Hivi Salakana wa CCM na Sungura wa NCCR wana Matatizo ya akili au?

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,765
2,000
Wana JF mimi ni mtanzania mwenye nia njema na nchi hii, nimeanza harakati za kupigania maslahi ya nchi hii tangu 1995 nikiwa darasa la tano.

Kwa uelewa wangu wananchi wa moshi mjini wana haki ya kumchagua mbunge wao wanaompenda kama ilivyo kwa maeneo mengine hapa nchini. Nashangaa sana kuona kauli za hawa jamaa walioshindwa ubunge wa moshi mjini hadi nafikia hatua ya kuhoji kama kweli wanatumia akili walizonazo au hawana kabisa akili tujue moja.

Kwanza nianze na huyu anayejiita Sungura wa NCCR, haingii akilini kuona mtu mwenye akili timamu karne hii ya 21 anachukua fomu ya kugombea ubunge na kupitishwa na chama chake kugombea na yeye kuamua kuingia mitini bila kufanya mkutano wa kampeni hata mmoja halafu baada ya uchaguzi kuisha na mshindi kutangazwa na kuapishwa anakimbilia mahakamani eti yeye ndio alistahili kutangazwa mshindi, hii inawezekana wapi? Hivi hata kama hao majaji wanalipwa kwa kodi za waTZ kwa nini wapoteze muda kwenye kesi kama hizi, na amepata wapi hizo 5M za kufungulia kesi? Mimi naanza kuwa na wasi wasi na hawa jamaa kama hakupiga kampeni na amepata kura 42 ashukuru sana maana tunaposema chadema isiungane na NCCR ndio sababu wananchi wengi wanaunga mkono hii hoja.
Mimi ningekuwa wale wananchi 42 waliompigia kura tunafungua kesi dhidi ya huyu Sungurakwa kukihujumu chama kwa kuzuia watu wengine baada ya kupita yeye kaamua kuacha kupiga kampeni hiyo ni dalili ya kupewa na kupokea rushwa.

Pili kwa huyu jamaa, wa CCM anayeitwa Salakana kwanza kabisa huyu jamaa ametoa rushwa nyingi wakati wa kampeni na wananchi wakaamua kumtosa kutokana na tabia yake hiyo, na akaambulia kura kama 16,972 ambazo nyingi ni za uchakachuaji bado anadanganyika na kauli za makamba eti "Mgombea yeyote wa CCM aliyeshindwa na mgombea wa chadema afungue kesi kwa sababu wabunge wa chadema hawamtambui rais " kumbe ni wananchi wengi hawaitaki CCM sasa utawalazimisha wananchi waichague CCM, Naye huyu jamaa nina wasi wasi na uwezo wake wa akili.
Watu hawakutaki waachie kwani lazima yeye na CCM wawe viongozi wa wananchi. Ona madai anayotoa ni ya kitoto sana eti padri alisema mtichague waliotoa rushwa wakati wa kampeni, hii si iko wazi hata JK mwenyekiti wa CCM mbona alikuwa anasema au haelema maana ya kutoa au kupokea rushwa, asifikiri waTZ ni wajinga kama anavyofikiri.

Tuendelee kuwaunga mkono wananchi wa Moshi na sehemu zingine, waliochagua mabadiliko na wanaipenda TZ na watu wake.

Peoples Power!!!!!!!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom