Hivi serikali ya JK haiuoni uchochezi unaofanywa na RADIO IMANI?

Status
Not open for further replies.
Inapatikana ktk frequnce ngapi?Lakini mtu anawezaje kutangaza kitu kama hajafanyia uchnguzi?Tunafikishiwa taarifa sawa..anaetufikishia habari ameambiwa?Amesikia?Au ameona?Sababu kwa tanzania mtu atakuletea kiswaili Cha sasa(Navyoona mimi)Sasa najiuliza unavyoona ww.au unavyo fikiri ww kiswahili fasaha?Tujue tz tunapat habari zakufikirika?Niayo tuu.heri ya 2012.
 
huyu kaleta umbeya hapa amedhani hili ni gazeti la uwazi.chuki tu zisizo na msingi.unataka vya kanisani tu vya upande wa pili ni mwiba kwako...... nyo..................................k yako.
 
Allah (SWT) ametufahamisha ya kuwa amewaumba majini kutokana na moto na hiyo ni katika aya tofauti mfano, Neno lake Allah ( S W T): "Na majini tumewaumba hapo mwanzo kutokana na moto wa upepo wenye joto kubwa", Al- Hajar 27 . Na akasema katika aya nyingine katika sura ya Ar-Rahman, aya ya 15: "Na akaumba majini kutokana na ( ncha ) ya ulimi wa moto".

Vilevile Mtume (SAW) ameeleza kuhusu namna walivyoumbwa majini wakati aliposema: "Wameumbwa malaika kutokana na nuru, wakaumbwa majini kutokana na ulimi wa moto. Na wameumbwa binadamu kutokana na namna mlivyoelezwa."Allah (SWT) ametufahamisha ya kuwa amewaumba majini kutokana na moto na hiyo ni katika aya tofauti mfano, Neno lake Allah ( S W T): "Na majini tumewaumba hapo mwanzo kutokana na moto wa upepo wenye joto kubwa", Al- Hajar 27 . Na akasema katika aya nyingine katika sura ya Ar-Rahman, aya ya 15: "Na akaumba majini kutokana na ( ncha ) ya ulimi wa moto".

Vilevile Mtume (SAW) ameeleza kuhusu namna walivyoumbwa majini wakati aliposema: "Wameumbwa malaika kutokana na nuru, wakaumbwa majini kutokana na ulimi wa moto. Na wameumbwa binadamu kutokana na namna mlivyoelezwa."

majini wana majina mbali mbali katika lugha ya kiarabu tutataja baadhi yake:
( a ) Jinni : Anapokusudiwa jinni tu. Na maana ya neno jinni ni kitu kisichoonekana au kilichofichika.
( b ) Aamir : Anapokusudiwa yule anaishi katika majumba ya watu.
( c ) Shetani : Anapokuwa na shari
( d ) Rauhaan : Yule anaewatokezea watoto
( e ) Afriit : Anapokuwa na nguvu za kupindukia

3. Je majini wana uwezo wa kujibadilisha?

Majini wana uwezo huo, tena uwezo mkubwa mno wa kujigeuza katika maumbile tofauti kama vile kuwa kama majoka, nge, farasi, ng'ombe, ngamia, kondoo na ndege. Na pia wana uwezo wa kujigeuza katika maumbile va kibinadamu.

4. Uwezo wa majini

Majini wana uwezo na nguvu ambazo ni zaidi ya alizonazo binadamu na miongoni mwa nguvu zao hizo ni ule uwezo wao mkubwa wa kusafiri. Na mfano wa haraka haraka ambao tungependa kuutoa ni ule wa ahadi ya mmoja kati ya Majini wenye nguvu, Afriit, alipomwahidi Nabii Suleyman (AS) katika baraza lake, kwamba angeweza kumletea kiti cha enzi cha Malkia wa Yemen kutoka huko mpaka pale walipo ambapo ni Palestina kabla ya Nabii Suleyman (AS) kuvunja kikao chake. Allah (SWT) anatuhadithia katika suratun - Naml aya ya 38, 39: "( Suleyman akakusanya mawaziri wake akasema): 'Enyi wakuu! Ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajakuja kwangu, hali ya kuwa wamekwisha silimu?' Mjasiri mmoja wa majini akasema: 'Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo na mimi hakika ninazo nguvu na uwezo wa hilo na ni mwaminifu'". Miongoni mwa nguvu zao pia ni ule uwezo wa kupaa mbali mbinguni kusikiliza habari. Na hiyo ilikuwa kabla ya kuja Mtume Muhammad (SAW).

5. Je majini hufa?

Hilo halina shaka kwani nao wanajumuishwa kwenye tamko la Allah (SWT) katika Qur-an, suratur- Rahman 26, 27: " Kila kilichoko juu yake ( ardhi na mbingu ) kitatoweka; na inabaki dhati ya Mola wako ( tu Mwenyewe ) Mwenye utukufu na heshima ". Na Mtume (SAW) amesema katika dua: "Najilinda kwa utukufu wako, ambapo hapana mwingine apasaye kuabudiwa kwa haki isipokua wewe ambaye hufi, lakini majini na watu wote wanakufa", imepokewa na Bukhari. Hivyo, kutokana na ushahidi uliotangulia majini hufa kama wanavyokufa viumbe wengine lakini Iblisi yeye amepewa muda mrefu wa kuishi mpaka siku ya kiyama, kama inavyoeleza Qur-an Tukufu, Al-A'raaf 14, 15: "Akasema ( Shetani ), 'Nipe muda ( nisife ) mpaka siku watakapofufuliwa ( viumbe )'. Akasema( Allah SWT ), 'utakua ni miongoni mwa waliopewa muda ( lakini si mpaka wakati ulioutaja ).'"

6. Ni vipi wanavyotembea mashetani?

Katika hili Mtume (SAW) anatufundisha kwa kusema: "Yeyote kati yetu asitembee na kiatu kimoja kwani shetani hutembea na kiatu kimoja."

7. Ni muda gani ambao wanatapanyika mashetani?

Wanatapanyika wakati unapoingia usiku na hiyo ni kutokana na uthibitisho wa hadithi ya Mtume (SAW) aliposema, "Unapoingia usiku au linapoingia giza wazuieni watoto wenu ndani, kwani mashetani hutapanyika wakati huo, litakapopita lisaa limoja baadaye muachilie, na fungeni milango na mumtaje Allah (SWT), kwani hakika shetani hafungui mlango uliofungwa." Imepokewa na Bukhari kutokana na Jabir bin Abdallah.

8. Wapi kipo kiti cha enzi cha Iblis?

Kiti cha enzi cha Iblis kipo baharini. Imepokewa na Imam Ahmad kutoka kwa Jabir kwamba Mtume (SAW) amesema, "Hakika Iblisi ameweka kiti chake cha enzi kwenye maji, kisha hutuma majeshi yake."

9. Mayoe ya Iblisi

Ametoa mayoe Iblisi mara nne:*

( a ) Kapiga yoe wakati alipolaaniwa
( b ) Wakati alipotolewa kwenye pepo
( c ) Wakati alipopewa utume Mtume Muhammad (SAW)
( d ) Wakati ilipoteremshwa Suratul - Fatihah

10. Mambo aliyotangulia kufanya Iblisi kabla ya binadamu

( a )Iblisi ndiye aliyetangulia kulia kwa sauti
( b )Iblisi ndiye aliyetangulia kulinganisha ubora wa viumbe, yaani yeye ndiye wa mwanzo kujilinganisha na mwanadamu na kujiona bora.
( c )Naye ndiye aliyeanzisha nyimbo na kuimba
 
Majini ni viumbe miongoni mwa viumbe wa Allah (SWT) ambao wamepewa majukumu ya kiibada, lakini majukumu yao ya kiibada hayalingani sawa na majukumu ya kiibada waliyopewa wanadamu isipokuwa majukumu yao yanafanana na ile hali yao ya kimaumbile walioumbiwa. Anasema Ibn Taimiyah: "Majini wameamrishwa katika mambo ya kimsingi katika ibada kwa maumbile yao. Kwani wao hawapo sawa sawa na wanadamu katika hukumu za kidini, haiwezekani kuwa waliyoamrishwa na waliyokatazwa yawe sawa sawa na yale waliyoamrishwa na kukatazwa wanadamu. Lakini tu wao wanashirikiana na wanadamu katika ile hali ya kuwa wao pia wamepewa majukumu ya kidini, kama mambo ya halali, haramu n.k. Hili kwa ninavyofahamu halina utata kwa waislam wote." [ Majmuu'atil - Fataawiy 4:233 ]

1. Je kulikuwepo na Majini mitume / manabi ?

Swali hili aliulizwa Adhwihaak ya kwamba, je kuna waliokua mitume au manabii miongoni mwa majini kabla ya Mtume Muhammed (SAW)? Akajibu kwa kusema, "Hivi hamkusikia tamko la Allah (SWT) lisemalo 'Enyi makundi ya majini na wanadamu, Je hawajakufikieni Mitume miongoni mwenu kukubainisheni aya zangu ..' Al - An'am 130." Aya hii kwa alivyoona Adhwihaak inafahamisha ya kwamba Allah (SWT) alipeleka majini wakiwa ni Mitume. Lakini yeye amepingwa kwamba hii aya haikuweka wazi mitume waliyotajwa walikua ni katika jamii ipi mojawapo, majini au watu, kwa sababu neno lake Allah (SWT) "miongoni mwenu" inawezekana kwamba mitume walitumwa katika jamii zote hizo mbili na inawezekana ikawa mitume walikuwepo katika jamii moja lakini kwa wote hao. Katika jambo hili wanazuoni walitofautiana katika makundi mawili wengi wao walikubaliana ya kwamba mitume hawakuwepo katika jamii ya majini kamwe, mitume walikuwepo tu katika jamii ya wanadamu.Ni wanazuoni wachache tu ndio walioonelea kwamba kulikuwepo na mitume waliyopelekwa katika jamii ya majini, na miongoni mwa walioonelea hivyo ni huyu mwanazuoni aitwaye Adhwihaak.

