Hivi serikali imewakilishwa na nani kwenye msiba, imesusa?

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Ndugu wana jamvi nimejitahidi kutega sikio nisikie angalau salamu za rambirambi kutoka serikalini lakini hadi msiba unakwisha sikusikia chochote, ina maana serikali imesusia raia wake?

Ninavyofahamu mimi waliokufa ni watanzania regardless wanatoka chama gani, ingependeza sana na serikali ingeonekana ungwana kama ingewakilishwa na kiongozi yeyote msibani na kujitambulisha rasmi hata kutoa mkono wa pole.

Naomba kama kuna mwana JF aliyekuwepo kwenye msiba au hata kasikia ni kiongozi fulani anisaidie. Tuelewe kwamba sisi sote ni watanzania tunajenga nchi moja mazuri na mabaya yakitokea ni yetu sote. Siku Tanzania ikibarikiwa neema tutakaofaidi ni watanzania na si Chadema, CCM wala CUF pekee.

Nitasikitika sana endapo serikali yangu itakuwa haijawakilishwa.

Naomba kutoa hoja.
 
kwa serikali hii anza tu kusikitika mapema
 
Kutokuwepo kwa mwakilishi kutoka Serilakini kunaonyesha wazi kwamba ... Serikali hii ya Rais Kikwete...haiwajali wananchi wake.
 
Ndio mnajua leo, kodi yetu wenyewe ndio inaenda kununua migwanda kama ya kwenda mwezini ilihali mahospitalini hakuna madawa, hivi nikiwaita hawa watu laanabuk nitakua ninakosea jamani?
 
Luteni,

Leo ni siku ya Mapinduzi Zanzibar, hivyo viongozi wote wako Zanzibar uwanja wa Amaan kuonyesha mshikamano. Mazishi yangefanyika siku ingine yeyote, labda majukumu ya kwenda kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi yasingekuwepo.
 
'waache wafu wazikane' -------jesus christ

acha kumsingizia yesu wewe. hajawahi kamwe kutamka maneno uloandika. Kama unabisha tupe katabu, sura na mstari unaoonesha yesu alitamka huu uwongo wako.
 
Luteni,

Leo ni siku ya Mapinduzi Zanzibar, hivyo viongozi wote wako Zanzibar uwanja wa Amaan kuonyesha mshikamano. Mazishi yangefanyika siku ingine yeyote, labda majukumu ya kwenda kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi yasingekuwepo.
Rev.Kishoka

Nakubaliana na wewe kuwa leo ni siku ya Mapinduzi Zanzibar lakini kwani viongozi wote walikuwa huko, kama kweli nia ilikuwepo RC au DC wa mkoa wowote angeweza kuwakilisha kama wa Arusha asingeweza.
 
Hii serikali imepooza dhamiri. Haina feelings na wananchi wake, wala objectivity kifikra. Hawezekani wananchi wafanyiwe maziko rasmi asiwepo hata kiongozi mmoja. Huko ni kusema msiba huu hauwahusu, hauwagusi, wanaguswa zaidi na jengo lao lililopigwa mawe. Wako interested na ulaji tu si wananchi. Si mnajua sasa hivi Tanzania kuna WANANCHI NA WALANCHI? sasa unategemea walanchi wachague kuhudhuria wapi kati ya mazishi yasiyo wapa sitting allowance na vikao vyao? (mapinduzi)
 
Rev.Kishoka

Nakubaliana na wewe kuwa leo ni siku ya Mapinduzi Zanzibar lakini kwani viongozi wote walikuwa huko, kama kweli nia ilikuwepo RC au DC wa mkoa wowote angeweza kuwakilisha kama wa Arusha asingeweza.

Mkuu,
Kama wamesusia, nafikiri ni kwa sababu mazishi yamepangwa kufanywa kisiasa zaidi na wao wanajua katika hali ya kawaida watu wa serikali wanatizamwa kwa jicho baya na jamii kwa yaliyotokea.

pengine ni "busara" kwao kuepuka kizazaa kama wao wangejitokeza.
hapa sina maana ya kuwatetea lakini pia kwa nini waje kwenye msiba ambao wao ndio chanzo? Waombolezaji wangeingiwa na uchungu zaidi kuwaona hao wa serikali katika mazishi ya wapendwa wao.
 
Kuna aina nyingi za kuiwakilisha serikali wangeweza kutuma hata barua ya salamu za rambirambi ikasomwa na kiongozi yeyote wa dini.
 
Wao wanaona kuja kwenye msiba NI MGOGORO WA KIMASLAHI kwani kuja ni kukana kwamba hawajaua. Ina maana kutokuja wamewahakikishia kwamba sisi serikali hatujutii tuliyoyafanya na Polisi kutokuwepo ni ili kuonyesha jinsi ambapo pasipo wao shughuli hiyo ingesababisha uvunjifu wa amani. Yaani Polisi na serikali wamekaa pembeni kuwa proof wrong kwamba bila wao mambo hayaendi teh teh!!!. shame upon them wameshindwa kwa jina la Bw....a

Wamemtega swala ndani ya bahari walivyo na akili za Mary Chatanda

Ni peoples power tu hapa hakuna makunyanzi
 
Nilikuwepo mwanzo mwisho, sijamwona wala kumsikia kiongozi yeyote wa serikali. Dhamira inawasuta. Lakini ilikuwa ni aibu sana kutokuhudhulia msiba wa Watanzania wenzetu kama serikali.
 
Back
Top Bottom