Hivi siasa ndio iharuhusiwa kuingilia Dini? Makamba kuna siku anasimama bila vifungu vya biblia kwenye mikutano ya CCM?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kuna Kitu ambacho bado sijakielewa! Mnaojua nifahamisheni jamani, hivi anaeruhusiwa kuchanganya DINI na SIASA ni Mwana Siasa tu?

Namaanisha kwamba mtu wa SIASA yeye ndiye anaeruhusiwa kisheria kuitumia Dini akiwa kwenye SIASA, akanukuu Vifungu vya BIBLIA, ama Quran, kuwasema watu wa DINI kupitia maandiko ya BIBLIA na Quran, ila Mtu wa Dini yeye haruhusiwi kuwasema watu wa Siasa awapo kwenye NYUMBA ya IBADA??

Maana nakumbuka wakati nikiwa bado nachipukia kwenye UTUMISHI, nilikuwa nikimsikia sana, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM ndugu YUSUFU MAKAMBA! akinukuu sana maandiko ya BIBLIA, awapo kwenye MAJUKWAA ya SIASA! (Kuna mtu asiyejua hili?) Ila sikuwahi kusikia akimbiwa either na msajili wa VYAMA vya SIASA kwamba, haruhusiwi kutumia maandiko ya DINI! kwa sababu sijui taratibu na Sheria za VYAMA vya SIASA na TAASISI za Kidini, nimekuja kwenu mnaojua mnifahamishe JE! kisheria, Mtu wa SIASA yeye anayo ruhusa kuchanganya DINI na SIASA, ila Kiongozi wa DINI yeye haruhusiwi?

Maana naona BIBLIA na Quran, BUNGENI zipo! na zinatumika kuwaapisha watu wenye imani kulingana na Kitabu Husika! Hata Mawaziri, Makatibu, Wakuu wa Mikoa, Na Wateule wengine wa Rais wetu! niliwaona wakiapa kwa kutumia Vitabu hivyo vya DINI!

ANGALIZO:- kama huna ujuzi na haya ambayo nimeyaulizia tafadhali sana, usicomment kwa jaziba, Kashifa, dhihaka wala Matusi! kwa viongozi wa aina yo yote, Wawe wa Kiserikali, BUNGE, Mahakama, wala Kidini!

Bali nipe darasa kulingana na Sheria za NCHI zisemavyo! hii itanisaidia kufahamu, na kutokuwa mropokaji linapotokea jambo ama kulaumu, kwa kuona mtu anakandamizwa ama kuonewa wakati Sheria ipo inayo mbana. Ahsante.

Ndimi ABEL SULEIMAN SHILIWA

USTADH MHUBIRI WA INJILI.
 
kwanza nini maana ya
i/dini
ii/siasa
yawezekana hata hujui mtoa post unakurupuka tu.
 
Hapa bongo sheria hupindishwa ili jambo flani lisifanyike, hivi unajua ni kwanini wakuu wa miko na wabunge hawakukumbwa na mambo ya vyeti feki!? Ni kwamba walipindisha sheria! Bongo sheria ya barabara ilishawahi kwenda kupigwa kiraka ili majengo flani yaonekane yako kwenye rodi rezevu:)), ili yabomolewe! Sasa hivi watapindisha tena, ili ukiwa wa kanisani au msikituni wote mtakuwa hamuwezi kuongelea siasa, mfano kutaja chama flani waziwazi kama alivyofanya kakobe, na bahati mbaya sana tayari baadhi ya wailslamu wameonyesha kuunga mkono hili
 
Rwakatare ni mchungaji na ni mbunge wa ccm yeye amechanganya nini sasa
 
Back
Top Bottom