Hivi samaki huwa wanashushwa kama mvua?

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,482
14,347
wanajamvi naomba tujadiliane hili jambo, kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza: hivi inakuaje sehemu ambapo maji ya mvua hutulia na baada ya muda hukauka kabisa na sehemu ile huwa kavu kabisa mpaka huwa panakua na mipasuko lakini baadaye mvua ikianza kunyesha mahali pale Samaki huwa wanatokea tena wakubwa kama Kambale na perege mpaka wakati mwingine raia huwa wanavua na kupata kitoweo..
maswali yangu...
1. hivi inakuaje sehemu ambayo ni kavu baada ya mvua kunyesha samaki huanza kutokea?
2. inawezekana hawa samaki huwa washuka wakati mvua inaponyesha?
3. au kuna mbegu ambazo huwa zinashushwa kutoka juu ambazo zikitua ardhini hurutubishwa halafu samaki hutokea?
vilevile: sio samaki hata vyura pia huwa wanatokea baada ya mvua kunyesha na maji kujaa kwenye madimbwi nao hutokea wapi?
naomba kujuzwa naamini kuna wataalamu waliobobea katika haya mambo.
 
Kambale ni samaki mwenye uwezo wa kujichimbia chini kwa muda mrefu (miezi kadhaa bila kufa) kusubiri mvua kunyesha tena, akiwa huko chini hula tope....na pale anapokuwa sijui anafanyaje panakuwa na tope muda wote...mvua ikinyesha ile mipasuko ya udongo huingiza maji hadi chini na kambale hutoka na kuja tena juu,...na maisha huendelea....
 
Kambale, Mumi, baadhi ya samaki wengine kama Nembe, hawa wanapatika sehemu za mito pamoja Vyura!
Hawa wana tabia ya kutaga mayai yao chini ya ardhi na wakati wa ukame wanapoona Maji yanapungua na ardhi inaanza kuwa ngumu!
Hapo uingia chini ya tope na kukaa huko kwa muda mrefu, kwa jinsi walivyoumbwa wana uwezo wa kukaa chini ya tope huku wamefunikwa na ardhi zaidi ya miezi mitatu.
Mvua au maji yanaotaletwa na mafuriko yakifika sehemu
hiyo ardhi inakuwa tepe tepe na samaki wanatoka nje kwa wingi pamoja na vyura!
 
thanx mkuu kwa maelezo yako, hapo kwenye blue inakuaje hayo mayai huwa hayaharibiki? wakati panapokua na ukame wa zaidi ya miezi sita huwa inakuwaje? maana ninavyojua mayai ya samaki huwa kama ute fulani
 
Back
Top Bottom