Hivi ' Serious ' kabisa Serikali kupitia Rais JPM na Waziri Mkuu wake ' wamelibariki ' hili jambo la ' Aibu ' huko Dodoma?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Hivi Waziri Jafo alishindwa nini tu Kuomba radhi kwa Mheshimiwa Rais kwa kuchelewa Kumaliza Ujenzi wa Jengo la Wizara ili waendelee kubakia Kwanza huko walikokuwa na wakishamaliza Ujenzi ndiyo wahamie hapo eneo la Mitumba?

Yaani kabisa Wizara kama ya Jafo inakuwa katika ' Mabati ' halafu linaonekana ni jambo zuri na hapo hapo tena Waziri Mkuu nae anaenda Kuitembelea hiyo hiyo Ofisi ya ' Mabati ' tena bila hata ya chembe ya ' Aibu ' hasa kwa heshima kubwa ya Cheo chake hicho.

Kwa mtizamo wangu nahisi kwamba japo Mheshimiwa Rais alikasirika vile na kuamua kuwa Ofisi za hiyo Wizara ziwe hivyo hivyo katika ' Mabati ' hayo ila nadhani hakumaanisha hivyo na pengine angeombwa radhi pale pale huku akieleweshwa vyema juu ya huo Ujenzi basi angeelewa na kuwapa muda ila hapa tatizo naliona kwa Waziri husika wa hiyo Wizara.

Kama nyie Watu wa Serikalini hasa hiyo Wizara ya ' Mabati ' mnaona kuwa kwa kuhamia hapo na hivyo hivyo Jengo likiwa ni ' Full ' mwendo wa ' Mabati ' ni Sifa au Kuonyesha ' Utiifu ' kwa Mheshimiwa Rais badi jueni kuwa kama kuna ' Aibu ' kubwa ambayo kwa Siku za hivi karibuni Tanzania imepata ni Kitendo hicho cha ' Kipuuzi ' kabisa cha kuhamia ' Kinafiki ' na ' Kiuwoga ' hapo ' Mabatini ' Kwenu.

Kwa huu ' Upuuzi Upuuzi ' wenu ndiyo wengine tukitoka tu nje ya mipaka ya Tanzania huwa tunaukana ' Utanzania ' Wetu kwa muda na ' Kujilipua ' tu kuwa tunatoka Mataifa mengine kwani siyo Siri kama kuna nchi ambayo huko nje inaonekana ni ya ' Kimbwigira / Kishamba ' kuliko zingine zote basi ni Tanzania na sababu Kubwa ni aina hizi hizi za mambo yenu ya ' Kipuuzi ' kama haya.

Halafu na Wewe Waziri Mkuu tena Mwana Simba Sports Club mwenzangu kabisa na Mwalimu mzuri sana tu ' Kitaaluma ' hebu basi Siku zingine uwe unapima ' Matendo ' yako ya Kiserikali na kama kuna mahala ukiona hapako sawa basi usiwe ' Muoga ' kumwambia au kumshauri Bosi wako Mkuu Mheshimiwa Rais kuliko na Wewe kujitia ' Aibu ' na Suti zako kabisa na kwenda ' Kuzindua ' Wizara ya ' Mabati ' kama hiyo ya Waziri Jafo. Umeniangusha sana Mheshimiwa Waziri Mkuu na kwa ' Umefeli ' mno tu kwa hilo.

Hivi ni nani ' ameiroga ' Tanzania yetu hii na hasa katika ' Mfumo ' wetu mzima wa Akili na matumizi yake? Yaani kabisa Watu ' Wasomi ' na ' Misuti ' yenu mnakubali kwenda Kujenga ' Mabati ' na Kuweka Vibao vya Ofisi na Idara zake katika Jengo ambalo bado linaendelea na Ujenzi wake halafu mnakaribisha kabisa Wananchi kupata Huduma hapo huku ' mkijisifu ' kabisa na ' Makamera ' kedekede?

Natamani mno ' Kenneth ' akimalizana na Mtwara, Lindi na Dar es Salaam kuanzia leo Usiku hadi Jumanne ijayo basi moja kwa moja ' ahamie ' Mkoani Dodoma na aende pale pale katika Wizara ' Mabati ' kisha ' afagie ' kila Kitu pale ili hayo ' Mabati ' yao waje kuyaokota Baharini Dar es Salaam yakiwa ' yanaelea ' Majini na ikiwezekana pia ' Kenneth ' aondoke na baadhi ya Watendaji Wakuu hadi Mtoni na huko Baharini ili Siku zingine Akili zao ziwakae sawa.

Nawasilisha.
 
