Hivi serikali inakabiliwa na ukata au ndio kufilisika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi serikali inakabiliwa na ukata au ndio kufilisika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Sep 8, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,015
  Likes Received: 37,743
  Trophy Points: 280
  Wadau sasa hivi serikalini naona kuna ukata mkubwa tu.Kuna taasisi moja ninayoifahamu ambayo mpaka sasa inaonekana haijapata fungu kutoka hazina tangu bajeti mpya itoke na kama kuna fungu lilitoka basi ni la mwezi mmoja tu.Watumishi wengi hawajalipwa stahiki zao mpaka leo.Mwezi July walipata mshahara ambao ulikuwa haujaongezwa kama ambavyo ilitarajiwa.Mwezi wa 8 walilipa mshahara mpya ila bila malimbikizo ya mwezi wa 7.Na mwezi huu mambo bado hayaeleweki?Madai ni mengi kama hela za likizo,matibabu, n.k.Sasa tatizo ni nini?

  Kuna hii hoja kuwa huenda hela zimetumika kwenye sensa ya watu na makazi.Swali hii sensa ni jambo la dharura?

  Kazi ipo nchi hii.
   
 2. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  hela zimetumika kununua mabomu ya machozi na kuwalipa askari wanaopambana na wanachadema.
   
 3. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Imefulia kwavile haina uwezo wa kukusanya mapato si unajua wanakusanya mapato kutoka kwa wafanyakazi pekee na kuacha migozi yote na wafanyibiashara wakubwa wote waende bila kulipa?
   
 4. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wapo wengine hawajapata hizo nyongeza tangu za mwaka jana.
   
 5. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu bajeti ya nchi yetu huwa ni kwenye makaratasi tu. Mpaka mwaka wa fedha unaisha, halmshauri nyingi zilikuwa zimepata asilimia chini ya arobaini ya pesa toka serikalini. Nafahamu kuna taasisi kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa ikifanya bajeti ya bil tatu kama OC, lakini mwaka iliopata pesa nyingi ilikuwa mwaka juzi, tulipewa mil 900 tu. Hapo ndo tunapokumbuka enzi ya uongozi wa Ben Mkapa.
   
 6. T 2015 CDM

  T 2015 CDM Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali haifilisiki tatizo kubwa sana lililopo ni ile kitu wanaita "Financial fungibility" pesa inapelekwa maeneo ambayo kwenye budget hayapo. Halafu hawakusanyi kodi kikamilifu usaaanii mtupu kila mtu anaangalia apige wapi. Na kumbuka wenzio sasa ivi hawaangalii watufanyie nini ili tutoke hapa tulipo pamoja na ahadi zao zaidi ya 77. Sasa wanawaza nani atakuwa raisi 2015 kutoka CCM na wanafanya mikakati watashindaje. So pisa mingi inafichwa kwa ajili ya 2015. TUBADILIKE TUONDOKANE NA HUU UJINGA WA KUENDESHWA KAMA MAGARI MABOVU.
   
 7. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,015
  Likes Received: 37,743
  Trophy Points: 280
  Hii awmu ya nne ni aibu tupu.Kila kitu kinawashinda hata kukusanya mapato.Bora Mkapa alijitahidi wao kazi yao kukopa wafanyakazi.Maofisi hayana mafungu mpaka leo alafu wanahubiri maendeleo.

  This is nonsense.
   
Loading...