2. Utume Wa Nabii Muhammad (SAW) kwa majini na wanadamu

Wanazuoni wote wa kiislam wamekubaliana kwamba Muhammad (SAW) alitumwa na Allah (SWT) kwa majini na watu wote. Na hivi ndivyo ilivyo kama asemavyo Ibn Taymiyah - kwani Qur-an inashindana na jamii ya majini na pia jamii ya wanadamu. Allah (SWT) anasema: "Sema hata wakijikusanya majini yote na watu wote, ili kuleta mfano wa hii Qur-an, basi hawangaliweza kuleta mfano wake, hata kama watasaidiana wao kwa wao." Al - Israa 88. Na kundi mojawapo la majini lilisilimu mara tu baada ya kusikia Qur-an tukufu: "Sema imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikia Qur-an likasema ( kundi hilo ), 'Hakika sisi tumesikia Qur-an ya ajabu inayoongoza kwenye uongofu, tukaiamini, na kamwe hatutamshirikisha Mola wetu na yeyote yule ....'" A1 - Jinn 1 - 2. Aya zote hizi za Qur-an zinafahamisha wazi kwamba Mtume (SAW) alitumwa kwa majini na watu wote. Ama kuhusu upande wa hadithi za Mtume (SAW) kuna uthibitisho wa wazi katika sahihi mbili Bukhari na Muslim kutokana na hadithi ya Jabir bin Abdallah (RA) kwamba Mtume (SAW) amesema: "Nimepewa mambo matano ambayo hajawahi kupewa Mtume yeyote yule kabla yangu - Mpaka alipofikia: Na kila Mtume alikua akipelekwa kwa kabila lake tu lakini mimi nimetumwa kwa watu wote." Na akasema Jauhariy kwamba makusudio ya watu wote hapa ni kwa majini na wanadamu wote pamoja. Hivyo basi Mtume Muhammad (SAW) alitumwa kwa wanadamu wote pamoja na majini akiwa ni Mjumbe Mwonyaji. Na huu ndio ubora wake uliowazidi mitume wote waliotangulia.

3. Mila na madhehebu ya majini

Allah (SWT) ametufahamisha ndani ya Qur-an aliposema, "Katika sisi wapo ( majini ) wema na kuna miongoni mwetu ( majini ) kinyume na hao tumekua njia mbali mabli." Al - Jinni 11. "Nasi ( majini ) wamo miongoni mwetu waislamu na wamo miongoni mwetu waliokengeuka. Waliosilimu hao ndio waliotafuta uongofu. Na wanaokengeuka hao watakuwa kuni za Jahannam." Al- Jinn 14 - 15 . Hivyo basi Allah (SWT) katufahamisha kwamba majini nao wana mila na itikadi tofauti kama vile wanadamu walivyo, kuna waislam, makafiri na madhehebu mbalimbali.

4. Je majini nao wanalipwa kutokana na vitendo vyao?

Wanazuoni wanatofautiana katika hili. Kuna pande mbili za maoni:

Upande wa kwanza: unaona kuwa majini watalipwa kwa wema watakaoufanya, na wataadhibiwa kwa maasi yao na hayo ni maoni ya Imam Malik, Shafii, Ahmad na Ibn Abbas.

Kundi la pili: linaona kwamba majini hawatakuwa na malipo yeyote isipokuwa kukombolewa na moto wa Jahannamu. Kisha wataambiwa wawe mchanga kama vile itakavyokuwa hali ya wanyama. Na hayo ni maoni ya Imam Abu Hanifa, Laith, Abu Salim na wengineo.

Lakini usahihi ni kwamba majini watalipwa kwa vitendo vyao vizuri au vibaya kwa ushahidi wa Qur-an, Allah (SWT) anasema: "Na wote wana daraja ( malipo ) sawa kwa yale waliyoyatenda. Na Mola wako si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda." Al - An'am 132.

Je kuna ndoa kati ya majini na watu?

Imeenea katika baadhi ya maeneo kwamba kuna mtu ameoa jini; au kwamba mwanamke wa kibinadamu kaolewa na jini au ameposwa, kuna ukweli gani katika jambo hili? Ni kweli kwamba ndoa huenda ikawa kati ya mwanadamu na jini, Allah (SWT) anasema katika Qur-an Tukufu, "Nashirikiana nao katika mali ( zao ) na watoto ( wao )." Al - Israa 64. Akasema Mtume (SAW), "Anapokutana na mume na mkewe pasi na kutamka jina la Allah, basi shetani hushirikiana na huyo mume katika tendo la ndoa." Hadithi hii ameitoa Shubly katika kitabu Ahkamul - Murjaan. Na amepokea Hafidhi bin Jarir kutoka kwa Ibn Abbas (RA) kwamba Mtume (SAW) amesema: "Pindi amwingiliapo mume mkewe wakati akiwa katika hedhi, shetani humtangulia na ( mkewe ) akishika mimba basi atazaa mtoto ( khanithi ). Na ( makhanithi ) ni watoto wa majini." Na kuhusiana na hilo amesisitizia Ibn Taymiyah kwamba: "Inatokea kujamiiana kati ya majini na wanadamu na ikiwa ni hivyo basi huzaliwa watoto mara nyingi ( kwa kujamiiana huko ) kwa inavyofahamika." Wanazuoni wa mambo ya historia wameelezea kuhusu habari zilizotangulia zinazohusiana na ndoa kati ya majini na binadamu tutataja kisa kimojawapo, kisa kilichotolewa na Abu Bakar bin Abid-Dunia, kutokana na Abu Yusuf Saruji kwamba yeye amesema: "Alikuja mwanamke mmoja kwa bwana mmoja huko Madina, akamwambia: 'Hakika sisi tumeshukia hapa jirani je utanioa?' Basi yule bwana akamwoa, kisha baada ya muda yule jinni ( mke ) akamwambia yule bwana, 'umefika wakati wa kuondoka, basi naomba unipe talaka.' Na alikua akimjia usiku katika maumbile ya mwanamke. Ikatokea baada ya kumpa talaka akamwona siku moja katika mtaa mmoja ( jinni ) huyo akiokota nafaka zilizoanguka kutoka kwa wauzaji wa mazao. Akamwuliza ( jinni huyo ), 'Je unazihitaji nafaka hizi?' Yule jini akaweka mkono wake kichwani kuonyesha kuumbuka, kisha akainua uso wake akamtazama yule bwana, akamwuliza, 'umenionaje?' Yule bwana akajibu, 'kwa jicho hili', yule jini akanyoosha kidole chake kwenye lile jicho la yule bwana na kulipofua."

Na pamoja na kwamba kuna visa vingi vilivyopokewa kuhusu kuwepo ndoa kati ya wanadamu na majini, isipokua kuna wanaodai ya kwamba Majini wana asili ya maumbile ya moto, na wanadamu wana asili ya vitu vinne ( Hewa, maji, udongo na joto ), hivyo basi kuwepo kwa asili ya moto katika majini kunazuia kukaa yale ( manii ) ya binadamu katika tumbo la uzazi la jini, kutokana na moto uliopo.

Imepokewa na Ahmad kutoka kwa Ubaid bin Umair kwamba Iblis alisema: "Ee Mola wangu, umenitoa mimi peponi kwa sababu ya Adam, na mimi sitomweza isipokua kwa nguvu za ufalme wako". Allah (SWT) akamwambia: "Basi tutakusalitisha nae. " Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Basi hatopatikana mtoto wa kibinadamu isipokua atazaliwa na mtoto wako vile vile." Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Vifua vyao vitakua ndio sehemu yako na utatembea katika mishipa yao ya damu." Na hiyo ni sawa na kauli ya Allah (SWT) katila Qur-an Tukufu aliposema: "Na uwakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali zao na watoto wao, na waahidi ahadi za uongo. Na shetani hana ahadi isipokua ni udanganyifu." Al - Israa 64.

