Hivi Shirika la Posta linaendeshwa na akili timamu kweli? Nashangaa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,985
17,850
Wafanyakazi wa Posta na maboss wenu mliopo humu ujumbe huu uwafikie

Kwanza mna huduma mbovu kweli kweli yaani nyie ni zero tu hadi shirika hili nahisi linaongozwa na watu wasio timamu au vichaa tu

How come mtu anaagiza mathalan kitu cha 500 tsh mnamchaji 2350 kama tozo na pia mnamchaji 5900 hii mnaijua wenyewe bado mnakabidhisha kwa mtu wa TRA analipa tena ushuru

Hivi mna akili kweli nyie posta???Hivi mmelogwa na nani?Sijapata kuona shirika la hovyo hapa duniani na akhera kama posta Tanzania

Mna huduma za kutuma mizigo mikoa yote lakini hata hampromote halafu gharama ni kubwa kuliko bus na inachelewa balaa

Ni kawaida kwa posta mzigo unatumwa kutoka China ndani ya siku 7 umefika bongo lakini Posta hadi uupate inachukua mwezi au miezi 2

Kuna kipindi mlijitahidi kiasi mfano 2019 mlifanya vizuri, mlikua hata hamtoz viparcel vidogo na mkaweka charges za kawaida nakumbuka ilikua 1000 au 1500 watu wakaanza kutumia posta kwa wingi


Na nyie TRA ambao ni maadui wa wafanya iashara nchi hii mmefungua ofisi posta kazi yenu ni kukodolea viparcel macho na kuwalimu watu kodi kubwa mfano mdogo tu niliagiza saa ya laki moja mtandaoni kufika tu nikalimwa kodi 45000/= hapo posta washanipiga 2350 na 5900 yaani acheni tu

Shirika la posta pia limejaa janja janja nyingi utasikia njoo kesho njoo kesho kutwa mara Rukia wa viparcel hayupo mara katoka unazungushwa tu ujinga mtupu na upuuzi

Wafanyakazi wa posta wapo wanaohudumia kama vile hawataki customer care mbovu halafu vizee,na vizuka ni wengi posta yaani wamezeekea shirikani wapo wapo tu wanafanya kazi kwa mazoea na hawakubali mabadiliko

Namuomba mama Samia aliangalie hili shirika la posta linatia aibu nchini
 
Pole sana kaka mkubwa kimsboy

Ngoja waje watu wa posta tuone na wao watasema nini kabla ya mimi kutia neno kwa maana sio sahihi kutoa hukumu kwa kusikiliza malalamiko ya upande mmoja tu.

Ngoja na wao waje kwanza.
 
Prof Assad akisema 60% ya watumishi wa umma ni vilaza, haeleweki na mnamuona anaongea utumbo.

Sekta ya watumishi wa umma nchi hii inatakiwa kufanyiwa "REBOOT" yote, yani inatakiwa ni mwendo kufukuza pimbi wote serikalini, imejaa wana "CCM" na "MATOTO YAO" tu kwa kupeana pasi za visigino.

Unakuta TRA au WIZARA inatoa nafasi ya ajira 3, ila wanafanya interview kwa vijana 600 wanaopanga foleni siku nzima juani au kwenye mvua, halafu hakuna hata mmoja katika hao 600 anapata nafasi ya kazi (Kumbe wameshaandaa watu wao hao 3 tayari).
 
Mkuu hili shirika linahitaji maboresho makubwa sana kwa sasa Africa kiteknolojia tupo nyuma sana lakini tukiboresha shirika la Posta liwe nyenzo ya biashara za mtandaoni kutuma parcels na biashara zote za mtandaoni imports and exports tungekua mbali na nchi ingetengeneza faida kubwa sana
Pole sana kaka mkubwa kimsboy

Ngoja waje watu wa posta tuone na wao watasema nini kabla ya mimi kutia neno kwa maana sio sahihi kutoa hukumu kwa kusikiliza malalamiko ya upande mmoja tu.

Ngoja na wao waje kwanza.
 
Kabisa
Hili shirika limekosa ubunifu linaendeshwa kwa mfumo wa miaka ya 1970 enzi za utawala wa mwalimu. Hata wafanyakazi nao ukiwaangalia tuu wamekaa kizamanizamani. Linahitaji msaada kufufuliwa na kuendeshwa kisasa.
 
Hili shirika limekosa ubunifu linaendeshwa kwa mfumo wa miaka ya 1970 enzi za utawala wa mwalimu. Hata wafanyakazi nao ukiwaangalia tuu wamekaa kizamanizamani. Linahitaji msaada kufufuliwa na kuendeshwa kisasa.
Aisee..
 
Back
Top Bottom