Hivi salamu ya' Heshima yako'?! maana yake nini?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,362
Wakuu habari!
kichwa cha habari kinajieleza.
Nilikua naangalia sherehe ya kuagwa Dr.Kimei wa CRDB,sasa alipohojiwa Mwenyekiti wa Bodi akasalimiwa heshima yako nae akajibu 'heshima yangu ni nzuri'

Nimejiuliza hii salamu maana yake nini hasa,wanasalimiwa rika gani na inajibiwa vp?
N:B nimeambatanisha video wenye mb wanaweza kuona sekunde 5 za mwanzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salamu hiyo aghalabu hutolewa kwa mtu ambaye huna hakika na umri wake kama anakuzidi au la! Unamwambia heshima yako ili yeye aitikie kadiri anavyojiona akijilinganisha na wewe anavyokuona
 
Kama ni hivyo basi inatumiwa vibaya maana hata ukiangalia kwenye hio video huyo mtangazaji anamhoji mtu wa umri wa baba yake kabisa na ambao hawezi kua na shaka nao lakini bado kamsalimu 'heshima yako'
 
Ni miiko ya journalism, hata kama unamhoji rais huwezi kumsalimia shikamoo, labda kama ni off record lakini ukiwa hewani ni heshima yako tu, hata kama angekuwa na miaka 100. Fuatilia umewahi kusikia wapi mtangazaji anamsalimia anayemhoji kwa shikamoo.
 
OK sikuwahi kujua hilo lakini kwanini 'heshima yako' na sio habari za asubuhi,mchana au jioni nk?
 
Napenda kuitumia hii salamu nikidhani ni heshima, tena kwa wakubwa ila wengi huwa wanaitikia ‘marhaba’ tu.... mi nikianzishiwa hivyo huwa nahisi sio sawa kujibu marhaba.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom