Hivi Siku hizi kila Mtu akijisikia tu anaweza kwenda Bungeni Kusikiliza na Kutambulishwa kwa Wabunge hata akiwa hana na hajafanya la maana kwa Taifa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,324
2,000
Ifike muda sasa Heshima ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwepo kama enzi za Awamu ya Kwanza, ya Pili, ya Tatu na kidogo ya Nne. Bunge siyo sehemu ya kuingia Wahuni, Watu wakorofi, Vibaka na Watu wasiotaka kwa Makusudi kuhama eneo Hatarishi la Jangwani ambalo kila Siku tu Serikali inawahimiza wahame ili kuokoa Maisha yao na ya Majengo yao Machafu na yaliyochakaa miaka nenda rudi.

Bunge la Awamu ya Tano lenye muendelezo wa Rais wa Sita naona kama vile Hadhi yake ama inaanza Kupotea au huenda hata linadharaulika kwa sasa ambapo limekuwa linapokea tu Wageni ambao wengine wana Upuuzi Upuuzi mwingi na hawana Thamani yoyote ile ya Kimaendeleo kwa Taifa la Tanzania.

Nijuavyo GENTAMYCINE ni kwamba mpaka ukiona umealikwa Bungeni Dodoma na kuketi kule juu katika Visitors Gallery basi ama ni Mtu Muhimu sana na umefanya Jambo Kubwa, jema na lenye Faida na Mantiki kwa nchi ya Tanzania hivyo Wabunge nao wanataka Kukutambua kama Mhimili Mkuu Kikatiba.

Nimesikitika sana jana nilikiona Kikundi fulani cha Wahuni na Washamba Bungeni kinachotokea katika Kitovu Kikuu cha Mafuriko kwa Jiji la Dar es Salaam katikati ya Kigogo na Muhimbili kikiwa Kimealikwa Bungeni na Nguo zao zenye Rangi Mbovu, Kikitambulishwa na baadhi ya Wabunge wasiojielewa wakaanza Kukishangilia.

Nimejaribu kukifuatilia hicho Kikundi kuona labda kimefanya nini cha maana na Kugundua kuwa ndani ya Miaka Mitatu (3) mfululizo na ukielekea wa Nne (4) huu hakuna cha maana kilichofanya hadi jana Kikaribishwe Bungeni na mpaka Wabunge wasiojielewa nao kuanza Kukishangilia.

Spika wa Bunge Ndugu Job Ndugai tafadhali rejesha Heshima ya Jengo hilo la Bunge kwa kuhakikisha kuwa wanaoalikwa hapo wawe ni Watu wa maana na ambao wameleta Chachu ya Kimaendeleo na Ufanisi mkubwa wa Kiuchumi kwa Tanzania yetu na siyo kualika Watu ambao wakipangiwa Ratiba ya kwenda Vitani Kupambana na Adui wao Wanakimbia na kuanza kuleta Visingizio vya kila aina.

Na sijui kama hiyo Jana baadhi ya Vifaa (Electronic Gadgets) hapo Bungeni hawakuviiba au hata Wabunge nao hawakuchomolewa (hawakuibiwa) Simu na Pochi zao kwani Kikundi hicho kinachotoka Kariakoo Bondeni kinajulikana sana kwa Kuiba, Kupiga, Ubishi na Kulalamika hovyo kikiwa katika Majukumu yake yanayotambulika na Jengo moja hivi Kubwa lililopo Karume.
 
funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
12,043
2,000
Niliwahi kwenda Bungeni nikiwa Primary pia nilienda tukiwa chuo kikuu na baadae nimeenda sana kikazi. Bunge ni sehemu ambayo mtu yoyote anaweza kwenda kama akifuata taratibu zinazotakiwa. Ni sehemu huru na kuna namba ya wageni wakuingia kwa siku ambao wanaleta maombi na wengine wanaalikwa na Bunge lenyewe au wabunge kwa kufuata taratibu

Nadhani mtu yoyote ana haki ya kwenda bungeni kama akifuata taratibu zilizopo ndio maana unaona watu kama kina Bolizozo na wengine wanaenda Bungeni na kukaribishwa na kutokana na utaratibu wao bungeni wageni uwa wanatambulishwa na kukaribishwa kama ilivyo kwenye makanisa (sijui msikitini)

Taratibu hizi hazijabadilika awamu yoyote maana kama mie niliingia nikiwa primary enzi za Mwalimu Nyerere ingekuwa wana nongwa tusingeruhusiwa sie watoto wadogo enzi zile
 
Walioenda jana ni Wahuni na Vibaka tu.
 
bolivia

JF-Expert Member
Mar 3, 2021
607
1,000
Nipo njiani naelekea bungeni ina Maana nishuke niishie hapa hapa3 nirudi au ?? Acheni bana bungeni ni sehemu huru.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom