Hivi serikali za CCM miaka 70 ya uhuru zimeweza nini mbona vitu muhimu kama Maji na umeme bado shida kuu?

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,423
2,000
Hawa jamaa wa CCM wanapenda kutawala kupita kiasi, lakini performance yao ni ndogo kupita maelezo

Huwa wanapenda kujilinganisha na chama cha Kikomunisti cha China, lakini wenzao huko China wameshafanikiwa kusolve tatizo la vitu basic kama maji na umeme na sasa wanajiposition kuwa superpower wa dunia, CCM yenyewe hata ishu ya madawati wameshindwa kusolve miaka yote hii ya kuwa madarakani.

Leo hii Nchi imekauka kaukau, maji hakuna, umeme wenyewe ni wa mgao. Nchi ina maziwa makubwa mengi na mito lukuki lakini serikali za CCM zimeshindwa kusolve hizi ishu.

Sasa kitu gani CCM wanachojua?
1. Wanajua kucontrol mass ya wananchi, kuwapumbaza, kuwalaghai na kufanya uzandiki

2. Wanajua kumbambikizia watu kesi za kisiasa, kutumia dola ili kubaki madarakani

3. Wanajua kufanya ubadhirifu na kutumbua pesa za umma, safari zisizo na tija, kupeana vyeo serikalini kutokana na koo, angalia wanavyogawiana nafasi kutokana na kuwa huyu ni mtoto wa fulani alikuwa na cheo fulani zamani

4. Mipango mibovu, na priorities feki
Leo unaenda kununua midege wakati watu hawana maji ya kunywa ya uhakika, shule hazitoshi, umeme siyo wa uhakika. Hata hiyo Stieglers ikikamilika, megawatts 2000 bado ni peanut, nilitegemea kuona tunaanza projects leo za kuzalisha megawatts kuanzia 10000 na kuendelea

Tatizo kuu la CCM ni Low IQ
Wenzao wa chama cha kikomunisti wanachukua wanachama based on merits, na watu wenye merits wana IQ nzuri. Sasa CCM inachukua watu kutokana na uwezo wao wa kusifu na kujipendekeza au uwezo wao w kumtukana Mbowe, What do you expect?
Hawa Low IQs wataifikisha nchi wapi

Ukiwasikiliza kwa sasa ni kama wamegawanyika, ccm ya sukuma gang, na ccm msoga line. Ccm sukuma gang wanaonyesha kwamba mgao wa maji wa sasa sio uzembe wa ccm iliyokaa madarakani muda mrefu, bali wanaonyesha ccm msoga line ndio tatizo. Ukiwauliza ukame wa 2016 wakati mwendakuzimu akiwa madarakani, kulikuwa na mgao wa maji na hakuna alilofanya mpaka mvua iliponyesha hawana majibu! Je wamejenga mabwawa makubwa ya kutunza maji wakati wa mvua ili kukitokea ukame kuwe na reserve hawana majibu!

Hili la mgao wa umeme sukuma gang wanamlaumu muhuni wa Msoga line @januarymakamba kwamba ndio chanzo. Ukiwauliza kwanini mwendakuzimu atie 7t kwenye mradi mpya wa maji utakaozalisha 2,115mg, wakati maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi, na asiweke 3t kwenye mradi wa umeme wa gas ambao tayari ulikuwa unazalisha umeme, maana ungeweza kuzalisha hizo megawati wanazotaka kuzalisha kwenye maji? Ukifika hapo wanasema ww ni chagadema, na Mbowe lazima ale mvua miaka 30 kwani mahakama ni huru ndio maana zimemfunga Sabaya!!!
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,276
2,000
Utajuwaje nawe ukitoka ni nyuma ya pick up kwenda kununua pumba shemeji akifurahi anakuachia guta siku hiyo linatembea kwa matairi matatu!
Miezi 8 uliokaa burigi naona hata akili zimebadilika umekuwa kama wenyeji wa burigi
 

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
415
500
Pole sana kamanda kwa umasikini.

Ila maboss zako kina Mbowe, Msigwa, Sugu, John Heche, Mnyika na Lissu wao siyo masikini tena chini ya utawala huuu huu wa CCM.

Wanakula mema ya nchi.

Akili kichwani. Wewe utabaki kutumika kwenye maandamano tu na kutukana mitandaoni.
Mmawiya kumbe wewe Nusu dengu Nusu Dona.kumbe kichwa I zimepuruka. Yaonyesha wewe unatetea Maisha yaleo. Hujali vijukuu vyako hapo baadae. Tunaangalia mustakabali wakesho yetu. HAO ulio watajua NI wapambanaji WA Maisha ya wajao. Hawajigikirii Leo yetu. Amakweli Leo ndo nayasadiki maneno ya wahenga,,,
Intellectuals solve problems, geniuses prevent them.
,,,(Wasomi hutatua shida, fikra zinawazuia.),,Sijui kama Tafsi yangu iko sahihi !!! Kalambwe na wale walumumba. Kabinie watwange mabwana zako wachimia tumbo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom