Hivi si alisema atabeba mikoba ya marehemu Mengi?mpaka sasa mbona kimya tena

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,795
Namsemea bwana mmoja mkuu wa mkoa kwenye ile siku ya kumuaga marehemu mzee mengi( r.i.p mzee wangu)alisema kuwa marehemu alikuwa ni mtu mwema sana,tena akaenda mbali na kusema kuwa hajawahi ona mchaga mwenye moyo kama wa mzee mengi na haitakuja tokea.

Huyu mh.alijipambanua mbele ya hadhara kuwa atahakikisha amebeba mikoba ya marehemu kwenye kusaidia walemavu,masikini,viwete na wasiojiweza.

Kufuatia kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa ramadhani unakaribia kumalizika na kama mnavyoona au kujua kuna wale wasiojiweza kipindi kama hiki ilitakiwa kuwe na angalau msaada fulani kwao.je?

Ile kauli ndio iliishia pale pale au ilikuwa danganya toto mbele ya mike/hadhara.nilikuwa namkumbusha tuu vipi imekuwaje tena mheshimiwa?
 
Back
Top Bottom