Mbona yeye mwenyewe hajahamia kama alivyo ahidi kwa sababu majengo yake hayaja kamilika? Tatizo la Tanzania kama Jafo angetamka kuwa afanyavyo Rais sio sahihi basi ingeonekana kama kakufuru na asulubiwe.
Mbona mawaziri katika nchi zenye demokrasia wanaweza kumchalenji Rais katika maamuzi ya kibwege?
LAKINI WACHA WAHAMISHIWE HATA CHOONI NDIO WATATAMBUA TUNAPOSEMA HUYU NI DIKTETA WANABISHA WAWE NA UELEWA. Kifuatacho sasa ni watendaji kuchapwa bakora na kuitikia hewala bwana! nadeki! Jiwe charaza hao mifugo wako
 
Inaonyesha kwa akili zalizopo kwa sasa Tz ndio sehemu mnatakiwa mkaesio kwenye nyumba nziuri bali mabati uchafu ndio mjue hakuna kitu kwa kweli
 
Acha wafanyie kazi humo pengine watajiongeza kumaliza jengo lao kwa haraka.
Kama pesa ipo, kwanini jengo lisiishe?,

Ndiyo wahamie katika ' Ofisi Mabati ' Mkuu? Yaani na Wewe kabisa hili unaliunga mkono? Kweli sasa naanza Kuamini kuwa Tanzania bado sana na huenda ' Tulishalaanika ' na walioijenga na kuipigania vyema hii nchi.
 
Uzuri huyu mzee alishakiri mwenyewe kwamba yeye ni kichaa au mwendawazimu ukipenda!
Maamuzi mengi ya kiongozi mkuu yanasababisha hasara au majonzi kwa jamii anayoingoza....majuzi hapa katudanganya ameirudisha ile ndege ya serikali (foker)ATCL ili ikawapige "jeki" kumbe kichaa wa watu alikuwa anaimezea mate ile "Dreamliner" ya ATCL.....ni shetani tu anaweza kumuelewa huyu mwendawazimu wa nchi yetu.
 
Hii ni nzuri sana tu kwa maoni yangu, inaonyesha 'Uwajishaji' wa wanaochwlewesha mambo. Zaidi uzalendo mkubwa kutangaza jina la nchi yetu, maana tumeingia kwenye record Wizara ya majengo ya aina yake nchini TANZANIA.
 
Kama Waziri wa Nishati alizindua nyumba ya nyasi kuwekwa umeme kuna jipya tena la kushangaa?
Kwa mtazamo wangu hapo tatizo liko upande wa Wizara yenyewe na wala si mkandarasi anayejenga hilo Jengo. Inasemwa kwamba Jaffo alijianzia tu kujenga hilo jengo bila ya kumshirikisha Rais ambaye ndiye Waziri wa Wizara husika.

Maana ingekuwa ni Mkandarasi ungesikia amri zinavyotolewa. Tafakari tu ya kizushi: Hivi huo ni uzalendo ama kuzalilishana.
 
Kama Waziri wa Nishati alizindua nyumba ya nyasi kuwekwa umeme kuna jipya tena la kushangaa?

Hofu yangu tu ni kwamba hii kubali kubali tu ' Kuamrishwa ' kuna Siku litatokea ' Tamko ' la Kila Wizara Kujenga Vyoo vyake maeneo fulani halafu labda Wizara moja ikashindwa Kujenga kwa wakati hivyo ' Amri ' ikatoka kuwa Watendaji wa hiyo Wizara wawe ' wanakunya / wanaukweka ' tu hivyo hivyo hata katika Nyasi za pembeni na kweli nao wakakubali na tukawa tunaona hao Watendaji wakishindana kutafuta ' Vipori ' vya Kushushia ' Mizigo Taka ' yao. Na si ajabu hata Media nazo zikaitwa Kufanya ' Live Coverage ' wakati wao wakiwa ama ' Wanakojoa ' au ' Wanakunya ' na tukarushiwa vile vile.
 
Hii iwe funzo kwamba ukipewa majukumu basi simamia kwa nguvu ili yakamilike kwa wakati. Raid alikuwa mkali mpaka kuagiza jeshi kuingilia kati kazi za ujenzi zinapodorora sasa kwanini kilasiku yeye ndiyo aingilie kati viongozi wengine hawawezi??

Wakati mwingine inafaa kiongozi afanye maamuzi ya kibange bange ili mambo yawe yanakamilika kwa wakati. Siyo jambo zuuri lkn ni ok ukizingatia uzembe wa watendaji walio wengi.

Kukataa kujiita mtanzania huo ni upuuzi wako mtoa mada,nyie ndowale mnaopeleka wachumba nyumba ya jirani kujidai ndiyo kwenu.
 
Back
Top Bottom