Hivi Simba kweli wamemuacha Mohamed Ibrahim,inashangaza!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,161
9,365
Mojawapo ya wachezaji wenye vipaji nchini ni Mohamed Ibrahim MO!Inasikitisha sana kuona Simba alishindwa kuendeleza kipaji chake! Sijui Tatizo nini Naomba kujulishwa huyu kijana amesajiliwa wapi!
 
Wamemuachia yule mzee aliyeshikilia hati za Simba atoe pesa yake mfukoni amsajiri huyo dogo.
 
Kiukweli mo ana kipaji kikubwa lakin sioni kama atasogea mbele zaidi ya kurud nyuma kama ataendelea namna hii, anaujua mpira lakini hana jitihada za dhati kusogea mbele, kipaji bila juhudi ni bure..

Cr7 kuna watu kibao wa uzawa wake walikuwa wamemzidi kipaji ama wako sawa ila mwisho wa picha kwa juhudi zake yuko juu, watu wanamuweka siti moja na messi!!

Mtizame martial ni kama karidhika, ana kipaji kikubwa kweli,
Kisha mtizame rashford hatosheki hana kipaji kikubwa kama martial ila haridhiki hata kidogo kila siku anataka kusogea mbele..

Na hili tatizo lipo kwa karibia 95% ya wachezaji wetu hapa bongo.
 
Alikuwa hapati hata namba... May be huko atapata more time na kufanya poa zaidi
 
Mo Ibrahim ni mchezaji mwenye kipaji sana tena cha asili kila mpenda mpira analitambua hilo. Hata alipofika Simba msimu wa kwanza alicheza vizuri sana na alikuwa tegemeo sana. Alikuwa ana drible vizuri anapiga mashuti vizuri. Nafikiri baada yakufanya vizuri msimu wa kwanza Simba alijisahau badala ya kupandisha kipaji chake yeye akawa anachezea mazoea kuwa mpira anaujua. Matokeo kiwango kilishuka ghafla sana akaanza kupigwa benchi hapo ndipo alipochanganyikiwa kabisa. Kila akijaribu kupandisha kiwango chake ndani ya hii misimu miwili kashindwa kabisa. Cha msingi ili asipotee mazima bora akaanze moja KMC sio mbaya akishindwa arudi tu nyumbani Manungu. Akishindwa kurudisha kiwango chake Manungu basi aache mpira akafanye shughuli nyingine. Lakini Mo Ibrahimu bado ana uwezo wa kucheza ligi kuu kwa muda mrefu tu ujao kikubwa azingatie mazoezi halafu afute kwenye mawazo yake kuwa aliwahi kucheza timu kubwa.
 
simba kuna tatizo kubwa wamemwacha juuko wanamsajili wawa wakati mo yuko kwenye kampeni ya kupewa simba aliponda simba kuuza wachezeaji wazuri lakini tunashuhudia wachezaji wazuri wanaondoka bure
 
Sure, wachezaji wengi wa bongo badala ya kufanya jitihada binafsi, huishia kutafuta mtu wa kumnyooshea kidole na kumlalamikia. Hawajiongezi ipasavyo.
Kiukweli mo ana kipaji kikubwa lakin sioni kama atasogea mbele zaidi ya kurud nyuma kama ataendelea namna hii, anaujua mpira lakini hana jitihada za dhati kusogea mbele, kipaji bila juhudi ni bure..

Cr7 kuna watu kibao wa uzawa wake walikuwa wamemzidi kipaji ama wako sawa ila mwisho wa picha kwa juhudi zake yuko juu, watu wanamuweka siti moja na messi!!

Mtizame martial ni kama karidhika, ana kipaji kikubwa kweli,
Kisha mtizame rashford hatosheki hana kipaji kikubwa kama martial ila haridhiki hata kidogo kila siku anataka kusogea mbele..

Na hili tatizo lipo kwa karibia 95% ya wachezaji wetu hapa bongo.
 
Mo Ibrahim ni mchezaji mwenye kipaji sana tena cha asili kila mpenda mpira analitambua hilo. Hata alipofika Simba msimu wa kwanza alicheza vizuri sana na alikuwa tegemeo sana. Alikuwa ana drible vizuri anapiga mashuti vizuri. Nafikiri baada yakufanya vizuri msimu wa kwanza Simba alijisahau badala ya kupandisha kipaji chake yeye akawa anachezea mazoea kuwa mpira anaujua. Matokeo kiwango kilishuka ghafla sana akaanza kupigwa benchi hapo ndipo alipochanganyikiwa kabisa. Kila akijaribu kupandisha kiwango chake ndani ya hii misimu miwili kashindwa kabisa. Cha msingi ili asipotee mazima bora akaanze moja KMC sio mbaya akishindwa arudi tu nyumbani Manungu. Akishindwa kurudisha kiwango chake Manungu basi aache mpira akafanye shughuli nyingine. Lakini Mo Ibrahimu bado ana uwezo wa kucheza ligi kuu kwa muda mrefu tu ujao kikubwa azingatie mazoezi halafu afute kwenye mawazo yake kuwa aliwahi kucheza timu kubwa.
Yeah, pale aende kuanza moja, ajitume kwa 100%, asijifanye star anayeenda kucheza na madogo, atapotea.
 
Back
Top Bottom