Hivi Serious Yanga mnakubali huu mtego wa Manji?.

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Hivi Serious Yanga mnakubali huu mtego wa Manji?. Sio kwamba simtaki Manji bali Yanga kwa sasa inahitaji viongozi wapya ambao watakuja kuinusuru klabu hali mbaya kwa sasa kwenye klabu wachezaji halipwi mishahara kwa wakati, Fedha za kuendesha klabu kwa sasa hamna, Fungu la Usajili kwa sasa Hamna dirisha linafunguliwa November 15 na kufungwa December 15.

-Harafu munaambiwa Manji anarejea kazini January 15 siku Mbili baada ya Uchaguzi wa January 13 itakuwa kama Yanga mtakubali kuingia kwenye huu mtego msifanye uchaguzi kwenye nafasi ya mwenyekiti then na hiyo January 15 asirejee nani atalaumiwa? Cha msingi kwa sasa Manji na Wenye Yanga yao wangekubali tu ufanyike uchaguzi na Manji asigombee ila viongozi wanaoingia madarakani wafanya mchakato wa kubadili mfumo wa klabu uwe wa Hisa kama Simba na Manji aingie Yanga kama mwekezaji.

-Kuendelea kumlilia Manji wakati klabu iko kwenye hali mbaya hii haikubaliki kabsa harafu wanachama wa Yanga hebu kumbukeni Viongozi wa Yanga wamesema mara ngapi Manji anarejea kila mara mlikuwa munaambiwa mwezi mmoja anarejea mara miezi mitatu lakini yote hupita bila kumuona sasa mnataka kuaminishwa kitu ambacho mlidanganya huko nyuma. Yanga kwa sasa inahitaji viongozi wapya wenye uchungu na Yanga kuliko Manji.

-Na sasa hivi wanachama wa Yanga wako makundi Matatu moja wanakubali kufanya uchaguzi, wengine wanapinga kufanyika kwa uchaguzi nafasi ya Mwenyekiti, wengine wako njiapanda hawajui wafanye nini wanaumia kimoyomoyo tu hawajui wasapoti kundi lipi ila bora kuifikilia Yanga zaidi kuliko kuongozwa na mihemuko ya muda ambayo itakuja kuwacost baadae.

-Yanga ina watu, Yanga ina viongozi wengi wenya kujua kila fitina ya mpira hapa Tanzania ila walikaa pembeni kwa sababu ya Manji kwa nini wasiandae mfumo ambao utamruhusu Manji aingie kama ana uchungu na Yanga kuliko sasa kumuona kama Mungu mtu na kuamini Yanga haiendi bila Manji? Me naamini Viongozi, wanachama wa Yanga wanaweza kufanya kitu na wakaukwepa huu mtego ambao utakuja kuwatesa miaka mingi Ijayo.

-Yanga kataeni Utumwa huu wa Manji mbona mashabiki wa Simba waliukataa utumwa wao kwa Masoud kuna mtu wa Simba kwa sasa anamtaja Msoud? Jibu ni hapana kwa nini na nyie Yanga huu utumwa msiukatae tumieni busara kutoingiza klabu kwenye migogoro ya ndani ya Klabu na mgogoro dhidi ya Shirikisho huu ndio muda mwafaka wa kukaa chini na kutafakari kwa makini ili kufanya maamuzi sahihi wakati huu Sahihi.
 
Mambo ya Yanga yaamuliwe na waba Yanga kwa manufaa yao.

Yanga haiwezi kupokea amri za Simba kupitia TFF ya Msomali na Mrundi. BMT waliotoa maamuzi ni Simba tupu.

Kama wenye timu wanataka iwe hivyo, itakuwa hata aje nani.

Akilimali anatumiwa na Mzee wa ku bet Abbas Tarimba. Hapo kapoteza credibility yote. Hiki kizee kina njaa ya kufa. Kinaweza kutumiwa na matopeni vile vile.

Iweje Uchaguzi uendeshwe na TFF iliyojaa maslahi ya Simba. Kwa nini Kamati ya Uchaguzi Yanga isifanye kazi hiyo?

Simba kupitia Msomali na Mrundi kamwe hawataweza kuiamulia Yanga.

Yanga tunajua hata PM ana mkono kwenye kutaka kuharibu Yanga. Apambane na korosho Jimboni kwake
 
Madai mazito ukibanwa uthibitishe utaweza?Au umekalia majungu? You are sliding in thin ice. Chunga.
 
Hapo mwanzo Simba na Yanga walipewa siku 60 waandae mchakato wa uchaguzi ikawa Simba tu wametimiza hilo.

Kwahivyo lazima msimamiwe na TFF kwani wenyewe kwa awamu hii mmeshindwa kufanya uchaguzi, hata dalili hakuna mmeng'ang'ana na Manji
Mambo ya Yanga yaamuliwe na waba Yanga kwa manufaa yao.

Yanga haiwezi kupokea amri za Simba kupitia TFF ya Msomali na Mrundi. BMT waliotoa maamuzi ni Simba tupu.

Kama wenye timu wanataka iwe hivyo, itakuwa hata aje nani.

Akilimali anatumiwa na Mzee wa ku bet Abbas Tarimba. Hapo kapoteza credibility yote. Hiki kizee kina njaa ya kufa. Kinaweza kutumiwa na matopeni vile vile.

Iweje Uchaguzi uendeshwe na TFF iliyojaa maslahi ya Simba. Kwa nini Kamati ya Uchaguzi Yanga isifanye kazi hiyo?

Simba kupitia Msomali na Mrundi kamwe hawataweza kuiamulia Yanga.

Yanga tunajua hata PM ana mkono kwenye kutaka kuharibu Yanga. Apambane na korosho Jimboni kwake
 
Achukue tu fomu za kugombea uenyekiti tutamchagua.
Au aweke hisa kama alivyofanya MO pale Msimbazi.
Nadhani itakuwa bora zaidi
 
Hapo mwanzo Simba na Yanga walipewa siku 60 waandae mchakato wa uchaguzi lazima Simba tu wametimiza hilo.

Kwahivyo lazima msimamiwe na TFF kwani wenyewe kwa awamu hii mmeshindwa kufanya uchaguzi, hata dalili hakuna mmeng'ang'ana na Manji
inawahusu nini mikia nyie
 
Hapo mwanzo Simba na Yanga walipewa siku 60 waandae mchakato wa uchaguzi lazima Simba tu wametimiza hilo.

Kwahivyo lazima msimamiwe na TFF kwani wenyewe kwa awamu hii mmeshindwa kufanya uchaguzi, hata dalili hakuna mmeng'ang'ana na Manji
Mkuu, kama mlivyong'ang'ana na Mo. Hakuna wengine? Mkidumu mwaka, nitaamini mmefanikiwa.
 
Mnashangaa nini?Kuna watu walimpigia magoti na hali hiyo ya ufalme ameizoea.
Katiba ya Yanga inasemaje mtu akijiuzulu?
Kiongozi asipohudhuria mikutano 4 mfululizo ya kamati ya utendaji ya klabu inakuaje?
Manji anajua wanachama wako brain washed kwamba bila yeye hakuna Yanga na anaitumia anavyotaka.
Halafu wanachama hao hao na wapenzi wako mstari wa mbele kukosoa timu zingine. Ni kweli nyani hana kioo.
 
Back
Top Bottom