Hivi Seif Kaongea Huko Pemba ??? Mbona Hatujasikia Kweye Radio au TV Speach yake??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Seif Kaongea Huko Pemba ??? Mbona Hatujasikia Kweye Radio au TV Speach yake???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KING COBRA, Dec 17, 2011.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Wakuu leo Seif alisema atatoboa Siri juu ya Bifu lake na Hamad Rashid kwa Kuongea na Media saa tatu asubuhi Ikulu ZNZ sasa nimefutilia sana TV na Radio sijasikia lolote , je ameogopa baada ya Hamadi rashid Kusema ataanzisha Chama???
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Maalim Seif kunena leo Ikulu Zanzibar

  KIONGOZI mashuhuri wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, amesema ataunda chama kipya na kikubwa cha siasa ikiwa atafukuzwa uanachama kwa kufuata taratibu na kanuni za Chama cha CUF.

  Hamad alisema chama atakachounda mara baada ya kutoka CUF kitasheheni viongozi wengine walioko ndani ya chama hicho ambao hawakubaliani na uongozi wa sasa ambao umekifanya chama hicho kilichokuwa na nguvu kubwa kuwa dhaifu.

  Hamad alibainisha hayo jana alipozungumza kwenye kipindi cha ‘Pambazuka' kinachorushwa hewani na kituo cha televesheni cha Channel 10 na kuongeza kuwa haogopi kufukuzwa ndani ya CUF kama alivyotishiwa na baadhi ya viongozi wenzake wanaopingana, lakini akaonya kuwa hatua hizo zifuate kanuni na taratibu za chama.

  Mbunge huyo wa Jimbo la Wawi alisema ikiwa viongozi hao watakiuka kanuni za chama za kumfukuza atawafikisha mahakamani kupinga kufukuzwa kwake, lakini iwapo ataridhika na taratibu zitakazotumika atashawishika kuunda chama kingine akishirikiana na viongozi wenzake."Wakinifukuza sina mpango wa kuhamia chama chochote cha siasa, kwani mimi si malaya wa kisiasa. Nitawashawishi wenzangu tuanzishe chama chetu," alisema.

  Pamoja na hayo, alisema hata wakimfukuza chama hicho kitaendelea kuwa dhaifu kwa kuwa hivi sasa viongozi hawakiendeshi chama kama taasisi."Nimefanya juhudi kubwa za kuimarisha chama Tanzania Bara, lakini pia kwa mujibu wa katiba kila mwanachama anapaswa kuimarisha chama katika eneo analoishi na mimi naishi Kinondoni, hivyo nilikuwa sahihi kuitisha mkutano ule, lakini cha kushangaza wakawaleta Blue Guards na kuwapiganisha na wanachama," alisema.

  Akizungumzia chanzo cha mzozo huo, Hamad alisema unatokana na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi ya ukatibu mkuu na baadhi ya wanachama kuhoji masuala ya msingi ndani ya chama ambao anadaiwa kuwapandikiza."Katika mkutano halali wa Baraza Kuu, Rakesh, Doyo Hassan na Yassin Mrotwa walihoji matumizi ya fedha za chama sh milioni 500 zipo wapi. Wakadai eti nimewapandikiza," alisema.

  Alisema alihoji matumizi ya sh milioni 307 katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, lakini mpaka sasa hajapatiwa majibu jinsi fedha hizo zilivyotumika."Watu wanapohoji matumizi hayo, wanaambiwa ni kundi langu, lakini katika uchaguzi huo, Mtatiro anasema walitumia sh milioni 49 kukodi ndege mara tatu. Atuambie chenji yetu iko wapi?"Wanatumia rasilimali za chama kuchafua jina langu bila kunishirikisha.

  Hivi kutangaza nia ya kuwania nafasi ya ukatibu mkuu imekuwa nongwa? Mbona Maalim Seif ametangaza nia hiyo katika mkutano wa baraza kuu?" alihoji.Alisema kuwa baadhi ya viongozi wanamtuhumu kuhongwa sh milioni 700 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kugombea urais kwa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao na yeye awe mgombea mwenza na pia wanamtuhumu kukipa nguvu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)."Madai yote haya yanayoelekezwa kwangu hayana ushahidi wowote.

  Mtatiro ananiita muasi, amepata wapi mamlaka hiyo? Ina maana ameshanihukumu bila ya kunisikiliza? Mbona hatuendi na kaulimbiu ya chama ‘Haki sawa kwa wote?' "Mimi sina ukorofi, lakini wao wanatumia vikao kunichafua, sipewi nafasi nikizungumza kwenye vyombo vya habari naonekana mkorofi, sasa wanataka nifanyeje?" aliuliza mbunge huyo.Alionesha kushangazwa kwake na kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ambayo alisema ndani ya CUF haipo, labda kama imeundwa hivi karibuni.

  Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad leo anakutana na waandishi wa habari Ikulu, Zanzibar. Hata hivyo haijajulikana nini atakiongea, ingawa kuna madai kuwa atazungumzia sakata hilo la mgogoro baina yake na Hamad Rashid.Katika siku za hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya mbunge huyo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, uliosababisha kuzuka kwa mapigano makali na watu kadhaa kujeruhiwa baina ya wanachama wanaowaunga mkono.::Tanzania Daima::
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Seif na Chama chake kaamua kuwauza wapemba gharama za posho na kingora hakika ulaji mzito yuko kama Nape
   
 4. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Seif kasema hawezi kujibishana Hamad Rashid kwenye vyombo vya habari, anasubiri vikao vya chama
   
Loading...