Hivi Somalia kukoje kukoje,nao wana vifurushi vya chuo?

Mzingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
4,562
9,971
Mimi nikisikia jina Zimbabwe,picha ya kwanza inayonijia kichwani ni Mugabe(sio ya Ngoma wala Kamusoko).

Nikisikia Somalia,picha ya kwanza ni Alshabab na vita vyao.

Sasa leo katika pitapita kwenye internet nikajua kuwa Shilingi 1 ya Somalia ni Shilingi 3.75 za Tanzania. Ndipo nikahisi si bure,hawa watu inawezekana hata wao wana mambo matamu tu yanaendelea huko. Mnaoijua Somalia hebu mtujuze kuna nini zaidi ya vita vyao?
 
nimekaaa kama miez mitatu (sitataja eneo) ila aisee kuna joto sijawah ona teeena linakufanya uwe mweusi tiiii. kitu kibaya kuna ubaguzi wa kidini saana na amani haipo kabisaaaaa. yaani wageni mpaka mlindwe na drones hata kwenda kwenye kale ka ATM. ni shidaa kiola raia ana kisasi na mtu au kabila fulani.
 
Mimi nikisikia jina Zimbabwe,picha ya kwanza inayonijia kichwani ni Mugabe(sio ya Ngoma wala Kamusoko).

Nikisikia Somalia,picha ya kwanza ni Alshabab na vita vyao.

Sasa leo katika pitapita kwenye internet nikajua kuwa Shilingi 1 ya Somalia ni Shilingi 3.75 za Tanzania. Ndipo nikahisi si bure,hawa watu inawezekana hata wao wana mambo matamu tu yanaendelea huko. Mnaoijua Somalia hebu mtujuze kuna nini zaidi ya vita vyao?
Somaliya ninayoijua mie ni nchi yenye hazina kubwa ya MAFUTA ambayo ardhi yao imehodhi
mafuta yenye kukadiriwa trilioni mia sita ya mapipa!! na ina samaki wengi kuliko eneo lingine lolote hapa duniani.... mwambao usiopungua kilometer 3000 !!
kuhusu ALS hao walianzishwa ktk kipindi cha utawala na idara ya Abama (O) ili supa power zingine zisiweze kuja kuwekeza.. ila wao wamewaka kiporo miaka ya 2050 !!!
 
Inahuzunisha sana tena sana hela za nchi kama Somalia Burundi Ethiopia na Kongo hela zao zinathaman kuliko yetu. Mikwara mingi tuu daraja la kigamboni mabasi ya mwendokasi.

Eti tuna gesi asilia Uranium na Helium.

Too sad
Bahat mbaya hawa jamaa wana vita tu.. Iwapo wangekua politically stable mbona tungeisoma namba
 
Kule mkuu starehe yao kubwa ni miraa aka khat aka mirungi. Ndio ulevi wao mkubwa. Na kwa taarifa yako Somalia unapata vitu kama madawa.. nguo electronic zenye European standard. Sigara wanazovuta ni benson.. malboro..dunhill etc.
Ila kaubaguzi kapo. Kama wewe unakunywa pombe unaonekana ni kafiri.. ila wao wanakula mirungi na sigara muda wote kwao sio dhambi
 
Back
Top Bottom