Hivi Sekretarieti ya Ajira Ipo salama?

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,781
2,301
Miongoni mwa mambo aliyoacha Kikwete na yaliyojenga heshima ni Sekretarieti ya Ajira. Wengi waliamini kuwa chombo kile kilikuwa huru kiasi fulani na vimemo havikutembea kwenye kazi hizi za kawaida.

Tokea serikali ilivyositisha ajira, chombo hiki kimekuwa kikitangaza nafasi za Watendaji Wakuu peke yake kama RITA na Shirika la Posta. Hata hivyo, kiuhalisia ajira zimeanza kujitokeza lakini kwa mlango tofauti.

Mfano, Workers Compensation Funds, Mamlaka za Maji za Mikoa nk hawa wote wametangaza ajira kwa milango yao. Ikumbukwe kuwa baadhi ya taasisi hizi zilikuwa zikipitia Sekretarieti ya Ajira.

Swali la kujiuliza, Sekretarieti ya Ajira inafifishwa taratibu au itabaki na shughuli gani? Je, mtoto yule wa mkulima ambaye alikuwa anapata nafuu wa kupata kazi za kawaida kwa usaili wa maelfu, atasalimika?

Au mfumo huo ni mbovu na bora turejee tulipotoka?
 
Turejee tulikotoka, ilikuwa ni usumbufu sana mtu anatoka Mwanza kwenda kufanya interview Dsm kwa siku 3. Gharama kubwa sana
 
Back
Top Bottom