Hivi sasa ajira ni za kujuana, Connections na "kamleteni"

MMOJA

JF-Expert Member
Aug 30, 2012
445
259
Habari JF,

Poleni vijana wenzangu na majukumu ya kila siku

Nimeleta tujadili uzi huu kila mtu kutokana na jinsi anavyojua kwenye sala kupata kazi

Nimeona baadhi ya makampuni mengi, hata kampuni niliyoajiriwa binafsi ikitokea kuna uhitaji wa kumuajiri mtu, kwanza inatangazwa mule kwa wafanyakazi wa ndani na Board of Directors kuwa kuna vacant ya nafasi Xx

Hivyo basi kama kuna mtu anaweza akafahamu wa kujaza nafasi hiyo atuletee cv yake

Kinachotokea hapo zile cv zinazowasilishwa na wafanyakazi na Board of Directors ndio zinapewa uzito wa hali ya juu, na ikiwa zimewasilishwa nyingi Basi hawatoki hata nje kutangaza hizo nafasi

Kwa makampuni mengine hauoni nafasi kutangazwa ila unaona tu tayari mtu amesha ajiriwa, hii mchakato wake unakua ni ule ule wa kujuana

Haya Basi kuna wafanyakazi huwa wanaitwa "Kamleteni" wafanyakazi Hawa ni wale ambao wana connection ya karibu na aliye recommend aajiriwe hapo ambaye huyo aliye recommend au referee wake ana mahusiano ya karibu sana na kampuni hiyo

Hawa "Kamleteni" huwa wanapata promotion kwa haraka sana ijapojuwa mnaweza mkalingana nae au kumzidi kwenye annual evaluation hata kwenye salary increment "Kamleteni" huwa wanapata percent kubwa ya salary increment tofauti na wa kawaida

Nini Kifanyike Ikiwa huna Connection au huna wa kukuunganisha na Kamleteni

1. Pitisha Sana Cv zako kwa hawa recruitment agencies maana wao kama una sifa stahili, wana kuunganisha na wateja wao

2. Pitia pia Utumishi

3. Tengeneza connections na meneja, HR na waajiri

Labda mungu asaidie na afanye wepesi unaweza pata kazi ila bila hivyo utajikuta unaomba kazi hata mara mia mbili na wala usiitwe hata kwenye interview

Karibuni kwa maoni wadau


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali ya ajira kwa sasa ni mbaya mno, haijawahi tokea tangu tumtoe mkoloni. Ila imewezekana kupitia awmu ya mzee baba hili nalo ni la kupongeza serekale ya awamu ya faivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hali ya ajira inazidi kuwa ngumu kadri siku zinavyozidi kwenda,
Maana kila mwaka vyuo vinatema na wasomi wanamwagika mtaani ila nafasi zinazozalishwa ni chache sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom