ya kijinga zama facebook. Sasa kuna mwenye kuweza kuniambia hii thread ina manufaa gani kwa mimi mwanaume rijali niliyekwenda jandoni?

Hivi huyu mama akivaa wigi jekundu au jeupe, wanaume inatuhusu nini? Mimi binafsi simpendi, tena kweli kweli. Lakini sio sbb ya wigi wala sura yake bali mwenendo wake. Angekuwa analima mchicha na kutuuzia kwenye tenga mtaani kila asubuhi angekuwa kipenzi changu lkn kwa kutuharibia nchi, namhara.

Wanaume mliopata ujasiri wa kujadili wigi ndio mlioshirikiana kutuchagulia Rais kwa kuangalia sura na matokeo yake ndio haya. Nyie endeleeni na umbea tu, ipo siku mtakutana na dada Marietha kichwa ngumu, mtavishwa sha...a wote.
 
Wanajamvini - kwa upande wangu, mawazoyangu kaniongezea siku za kuishi maana nimecheka vya kutosha... Nakubali fika kuwa swala muhimu ni utendaji kazi lakini tukumbuke pia kuwa "muonekano una nafasi yake" i.e. appearance matters. Na ndio maana kuna wake wa viongozi fulani na hata viongozi wenyewe (wake kwa waume) ..husifika kwa uvaaji wao. Basi, kuendesha Bunge kashindwa hata muonekano nao jamani?!! :laugh:
 
Hivi ni wigi lile.....mimi nilidhania ni nywele zake!:lol::lol::lol:

Ile nadhani wenyewe wanaiita weaving; wanashonea minywele bandia kwenye nywele fupi:)

Mambo ya urembo magumu; waweza kukuta jamaa wake wa karibu anapendezewa naye akiwa ktk style hiyo!
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana wigi analovaa huyu mama. kwa muda wote akiwa bungeni, nje ya nchi hata na wageni wake amekuwa akivaa wigi la aina moja tu ambalo kwanza halimpenezi bora hata angeacha nywele zake asuke mitindo mbalimbali au anunue mawigi ya aina mbalimbali ili alete mvuto wa kumuangalia. Kwa hilo alilonalo linachosha kuliangalia kila siku. Washauri wake au marafiki zake mtakaopita hapa JF hebu mpeni ushauri huu ili abadilike kidogo tumuone kwa muonekano mwingine tena unaweza ukampendezesha zaidi akawa wa kuvutia
Hapa hakuna haja kumushauri abadilishe Wigi .!!!Wigi ni Nywele za watu waliokufa!!! Ni vizuri viongozi wetu washangaike kuvaa Mawigi kama mitindo ya wazunguu!!! Kuvaa Wigi ni sawa na mtu mweusi anajichubua!!!

Wigi linawasha sana wakati huu wa jua kali na kutoa jasho lenye harufu Mbaya lakini Makahaba huwa wanavumilia kwa kuwa hakuna njia nyingine ya kuvuta wanaume!!!
 
Back
Top Bottom