Akasema Adam: "Ee Mola wangu umenisalitishia Iblisi na mimi sitoweza kujikinga nae isipokua kwako." Allah (SWT) akamwambia: "Kila mtoto atakayezaliwa kwako nitamwekea mlinzi wa kumlinda na mashetani wabaya." Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Jema moja nitalipa mara kumi na zaidi, na baya nitalipa mara moja na ninaweza kulifuta." Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Mlango wa toba sitaufunga kwa mja wangu akiwa bado yupo hai." Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Ninasamehe makosa yote wala sijali." Hapo Adam akasema: "Imetosha." Allah (SWT) anasema: "Enyi waja wangu mliopindukia katika maovu msije mkaiacha rehema ya Allah (SWT). Hakika Allah (SWT) husamehe madhambi yote." Hivi ndivyo alivyo mwanadamu na shetani ambaye ni katika majini.

( a ) Je kujamiiana kati ya majini na wanadamu kuna wajibu wa mtu kuoga janaba?

Aliuliza swali hili Abul-Maaliy wa dhehebu la Hanbali, kwamba kuna mwanamke mmoja alisema: 'kuna jini anayenitokezea kama vile awavyo mume na mke, je? nawajibika kuoga janaba?' Hapo baadhi ya wafuasi wa Imam Hanbal walisema, 'huyo hatooga janaba.' Abu-Maaliy akasema: 'Hata kama huyo mwanamke angesema, 'ameniingilia mimi jinni kama vile mwanaume afanyavyo' pia halazimiki kuoga janaba, hiyo ni kutokana na kukosekana ushahidi wa kuingiliwa na kushusha, hivyo basi hali hiyo ni sawa na kuota ndoto.'

( b ) Nini hukumu ya mke aliyetoweka mumewe kwa kutekwa na jini?

Kisa kama hiki kilitokea wakati wa utawala wa Khalifa wa pili Umar bin Al*khatab (RA). Kuna bwana mmoja alikwenda kusali sala ya Isha akiwa na jamaa zake, akatoweka. Mke wake akenda kwa Umar bin Al*khatab (RA) akamwelezea kuhusu mume wake. Umar (RA) akawauliza jamaa zake kuhusu maelezo ya yule mwanamke, wakasema ni kweli mume wake katoweka. Hivyo Umar (RA) akamwamuru yule mwanamke angojee na kumsubiri mumewe kwa muda wa miaka minne. Yule mwanamke akafanya hivyo. Baada ya miaka minne kupita, akarudi tena kwa Sayyidna Umar (RA) akamwambia kwamba miaka minne imepita na hakuna dalili yeyote ya kuonekana mume wake. Sayyidna Umar (RA) akawauliza jamaa zake. Nao wakamwambia kuwa ni kweli bado hajatokea. Hivyo akampa ruhusa ya kuolewa. Alipoolewa tu, yule mume wake wa kwanza akatokea, ikabidi aende kwa Sayyidna Umar (RA) akamwambia: 'Mtu unatoweka bila ya jamaa zako kuwa na taarifa yeyote kuhusu wewe.' Yule bwana akamwambia nilikuwa nina udhuru, Sayyidna Umar (RA) akamuuliza: 'udhuru gani huo.' Yule bwana akasema, 'siku moja nilipokuwa nakwenda msikitini kusali sala ya Isha nilikumbwa na jinni mwanamke - Nikawekwa kwao muda mrefu. Wakavamiwa na majini waislam. Waliovamiwa wakashindwa vita na wengine kuuawa na wengine wakatekwa, nami nikawa ni katika mateka. Wakaniuliza kuhusu dini yangu. Nikawaambia kwamba mimi ni mwislam. Wakaniambia kwamba wao pia ni waislam, hivyo si halali kwao kunifanya mimi ni mateka. Hivyo wakaniambia nichague kati ya kuondoka kurejea kwetu au kukaa nao, ndipo nilipochagua kurejea kwetu. Wakawa wakinimulikia usiku kwa vijinga vya moto na mchana nikifuata mwelekeo wa upepo kurudi.' Umar (RA) akamuuliza, 'ulikuwa ukila nini?' Akasema: 'kila kilichokua hakitajwi jina la Mwenyezi Mungu ( yaani nyamafu ).' Akamuuliza tena, 'Nini ulikua ukinywa?' Akajibu: 'kila kilichokuwa kama mvinyo.' Hapo Umar (RA) akamwambia kwamba anaweza kumrudia mke wake au achukue mahari yake kutoka kwa yule mkewe.

(c) Ni kipi chakula cha majini?

Kuna tofauti nne kuhusu chakula chao: Kuna wanaosema kwamba majini hawali wala hawanywi, kuna wanaosema kwamba baadhi yao wanakula na kunywa na baadhi nyingine hawanywi wala hawali. Kuna wanaosema kwamba majini wote wanakula na kunywa na hii ndio rai sahihi kulingana na kitabu kitakatifu Qur-an na sunna za Mtume Muhammad (SAW) aliposema, "Shetani atakuwa anakula na mtu, mpaka atakapotaja jina la Allah (SWT), shetani atatapika kile alichokula tumboni." Na katika sehemu nyingine alisema, "Msiende haja kwa kutumia samadi au mifupa kwani hivyo ni vyakula vya ndugu zenu majini." Na katika sehemu nyingine anatukataza kula kwa mkono wa kushoto kwani yeye alisema, "Anapokula mmoja wenu atumie mkono wake wa kulia, na anapokunywa atumie vilevile mkono wake wa kulia, kwani shetani anakula na kunywa kwa kutumia mkono wa kushoto." Huo ni ushahidi wa kutosha wa kuonyesha kwamba majini wanakula na kunywa.

Ni yapi makazi ya Majini?

Majini wanaishi katika mgongo wa ardhi, na wanapatikana kwa wingi katika majangwa na sehemu za takataka, sehemu zenye najisi, chooni na makaburini. Na hii ndio sababu hasa ya wale waganga ambao wana uhusiano na mashetani kupenda kuwashauri wateja wao kupeleka vitu vyao na uchawi wao katika maeneo hayo.

Zipo hadithi za Mtume (SAW) ambazo zinakataza watu kuswali chooni, na hiyo ni kutolana na najisi iliyopo sehemu hiyo, na pia ndiyo makazi ya mashetani. Vile vile majini hupatikana kwa wingi mno katika maeneo yanayokithiri maasi kama vile masokoni. Na hiyo ndiyo sababu Mtume (SAW) akamuusia mmoja wa masahaba wake akamwambia, "Ikiwezekana usiwe ni wa mwanzo kuingia sokoni, wala wa mwisho kutoka, kwa sababu humo sokoni ndipo penye harakati za shetani, na ndipo anaposimika bendera yakc." Imetolewa na Muslim.

Na kama ilivyo vile vile mashetani hukaa katika majumba ya binadamu, na Bismillahi tu ndiyo inayowakimbiza. Amepokea Muslim na Abu Dawood kutoka kwa Jabir kwamba Mtume (SAW) amesema: "Yeyote atakayeingia nyumbani kwake akataja jina la Allah (SWT) wakati anaingia na wakati anapokula shetani husema: ‘Leo hapana malazi hapa wala chakula’, na atakapomtaja Allah (SWT) wakati anapoingia nyumbani, na asitaje wakati wa kula, shetani husema, 'Mmewahi chakula lakini hakuna kulala', na mtu asipotaja jina la Allah (SWT) anapoingia nyumbani kwake shetani husema kuwaambia wenzake, ‘mmewahi chakula na malazi’."

Na mahali pengine ambapo shetani hupenda kukaa `ni kati ya jua na kivuli', na hiyo ndio sababu ya Mtume (SAW) kutukataza kukaa katika sehemu hizo, kama ilivyopokewa katika hadithi.

Vipando vya majini?

Mtume (SAW) ameelezea kwamba majini nao wana vipando, na hiyo ni katika hadithi sahihi iliyotolewa na Muslim kutokana na Ibn Mas'ud (RA) kwamba Majini walimwomba Mtume (SAW) awaombee chakula, ndipo Mtume (SAW) akasema: "Mtakula kila mfupa uliotajwa jina la Allah (SWT) ambao utakua ni bora kuliko nyama, na kila samadi itakua ni chakula cha vipando vyenu." Katika hadithi hii kuna dalili ya wazi ya kuonyesha kwamba Majini nao wana vipando.

Elimu na maarifa waliyonayo Majini

Kuna baadhi ya watu ambao wanadai kutibu wagonjwa na kwamba wao wamejifunza tiba hiyo kupitia kwa majini. Na kweli tokea zamani tunasikia kwamba kuna watu wa namna hii wanye uwezo wa kutibu baadhi ya maradhi sugu kama yanavyofahamika. Na miongoni mwa visa vinavyofahamika ni kile kilichosimuliwa na An-nadr bin Amril-Harithiy, aliposema: "Katika zama za ujahiliyah tulikua siku moja karibu na kisima, nikamtuma binti yangu na chombo ili anitekee maji, akakawia, tukamtafuta lakini hatukumwona mpaka tukakata tamaa. Akasema: 'Naapa kwa Allah (SWT) kwamba siku moja nilikua nimekaa mbele ya baraza yangu, akanitokezea Sheikh mmoja, alipoinama kuniangalia mara akawa ni binti yangu. Nikasema: 'Binti yangu.' Akasema: 'Binti yako ndiyo!' Nikasema: 'Ulikua wapi binti yangu?' Yule binti akasema, 'ile siku uliponituma kisimani, alinichukua jinni akawa ananizungusha huku na kule, nikawa nipo kwao mpaka ilipotokea vita kati ya makundi mawili ya majini. Akaahidi kwamba wakishinda vita atanirudisha. Wakashinda ndipo aliponirudisha.' Lakini akawa binti huyo amebadilika rangi yake ya mwili na akawa amekonda sana. Akakaa kwa muda akaanza kubadilika kuwa katika hali ya kawaida, akachumbiwa na mabinamu zake tukamwozesha. Lakini lile jinni likawa limempa ishara ya kumwita kwa moshi pindi panapotokea matatizo yeyote. Basi yule mume wake akawa anamkera na kumwambia wewe ni jini, shetani wala si mtu. Basi yule binti akawasha moshi, yule mume akasikia sauti inamwambia, 'Una nini na huyu ukimsogelea atakutoboa jicho. Nimemchunga tokea wakati wa ujahiliyah kwa maarifa yangu, na katika uislam kwa dini yangu.' Yule mume akamwambia, 'Huwezi ukajitokeza tukakuona?' Yule jinni akajibu, 'Haturuhusiwi. Hakika baba yetu aliomba mambo matatu. Tuone lakini tusionekane, tukae katika tabaka za ardhi, na aishi mmoja wetu mpaka atakapofikia kuwa mtu mzima, kisha atarudi tena kuwa kijana mdogo.' Yule bwana akamwuliza: 'Je unaweza kunipa dawa ya homa?' Lile jinni likajibu: 'Ndio. Unamjua yule mdudu mdogo katika maji, ambaye anafanana na buibui?' Yule bwana akasema, 'Namfahamu.' Basi yule jinni akamwambia, 'Mchukue halafu tengeneza nyuzi kutokana na miguu yake kisha ufunge katika mkono wako wa kushoto.' Yule bwana akafanya hivyo. Akawa kama aliyefunguliwa kamba ya shingo."

Pia Zayd bin Wahab alisema, "Tulipigana vita tukashuka katika kisiwa kimoja, wakawasha moto, pakawa pana chumba kikubwa, akasema mmoja wao, 'mimi naona kuna chumba kikubwa, pengine mnawaudhi waliomo ndani ya chumba hiki.' Wakazima moto wao. Akatokezewa usiku akaambiwa, 'Hakika wewe umeihami nyumba yetu tutakufundisha tiba ambayo itakusaidia, atakapokujia mgonjwa basi chochote utakachomwambia kuwa ni dawa basi atapona.' Ikawa siku moja akajiwa na mtu mwenye tumbo kubwa, alipokua amekaa katika msikiti wa Kufah. Yule mtu akamwomba ampatie dawa ya tumbo lake. Akamwambia, 'Hivi jamani hamshangai kumwona mtu ananiuliza kuhusu dawa naye atakufa leo kwa kula matunda?' Basi siku ile ilipopita watu wakamfuata kumwambia, 'Wewe ni mwongo mbona yule bwana hajafa?' Akawaambia, 'Muulizeni hali ya ugonjwa wake.' Wakasema amekwisha pona.' Akawaambia, 'Mimi nilimtisha asile sana!' Kimetolewa na Abadalla bin Muhammad A-Qurashiy.

( a ) Ipi sababu kuu ya uadui uliopo kati ya shetani na wanadamu?

Uadui kati ya shetani na mwanadamu ulianzia mbali mno tokea pale Allah (SWT) alipomuumba Adam (AS) na kumpulizia roho kisha akawaambia Malaika wamsujudie. Na alikua Iblisi akifanya ibada pamoja na Malaika naye akawa ni miongoni mwa walioamrishwa, lakini yeye alikataa na akafanya kiburi na wala hakusujudu.Wakati Allah (SWT) alipomwuliza sababu ya kukataa kwake kutii amri ya kumsujudia Adam (AS) alijibu kwa kusema: "Mimi ni bora kuliko yeye umeniumba kwa moto na yeye ukamuumba kwa udongo." Na hapa hasa ndio kiini cha uadui uliopo kati ya shetani na binadamu. Na picha nzuri ya historia ya uadui huo ni kama vile ilivyotolewa katika Qur-an Tukufu, Allah (SWT) anatuhadithia: "Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika msujudieni Adamu". Basi wakasujudu isipokua Ibilisi hakuwa miongoni mwa waliosujudu. Allah (SWT) akasema: "Nini kilichokuzuia kumsujudia nilipokuamrisha?" Akasema: "Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo." Akasema Allah (SWT): "Basi shuka huko, haikufai kufanya kiburi humo. Haya toka; hakika wewe ni miongoni mwa wadhalili - duni." Akasema: "Nipe muda ( nisife ) mpaka siku watakapofufuliwa viumbe." Akasema Allah (SWT): "Utakuwa miongoni mwa waliopewa muda, ( lakini si mpaka wakati huo)."Akasema: "Kwa kuwa umenihukumia upotovu basi nitawakalia waja wako katika njia yako iliyonyooka ( ili niwapoteze ), kisha nitawafikia mbele yao na nyuma yao na kulia kwao na kushoto kwao; wengi katika wao hawatakuwa ni wenye kushukuru." Akasema Allah (SWT): "Toka humo hali ya kuwa ni mwenye kudharauliwa na mwenye kufukuzwa. Atakaekufuata miongoni mwao ( nitamtia motoni ) niijaze Jahannamu kwa ninyi wote." Kisha Allah (SWT) akasema kumwambia Nabii Adam (AS): "Na wewe Adam kaa peponi pamoja na mkeo, na kuleni mnavyopenda, lakini msiukaribie mti huu msije mkawa miongoni mwa waliodhulumu nafsi zao." Basi shetani; ( naye ni yule yule Iblisi ) aliwatia wasi wasi ili kuwafichulia aibu zao walizofichiwa, na akasema: "Mola wenu hakukukatazeni mti huu ila msije kuwa Malaika au kuwa miongoni mwa wakao milele ( msife )." Naye akawaapia kwamba: "Kwa yakini mimi ni mmoja wa watoao ushauri mzuri kwenu." Basi akawateka wote wawili kwa kuwahadaa. Na walipoonja mti ule, aibu zao ziliwadhihirikia, na wakaingia kujibandika majani ya ( miti ya huko ) peponi. Na Mola wao akawaita ( akawaambia ): "Je sikukukatazeni mti huu na kukuambieni ya kwamba shetani ni adui aliye wazi?" Wakasema: "Mola wetu! Tumezidhulumu nafsi zetu, na kama hutotusamehe na kutuhurumia, bila shaka tutakua miongoni mwa wenye hasara kubwa." Allah (SWT) akasema: "Shukeni ( katika ardhi ), ninyi kwa ninyi maadui. Na makao yenu yatakuwa katika ardhi na starehe yenu pia." Al - A'raaf 11 – 23. Cha msingi tunachosoma katika aya hizi ni kwamba uadui uliopo kati ya shetani na mwanadamu hautomalizika wala kuondoka kwani yeye shetani anaona kwamba sababu ya yeye kufukuzwa kutoka kwenye neema za Allah (SWT) ni Adam. Hivyo ni lazima ampoteze yeye na kizazi chake na hii ndio sababu hasa ya Qur-an kutuhadharisha mno dhidi ya shetani huyu.

( b ) Ni maasi gani yanayompendeza mno Iblisi?

Anasema Mtume (SAW): "Hakika mamlaka ya Iblisi yapo kwenye bahari, kisha huwatuma majeshi yake, ili wawafitinishe watu. Katika fitna kubwa huja mmoja wao kumwambia, 'Nimefanya hili na lile.' Iblisi anamjibu, 'Hamna kitu.' Kisha anakuja mwingine anasema vilevile, naye humwambia pia, 'Hujafanya lolote.' Kisha anakuja mwingine anamwambia, 'Sikumuacha mtu yule mpaka nimehakiklsha ametengana na mkewe.' Hapo Iblisi humwinamia jinni huyo na kumwambia,'Wewe ndio.'" Imepokewa na Muslim.

source:MAJINI 9
 
Kichekesho ni Cd anazotoa Shekh ILUNGA yaani siasa ya dini ya uislam kuchafua uikristo.TUTAFIKA
 
Mtoa mada analake tu.Haishangazi kuona mnalalamikia radio imani.Tunajua hampendi kusikia wala kuona waislam wanaendelea katika nyanja zozote. Hilo litaendelea kuwauma na mpaka mnaingia kaburini nuru ya Uislam hamtaweza kuizima. Na kwataarifa yenu radio Imani iko 80% ya nchi yote,hivyo kama unadhani ipo Dar na Moro basi mmenoa. Kazi iliyobaki ni kumalizia 20% iliyobaki.Wenye roho mbaya na Uislam mpo? TV Imani nayo January hii itakuwa hewani. Kwa taarifa yenu tuko kamili,na kama mlidhan hatuwezi hapo mmechemsha.

hivi wewe umeona mkristo gani ana muda na upuuzi wenu hatuna time tuna time ya kufanya maendeleo nyie endeleen na huo upuuzi na nuru ya uislam haiziwi na wakristo ila nyie wenyewe.dini si ushindani ka chadema na ccm ni tofauti sana. hata hiyo redio isambae afrika nzima msipobadilika mtakuwa mnatusaidia kujua ni kiasi gani uislam ulivyo na si ukristo ulivyo jaribuni kujifunza kutoka uislam wa mataifa yaliyoendelea.dini sio fujo
 
TV imani imezinduliwa na SEIF wa CUF kwa ajili ya kuchochea na kudai znz na bara iwe nchi ya kiislamu na Seif awe rais
Mazungumzo ya Seif na Shehe Basaleh Mstiki wa idrisa na Shehe Ponda wa SHURA YA MAIMAMU
 
Mnaichukia radio imaan nani anawaambia muisikilize si muache tusikilize wenyewe?asikuambia radio imaan ina raha kuisikiliza mwanzo mwisho ni elimu tu bila mipaka hakuna miziki,inafichua yale ambayo kwa miaka yote hayasemwi.big up radio imaan,eti wengine wanasema haifiki kokote,waulize ndugu zako walio mikoa tofauti wakuambie.isikilize radio imaan ukiwa morogoro,dar,unguja na pemba,arusha ,kilimanjaro,tanga,pwani,mbeya ruvuma,mbeya tabora,kigoma,mwanza,dodoma,singida, mtwara nk safari hii mtapasuka,maana mmeshazoea kuona waislam wanakuwa nyuma kwa kila jambo sasa hv mkondo umegeuka,ujinga wenu unaanikwa.deci ,babu wa loliondo,na mkubwa wenu tayari jiwe limemgonga kaanza kuweweseka,mimi nashangaa vyuo vinaibuka kama uyoga kumbe biashara yenyewe ndiyo hiyo.

nadhani una matatizo ya akili au stress za hali ya juu ka huna itakuwa umeishia darasa la pili na hapo ulipo ni secretary wa ofisi fulani umeingia huku ka bahati mbaya jaribu kufikiria ndo utume post unazidi kuudhaliisha huo uislam kwamba uelewa hata wa waumin wake ni mdogo
 
Majini ni viumbe miongoni mwa viumbe wa Allah (SWT) ambao wamepewa majukumu ya kiibada, lakini majukumu yao ya kiibada hayalingani sawa na majukumu ya kiibada waliyopewa wanadamu isipokuwa majukumu yao yanafanana na ile hali yao ya kimaumbile walioumbiwa. Anasema Ibn Taimiyah: "Majini wameamrishwa katika mambo ya kimsingi katika ibada kwa maumbile yao. Kwani wao hawapo sawa sawa na wanadamu katika hukumu za kidini, haiwezekani kuwa waliyoamrishwa na waliyokatazwa yawe sawa sawa na yale waliyoamrishwa na kukatazwa wanadamu. Lakini tu wao wanashirikiana na wanadamu katika ile hali ya kuwa wao pia wamepewa majukumu ya kidini, kama mambo ya halali, haramu n.k. Hili kwa ninavyofahamu halina utata kwa waislam wote." [ Majmuu'atil - Fataawiy 4:233 ]

1. Je kulikuwepo na Majini mitume / manabi ?

Swali hili aliulizwa Adhwihaak ya kwamba, je kuna waliokua mitume au manabii miongoni mwa majini kabla ya Mtume Muhammed (SAW)? Akajibu kwa kusema, "Hivi hamkusikia tamko la Allah (SWT) lisemalo 'Enyi makundi ya majini na wanadamu, Je hawajakufikieni Mitume miongoni mwenu kukubainisheni aya zangu ..' Al - An'am 130." Aya hii kwa alivyoona Adhwihaak inafahamisha ya kwamba Allah (SWT) alipeleka majini wakiwa ni Mitume. Lakini yeye amepingwa kwamba hii aya haikuweka wazi mitume waliyotajwa walikua ni katika jamii ipi mojawapo, majini au watu, kwa sababu neno lake Allah (SWT) "miongoni mwenu" inawezekana kwamba mitume walitumwa katika jamii zote hizo mbili na inawezekana ikawa mitume walikuwepo katika jamii moja lakini kwa wote hao. Katika jambo hili wanazuoni walitofautiana katika makundi mawili wengi wao walikubaliana ya kwamba mitume hawakuwepo katika jamii ya majini kamwe, mitume walikuwepo tu katika jamii ya wanadamu.Ni wanazuoni wachache tu ndio walioonelea kwamba kulikuwepo na mitume waliyopelekwa katika jamii ya majini, na miongoni mwa walioonelea hivyo ni huyu mwanazuoni aitwaye Adhwihaak.

2. Utume Wa Nabii Muhammad (SAW) kwa majini na wanadamu

Wanazuoni wote wa kiislam wamekubaliana kwamba Muhammad (SAW) alitumwa na Allah (SWT) kwa majini na watu wote. Na hivi ndivyo ilivyo kama asemavyo Ibn Taymiyah - kwani Qur-an inashindana na jamii ya majini na pia jamii ya wanadamu. Allah (SWT) anasema: "Sema hata wakijikusanya majini yote na watu wote, ili kuleta mfano wa hii Qur-an, basi hawangaliweza kuleta mfano wake, hata kama watasaidiana wao kwa wao." Al - Israa 88. Na kundi mojawapo la majini lilisilimu mara tu baada ya kusikia Qur-an tukufu: "Sema imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikia Qur-an likasema ( kundi hilo ), 'Hakika sisi tumesikia Qur-an ya ajabu inayoongoza kwenye uongofu, tukaiamini, na kamwe hatutamshirikisha Mola wetu na yeyote yule ....'" A1 - Jinn 1 - 2. Aya zote hizi za Qur-an zinafahamisha wazi kwamba Mtume (SAW) alitumwa kwa majini na watu wote. Ama kuhusu upande wa hadithi za Mtume (SAW) kuna uthibitisho wa wazi katika sahihi mbili Bukhari na Muslim kutokana na hadithi ya Jabir bin Abdallah (RA) kwamba Mtume (SAW) amesema: "Nimepewa mambo matano ambayo hajawahi kupewa Mtume yeyote yule kabla yangu - Mpaka alipofikia: Na kila Mtume alikua akipelekwa kwa kabila lake tu lakini mimi nimetumwa kwa watu wote." Na akasema Jauhariy kwamba makusudio ya watu wote hapa ni kwa majini na wanadamu wote pamoja. Hivyo basi Mtume Muhammad (SAW) alitumwa kwa wanadamu wote pamoja na majini akiwa ni Mjumbe Mwonyaji. Na huu ndio ubora wake uliowazidi mitume wote waliotangulia.

3. Mila na madhehebu ya majini

Allah (SWT) ametufahamisha ndani ya Qur-an aliposema, "Katika sisi wapo ( majini ) wema na kuna miongoni mwetu ( majini ) kinyume na hao tumekua njia mbali mabli." Al - Jinni 11. "Nasi ( majini ) wamo miongoni mwetu waislamu na wamo miongoni mwetu waliokengeuka. Waliosilimu hao ndio waliotafuta uongofu. Na wanaokengeuka hao watakuwa kuni za Jahannam." Al- Jinn 14 - 15 . Hivyo basi Allah (SWT) katufahamisha kwamba majini nao wana mila na itikadi tofauti kama vile wanadamu walivyo, kuna waislam, makafiri na madhehebu mbalimbali.

