Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Moja ya sifa kuu ya sheria huwa inakuwa haina macho, sheria ni kama msumeno unakata huku na kule.
Lakini cha ajabu ni kwamba katika serikali ya awamu ya 5 sheria imekuwa na macho, inaangalia nani amefanya kosa hilo kama ni mteule wa Rais basi sheria hiyo haitamgusa na kama ni mtu mwingine, sheria hiyo itamgusa, tena kwa nguvu zote!
Lilianzishwa hapa zoezi la kuhakiki vyeti, maelfu ya watu wameathirika na zoezi lile, wemgi wamepoteza kazi zao na wamekosa kulipwa hata angalau stahiki zao za kutumikia serikali hii kwa kipindi kirefu.
Lakini lilipokuja kumgusa Mkuu wa mkoa wa Dar, watu wamesema sana kuhusu huyo mtu kutumia jina la mtu mwingine, jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kama ambavyo wale maelfu ya waathirika wengine wa serikali, lakini tumeshuhudia mtu huyo akiambiwa na mteule wake kuwa kijana piga kazi!
Tumeshuhudia pia huyo "dogo" huyo akivamia studio za Clouds akiwa na maaskari wenye silaha, za moto lakini tumeshuhudia mtu ambaye ameunda tume kuchunguza tukio lile la kinyama akifukizwa kazi ya uwaziri, huku akimwacha yule "dogo" akiendelea kuchapa kazi!
Tumeshuhudia pia Mkuu wa mkoa wa Arusha akitumia vibaya madaraka yake, mathalani akitumia vibaya rambirambi za wafiwa wa Lucky Vincent, tumeshuhudia pia mteule wake akisema kijana chapa kazi, usisikilize maneno ya mitaani!
Tumeshuhidia pia Mkuu wa wilaya ya Arumeru akifanya vituko vingi, miongoni mwake ni hii skandali inayotrend hivi sasa kwenye social media nyingi kuhusu hiki kituko cha mwaka inayohusu "ununuzi" wa madiwani wa Arumeru, lakini kama ilivyo kawaida ya aliyemteua hatutarajii lolote limtokee huyo jamaa zaidi ya kuambiwa kijana chapa kazi usisikiize maneno ya wapiga debe wa mitaani!
Sass ndiyo nauliza hivi kwenye utawala bora na utawala unaozingatia sheria, hivi makosa yaliyofanywa na wakuu wilaya na mikoa ambao hawako juu ya sheria, hivi si walipaswa kwanza kukaa pembeni na kupisha uchumguzi ili ikithibitika kuwa madudu wanayosemwa ni kweli basi watupishe??
Mimi nimejaribu kueleza kanuni za utawala bora na utawala unaozingatia sheria unavyopaswa kuwa ni hao jamaa wasingestahili kuwepo kwenye nafasi zao za sasa ili kupisha uchunguzi, lakini as usual tutajibiwa na mteule wao kuwa vijana chapeni kazi na msisikilize maneno ya mitaani!
Nchi hii inahitaji maombi makubwa kabisa kwa Mungu wetu ili atuongoze na tuvuke salama safari yetu.