4. Je majini nao wanalipwa kutokana na vitendo vyao?

Wanazuoni wanatofautiana katika hili. Kuna pande mbili za maoni:

Upande wa kwanza: unaona kuwa majini watalipwa kwa wema watakaoufanya, na wataadhibiwa kwa maasi yao na hayo ni maoni ya Imam Malik, Shafii, Ahmad na Ibn Abbas.

Kundi la pili: linaona kwamba majini hawatakuwa na malipo yeyote isipokuwa kukombolewa na moto wa Jahannamu. Kisha wataambiwa wawe mchanga kama vile itakavyokuwa hali ya wanyama. Na hayo ni maoni ya Imam Abu Hanifa, Laith, Abu Salim na wengineo.

Lakini usahihi ni kwamba majini watalipwa kwa vitendo vyao vizuri au vibaya kwa ushahidi wa Qur-an, Allah (SWT) anasema: "Na wote wana daraja ( malipo ) sawa kwa yale waliyoyatenda. Na Mola wako si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda." Al - An'am 132.

Je kuna ndoa kati ya majini na watu?

Imeenea katika baadhi ya maeneo kwamba kuna mtu ameoa jini; au kwamba mwanamke wa kibinadamu kaolewa na jini au ameposwa, kuna ukweli gani katika jambo hili? Ni kweli kwamba ndoa huenda ikawa kati ya mwanadamu na jini, Allah (SWT) anasema katika Qur-an Tukufu, "Nashirikiana nao katika mali ( zao ) na watoto ( wao )." Al - Israa 64. Akasema Mtume (SAW), "Anapokutana na mume na mkewe pasi na kutamka jina la Allah, basi shetani hushirikiana na huyo mume katika tendo la ndoa." Hadithi hii ameitoa Shubly katika kitabu Ahkamul - Murjaan. Na amepokea Hafidhi bin Jarir kutoka kwa Ibn Abbas (RA) kwamba Mtume (SAW) amesema: "Pindi amwingiliapo mume mkewe wakati akiwa katika hedhi, shetani humtangulia na ( mkewe ) akishika mimba basi atazaa mtoto ( khanithi ). Na ( makhanithi ) ni watoto wa majini." Na kuhusiana na hilo amesisitizia Ibn Taymiyah kwamba: "Inatokea kujamiiana kati ya majini na wanadamu na ikiwa ni hivyo basi huzaliwa watoto mara nyingi ( kwa kujamiiana huko ) kwa inavyofahamika." Wanazuoni wa mambo ya historia wameelezea kuhusu habari zilizotangulia zinazohusiana na ndoa kati ya majini na binadamu tutataja kisa kimojawapo, kisa kilichotolewa na Abu Bakar bin Abid-Dunia, kutokana na Abu Yusuf Saruji kwamba yeye amesema: "Alikuja mwanamke mmoja kwa bwana mmoja huko Madina, akamwambia: 'Hakika sisi tumeshukia hapa jirani je utanioa?' Basi yule bwana akamwoa, kisha baada ya muda yule jinni ( mke ) akamwambia yule bwana, 'umefika wakati wa kuondoka, basi naomba unipe talaka.' Na alikua akimjia usiku katika maumbile ya mwanamke. Ikatokea baada ya kumpa talaka akamwona siku moja katika mtaa mmoja ( jinni ) huyo akiokota nafaka zilizoanguka kutoka kwa wauzaji wa mazao. Akamwuliza ( jinni huyo ), 'Je unazihitaji nafaka hizi?' Yule jini akaweka mkono wake kichwani kuonyesha kuumbuka, kisha akainua uso wake akamtazama yule bwana, akamwuliza, 'umenionaje?' Yule bwana akajibu, 'kwa jicho hili', yule jini akanyoosha kidole chake kwenye lile jicho la yule bwana na kulipofua."

Na pamoja na kwamba kuna visa vingi vilivyopokewa kuhusu kuwepo ndoa kati ya wanadamu na majini, isipokua kuna wanaodai ya kwamba Majini wana asili ya maumbile ya moto, na wanadamu wana asili ya vitu vinne ( Hewa, maji, udongo na joto ), hivyo basi kuwepo kwa asili ya moto katika majini kunazuia kukaa yale ( manii ) ya binadamu katika tumbo la uzazi la jini, kutokana na moto uliopo.

Imepokewa na Ahmad kutoka kwa Ubaid bin Umair kwamba Iblis alisema: "Ee Mola wangu, umenitoa mimi peponi kwa sababu ya Adam, na mimi sitomweza isipokua kwa nguvu za ufalme wako". Allah (SWT) akamwambia: "Basi tutakusalitisha nae. " Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Basi hatopatikana mtoto wa kibinadamu isipokua atazaliwa na mtoto wako vile vile." Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Vifua vyao vitakua ndio sehemu yako na utatembea katika mishipa yao ya damu." Na hiyo ni sawa na kauli ya Allah (SWT) katila Qur-an Tukufu aliposema: "Na uwakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali zao na watoto wao, na waahidi ahadi za uongo. Na shetani hana ahadi isipokua ni udanganyifu." Al - Israa 64.

Akasema Adam: "Ee Mola wangu umenisalitishia Iblisi na mimi sitoweza kujikinga nae isipokua kwako." Allah (SWT) akamwambia: "Kila mtoto atakayezaliwa kwako nitamwekea mlinzi wa kumlinda na mashetani wabaya." Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Jema moja nitalipa mara kumi na zaidi, na baya nitalipa mara moja na ninaweza kulifuta." Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Mlango wa toba sitaufunga kwa mja wangu akiwa bado yupo hai." Akasema: "Ee Mola wangu nizidishie." Akamwambia: "Ninasamehe makosa yote wala sijali." Hapo Adam akasema: "Imetosha." Allah (SWT) anasema: "Enyi waja wangu mliopindukia katika maovu msije mkaiacha rehema ya Allah (SWT). Hakika Allah (SWT) husamehe madhambi yote." Hivi ndivyo alivyo mwanadamu na shetani ambaye ni katika majini.

( a ) Je kujamiiana kati ya majini na wanadamu kuna wajibu wa mtu kuoga janaba?

Aliuliza swali hili Abul-Maaliy wa dhehebu la Hanbali, kwamba kuna mwanamke mmoja alisema: 'kuna jini anayenitokezea kama vile awavyo mume na mke, je? nawajibika kuoga janaba?' Hapo baadhi ya wafuasi wa Imam Hanbal walisema, 'huyo hatooga janaba.' Abu-Maaliy akasema: 'Hata kama huyo mwanamke angesema, 'ameniingilia mimi jinni kama vile mwanaume afanyavyo' pia halazimiki kuoga janaba, hiyo ni kutokana na kukosekana ushahidi wa kuingiliwa na kushusha, hivyo basi hali hiyo ni sawa na kuota ndoto.'

( b ) Nini hukumu ya mke aliyetoweka mumewe kwa kutekwa na jini?

Kisa kama hiki kilitokea wakati wa utawala wa Khalifa wa pili Umar bin Al*khatab (RA). Kuna bwana mmoja alikwenda kusali sala ya Isha akiwa na jamaa zake, akatoweka. Mke wake akenda kwa Umar bin Al*khatab (RA) akamwelezea kuhusu mume wake. Umar (RA) akawauliza jamaa zake kuhusu maelezo ya yule mwanamke, wakasema ni kweli mume wake katoweka. Hivyo Umar (RA) akamwamuru yule mwanamke angojee na kumsubiri mumewe kwa muda wa miaka minne. Yule mwanamke akafanya hivyo. Baada ya miaka minne kupita, akarudi tena kwa Sayyidna Umar (RA) akamwambia kwamba miaka minne imepita na hakuna dalili yeyote ya kuonekana mume wake. Sayyidna Umar (RA) akawauliza jamaa zake. Nao wakamwambia kuwa ni kweli bado hajatokea. Hivyo akampa ruhusa ya kuolewa. Alipoolewa tu, yule mume wake wa kwanza akatokea, ikabidi aende kwa Sayyidna Umar (RA) akamwambia: 'Mtu unatoweka bila ya jamaa zako kuwa na taarifa yeyote kuhusu wewe.' Yule bwana akamwambia nilikuwa nina udhuru, Sayyidna Umar (RA) akamuuliza: 'udhuru gani huo.' Yule bwana akasema, 'siku moja nilipokuwa nakwenda msikitini kusali sala ya Isha nilikumbwa na jinni mwanamke - Nikawekwa kwao muda mrefu. Wakavamiwa na majini waislam. Waliovamiwa wakashindwa vita na wengine kuuawa na wengine wakatekwa, nami nikawa ni katika mateka. Wakaniuliza kuhusu dini yangu. Nikawaambia kwamba mimi ni mwislam. Wakaniambia kwamba wao pia ni waislam, hivyo si halali kwao kunifanya mimi ni mateka. Hivyo wakaniambia nichague kati ya kuondoka kurejea kwetu au kukaa nao, ndipo nilipochagua kurejea kwetu. Wakawa wakinimulikia usiku kwa vijinga vya moto na mchana nikifuata mwelekeo wa upepo kurudi.' Umar (RA) akamuuliza, 'ulikuwa ukila nini?' Akasema: 'kila kilichokua hakitajwi jina la Mwenyezi Mungu ( yaani nyamafu ).' Akamuuliza tena, 'Nini ulikua ukinywa?' Akajibu: 'kila kilichokuwa kama mvinyo.' Hapo Umar (RA) akamwambia kwamba anaweza kumrudia mke wake au achukue mahari yake kutoka kwa yule mkewe.

(c) Ni kipi chakula cha majini?

Kuna tofauti nne kuhusu chakula chao: Kuna wanaosema kwamba majini hawali wala hawanywi, kuna wanaosema kwamba baadhi yao wanakula na kunywa na baadhi nyingine hawanywi wala hawali. Kuna wanaosema kwamba majini wote wanakula na kunywa na hii ndio rai sahihi kulingana na kitabu kitakatifu Qur-an na sunna za Mtume Muhammad (SAW) aliposema, "Shetani atakuwa anakula na mtu, mpaka atakapotaja jina la Allah (SWT), shetani atatapika kile alichokula tumboni." Na katika sehemu nyingine alisema, "Msiende haja kwa kutumia samadi au mifupa kwani hivyo ni vyakula vya ndugu zenu majini." Na katika sehemu nyingine anatukataza kula kwa mkono wa kushoto kwani yeye alisema, "Anapokula mmoja wenu atumie mkono wake wa kulia, na anapokunywa atumie vilevile mkono wake wa kulia, kwani shetani anakula na kunywa kwa kutumia mkono wa kushoto." Huo ni ushahidi wa kutosha wa kuonyesha kwamba majini wanakula na kunywa.

Ni yapi makazi ya Majini?

Majini wanaishi katika mgongo wa ardhi, na wanapatikana kwa wingi katika majangwa na sehemu za takataka, sehemu zenye najisi, chooni na makaburini. Na hii ndio sababu hasa ya wale waganga ambao wana uhusiano na mashetani kupenda kuwashauri wateja wao kupeleka vitu vyao na uchawi wao katika maeneo hayo.

Zipo hadithi za Mtume (SAW) ambazo zinakataza watu kuswali chooni, na hiyo ni kutolana na najisi iliyopo sehemu hiyo, na pia ndiyo makazi ya mashetani. Vile vile majini hupatikana kwa wingi mno katika maeneo yanayokithiri maasi kama vile masokoni. Na hiyo ndiyo sababu Mtume (SAW) akamuusia mmoja wa masahaba wake akamwambia, "Ikiwezekana usiwe ni wa mwanzo kuingia sokoni, wala wa mwisho kutoka, kwa sababu humo sokoni ndipo penye harakati za shetani, na ndipo anaposimika bendera yakc." Imetolewa na Muslim.

Na kama ilivyo vile vile mashetani hukaa katika majumba ya binadamu, na Bismillahi tu ndiyo inayowakimbiza. Amepokea Muslim na Abu Dawood kutoka kwa Jabir kwamba Mtume (SAW) amesema: "Yeyote atakayeingia nyumbani kwake akataja jina la Allah (SWT) wakati anaingia na wakati anapokula shetani husema: ‘Leo hapana malazi hapa wala chakula', na atakapomtaja Allah (SWT) wakati anapoingia nyumbani, na asitaje wakati wa kula, shetani husema, 'Mmewahi chakula lakini hakuna kulala', na mtu asipotaja jina la Allah (SWT) anapoingia nyumbani kwake shetani husema kuwaambia wenzake, ‘mmewahi chakula na malazi'."

Na mahali pengine ambapo shetani hupenda kukaa `ni kati ya jua na kivuli', na hiyo ndio sababu ya Mtume (SAW) kutukataza kukaa katika sehemu hizo, kama ilivyopokewa katika hadithi.

Vipando vya majini?

Mtume (SAW) ameelezea kwamba majini nao wana vipando, na hiyo ni katika hadithi sahihi iliyotolewa na Muslim kutokana na Ibn Mas'ud (RA) kwamba Majini walimwomba Mtume (SAW) awaombee chakula, ndipo Mtume (SAW) akasema: "Mtakula kila mfupa uliotajwa jina la Allah (SWT) ambao utakua ni bora kuliko nyama, na kila samadi itakua ni chakula cha vipando vyenu." Katika hadithi hii kuna dalili ya wazi ya kuonyesha kwamba Majini nao wana vipando.

Elimu na maarifa waliyonayo Majini

Kuna baadhi ya watu ambao wanadai kutibu wagonjwa na kwamba wao wamejifunza tiba hiyo kupitia kwa majini. Na kweli tokea zamani tunasikia kwamba kuna watu wa namna hii wanye uwezo wa kutibu baadhi ya maradhi sugu kama yanavyofahamika. Na miongoni mwa visa vinavyofahamika ni kile kilichosimuliwa na An-nadr bin Amril-Harithiy, aliposema: "Katika zama za ujahiliyah tulikua siku moja karibu na kisima, nikamtuma binti yangu na chombo ili anitekee maji, akakawia, tukamtafuta lakini hatukumwona mpaka tukakata tamaa. Akasema: 'Naapa kwa Allah (SWT) kwamba siku moja nilikua nimekaa mbele ya baraza yangu, akanitokezea Sheikh mmoja, alipoinama kuniangalia mara akawa ni binti yangu. Nikasema: 'Binti yangu.' Akasema: 'Binti yako ndiyo!' Nikasema: 'Ulikua wapi binti yangu?' Yule binti akasema, 'ile siku uliponituma kisimani, alinichukua jinni akawa ananizungusha huku na kule, nikawa nipo kwao mpaka ilipotokea vita kati ya makundi mawili ya majini. Akaahidi kwamba wakishinda vita atanirudisha. Wakashinda ndipo aliponirudisha.' Lakini akawa binti huyo amebadilika rangi yake ya mwili na akawa amekonda sana. Akakaa kwa muda akaanza kubadilika kuwa katika hali ya kawaida, akachumbiwa na mabinamu zake tukamwozesha. Lakini lile jinni likawa limempa ishara ya kumwita kwa moshi pindi panapotokea matatizo yeyote. Basi yule mume wake akawa anamkera na kumwambia wewe ni jini, shetani wala si mtu. Basi yule binti akawasha moshi, yule mume akasikia sauti inamwambia, 'Una nini na huyu ukimsogelea atakutoboa jicho. Nimemchunga tokea wakati wa ujahiliyah kwa maarifa yangu, na katika uislam kwa dini yangu.' Yule mume akamwambia, 'Huwezi ukajitokeza tukakuona?' Yule jinni akajibu, 'Haturuhusiwi. Hakika baba yetu aliomba mambo matatu. Tuone lakini tusionekane, tukae katika tabaka za ardhi, na aishi mmoja wetu mpaka atakapofikia kuwa mtu mzima, kisha atarudi tena kuwa kijana mdogo.' Yule bwana akamwuliza: 'Je unaweza kunipa dawa ya homa?' Lile jinni likajibu: 'Ndio. Unamjua yule mdudu mdogo katika maji, ambaye anafanana na buibui?' Yule bwana akasema, 'Namfahamu.' Basi yule jinni akamwambia, 'Mchukue halafu tengeneza nyuzi kutokana na miguu yake kisha ufunge katika mkono wako wa kushoto.' Yule bwana akafanya hivyo. Akawa kama aliyefunguliwa kamba ya shingo."

Pia Zayd bin Wahab alisema, "Tulipigana vita tukashuka katika kisiwa kimoja, wakawasha moto, pakawa pana chumba kikubwa, akasema mmoja wao, 'mimi naona kuna chumba kikubwa, pengine mnawaudhi waliomo ndani ya chumba hiki.' Wakazima moto wao. Akatokezewa usiku akaambiwa, 'Hakika wewe umeihami nyumba yetu tutakufundisha tiba ambayo itakusaidia, atakapokujia mgonjwa basi chochote utakachomwambia kuwa ni dawa basi atapona.' Ikawa siku moja akajiwa na mtu mwenye tumbo kubwa, alipokua amekaa katika msikiti wa Kufah. Yule mtu akamwomba ampatie dawa ya tumbo lake. Akamwambia, 'Hivi jamani hamshangai kumwona mtu ananiuliza kuhusu dawa naye atakufa leo kwa kula matunda?' Basi siku ile ilipopita watu wakamfuata kumwambia, 'Wewe ni mwongo mbona yule bwana hajafa?' Akawaambia, 'Muulizeni hali ya ugonjwa wake.' Wakasema amekwisha pona.' Akawaambia, 'Mimi nilimtisha asile sana!' Kimetolewa na Abadalla bin Muhammad A-Qurashiy.

( a ) Ipi sababu kuu ya uadui uliopo kati ya shetani na wanadamu?

Uadui kati ya shetani na mwanadamu ulianzia mbali mno tokea pale Allah (SWT) alipomuumba Adam (AS) na kumpulizia roho kisha akawaambia Malaika wamsujudie. Na alikua Iblisi akifanya ibada pamoja na Malaika naye akawa ni miongoni mwa walioamrishwa, lakini yeye alikataa na akafanya kiburi na wala hakusujudu.Wakati Allah (SWT) alipomwuliza sababu ya kukataa kwake kutii amri ya kumsujudia Adam (AS) alijibu kwa kusema: "Mimi ni bora kuliko yeye umeniumba kwa moto na yeye ukamuumba kwa udongo." Na hapa hasa ndio kiini cha uadui uliopo kati ya shetani na binadamu. Na picha nzuri ya historia ya uadui huo ni kama vile ilivyotolewa katika Qur-an Tukufu, Allah (SWT) anatuhadithia: "Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika msujudieni Adamu". Basi wakasujudu isipokua Ibilisi hakuwa miongoni mwa waliosujudu. Allah (SWT) akasema: "Nini kilichokuzuia kumsujudia nilipokuamrisha?" Akasema: "Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo." Akasema Allah (SWT): "Basi shuka huko, haikufai kufanya kiburi humo. Haya toka; hakika wewe ni miongoni mwa wadhalili - duni." Akasema: "Nipe muda ( nisife ) mpaka siku watakapofufuliwa viumbe." Akasema Allah (SWT): "Utakuwa miongoni mwa waliopewa muda, ( lakini si mpaka wakati huo)."Akasema: "Kwa kuwa umenihukumia upotovu basi nitawakalia waja wako katika njia yako iliyonyooka ( ili niwapoteze ), kisha nitawafikia mbele yao na nyuma yao na kulia kwao na kushoto kwao; wengi katika wao hawatakuwa ni wenye kushukuru." Akasema Allah (SWT): "Toka humo hali ya kuwa ni mwenye kudharauliwa na mwenye kufukuzwa. Atakaekufuata miongoni mwao ( nitamtia motoni ) niijaze Jahannamu kwa ninyi wote." Kisha Allah (SWT) akasema kumwambia Nabii Adam (AS): "Na wewe Adam kaa peponi pamoja na mkeo, na kuleni mnavyopenda, lakini msiukaribie mti huu msije mkawa miongoni mwa waliodhulumu nafsi zao." Basi shetani; ( naye ni yule yule Iblisi ) aliwatia wasi wasi ili kuwafichulia aibu zao walizofichiwa, na akasema: "Mola wenu hakukukatazeni mti huu ila msije kuwa Malaika au kuwa miongoni mwa wakao milele ( msife )." Naye akawaapia kwamba: "Kwa yakini mimi ni mmoja wa watoao ushauri mzuri kwenu." Basi akawateka wote wawili kwa kuwahadaa. Na walipoonja mti ule, aibu zao ziliwadhihirikia, na wakaingia kujibandika majani ya ( miti ya huko ) peponi. Na Mola wao akawaita ( akawaambia ): "Je sikukukatazeni mti huu na kukuambieni ya kwamba shetani ni adui aliye wazi?" Wakasema: "Mola wetu! Tumezidhulumu nafsi zetu, na kama hutotusamehe na kutuhurumia, bila shaka tutakua miongoni mwa wenye hasara kubwa." Allah (SWT) akasema: "Shukeni ( katika ardhi ), ninyi kwa ninyi maadui. Na makao yenu yatakuwa katika ardhi na starehe yenu pia." Al - A'raaf 11 – 23. Cha msingi tunachosoma katika aya hizi ni kwamba uadui uliopo kati ya shetani na mwanadamu hautomalizika wala kuondoka kwani yeye shetani anaona kwamba sababu ya yeye kufukuzwa kutoka kwenye neema za Allah (SWT) ni Adam. Hivyo ni lazima ampoteze yeye na kizazi chake na hii ndio sababu hasa ya Qur-an kutuhadharisha mno dhidi ya shetani huyu.

( b ) Ni maasi gani yanayompendeza mno Iblisi?

Anasema Mtume (SAW): "Hakika mamlaka ya Iblisi yapo kwenye bahari, kisha huwatuma majeshi yake, ili wawafitinishe watu. Katika fitna kubwa huja mmoja wao kumwambia, 'Nimefanya hili na lile.' Iblisi anamjibu, 'Hamna kitu.' Kisha anakuja mwingine anasema vilevile, naye humwambia pia, 'Hujafanya lolote.' Kisha anakuja mwingine anamwambia, 'Sikumuacha mtu yule mpaka nimehakiklsha ametengana na mkewe.' Hapo Iblisi humwinamia jinni huyo na kumwambia,'Wewe ndio.'" Imepokewa na Muslim.

source:MAJINI 9
ka ndo mambo wanayofundishwa waumini wa hii dini mbona tabu tupu ka ushirikina vile na watoto wa kiislam kweli wataendelea katika elimu ya kawaida baada ya kujaziwa huu upuuzi kwenye akili. you have long way to go
 
Radio Imaan imefanya uchochezi gani ? Ongea kama Mtu mwenye akili zilizokamilika..........! Onyesha uchochezi huo kwa kuainisha A, B, C na kuendelea ! Sio kutuletea mambo yebu ya kwenye vjiwe vya kahawa................!
Tulia wewe mbwiga! Ongea kwa vituo. Hujui kama radio iman ni ya wale wafuga midevu na wavaa pedo wakishirikiana na kile chama cha wananchi wa upande mmoja wa Tanzania? Sasa we unawaona wale wanapenda amani?
 
Acheni kutafakari ujinga wa wajinga nanyi msije kuwa wajinga kati ya wajinga hao.Sikio lipo kwa ajiri ya kusikia na ndicho chakula chake lakini si kila kiingiacho sikioni chafaa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.Nashauri msiisikilize hii redio kama haina mwelekeo unaofaa kwa jamii.
Mfano mimi sikuisikiliza redio Tanzania kwa sasa TBC taifa kama miaka nane hivi sababu masikio yangu yalikuwa hayapati minofu iliyostahili toka huko,Lakini walipoanzisha vipindi baadhi vya kujenga nilianza kusikiliza vipindi hivyo tu vikiisha nazima au naweka mziki.
Ukisubiri serikali i ban redio hii unaota maana wakubwa hawajaguswa bado wakiguswa watakurupuka huko acha kabisa...
 
kwani ukiristo ni dini? Nipe ushahidi kwenye biblia ambapo yesu anasema nimewaletea dini ya ukiristo. Ushahidi unaonyesha ukiristo ulianza miaka 49 baada ya kuondoka yesu. Au paulo ndio mtume wenu.?... Tunajua hamuwezi kuridhika mpaka tufuate mila zenu. Lakini hamuwezi kuizima nuru ya Allah.

hivi kwa nini kila mtu asisishike na kuamini kitabu chake? Mpaka achukue cha imani ya wenzake? Kwa nini?
 
Kichekesho ni Cd anazotoa Shekh ILUNGA yaani siasa ya dini ya uislam kuchafua uikristo.TUTAFIKA

hapo ndipo panaponikera. Kwanini uchukue vitabu vya imani isiyokuhusu? Yule jamaa aliyeandika Satanic Verses,je? Isingepigwa marufuku kitabu chake ingekuwaje?
 
HAWAJIFUNZI MACHAFUKO YA DINI HUKO NIGERIA? kutukana ukristo hakusaidii kujenga uchumi bali chuki za kidini. sijui ni lini waislamu wataanza kuwapenda wakristo. Hii chuki yao ikeanza tokea Ismail alipotemwa na Ibrahim kuwa mwana mrithi wa kabila lake!!!!!!! mimi huwa siwashangai wanapotukana wakristo.
 
Niliwahi kusikia mtangazaji wa radio Imani ikisema kuwa waislam siyo mafisadi kwa kuwa hakuna muislam aliyefikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi, nadhani walisahau kuwa watuhumiwa wa EPA ni dini mbalimbali.
Huwa nawasikiliza siku moja moja, and I can assure you kuwa pamoja na sala na kaswida jamaa wanatafsiri issue yeyote kwa mtazamo wa ukristo kuwagandamiza waislamu. Nakupa mfano: Waliwahi kusema kuwa ile kampuni iliyorithishwa mkataba wa kina Richmond haina shida ila inapigiwa kelele kwa kuwa mmiliki wake ni muislamu.
Siku hiyo hiyo wakadai kuwa Rostam anasakamwa kwa kuwa ni muislamu (bila kujua jamaa wala si muislamu japo uislamu hata wa jina hana).
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom