Hivi Russia anasubiri nini kuivamia Ukraine, Kwanini amebaki mpakani tu?

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
Nimeona nije na hili wadau wenzangu, dunia inaelewa malengo na mahitaji ya Russia kwa nchi ya Ukraine yapo wazi sana swali ni kwanini amebaki mpakani???

Sasa takriban mwezi., NATO wamekuwa wa wazi sana na hawapepesi kauli zao ni kwamba wanasubiri Russia waivamie Ukraine ndio na wao lile lengo lao litatimia kwa nilivyofahamu mimi.

Lakini kuna maswali najiuliza hasa kwa Russia., Ivi baada ya Marekani na NATO kuwahi kuingia Ukraine ki-ulinzi na kuwa tayari kujibu mara Urusi ikivamia Ukraine Na hata jana Biden amesema watajibu thabiti kama Russia akijaribu kuvamia tu- Ivi Russia ndio imekuwa na hofu kubwa kukamilisha adhma yake?

Tuseme ni sahihi kusema Russia analiogopa Jeshi la NATO lakini na Marekani licha ya majivuno mbali mbali ya Putini? mara nyingi nikiangalia Televisheni CNN naona bado Russia wanailalamikia Marekani kutokuwa tayari kwa mazungumzo,

Na Kremlin mara kadhaa namsikia akisema hawana nia ya kuvamia Ukraine ivi ni kwanini hasa kauli hizi? Kuna nini nyuma ya Pazia la Russia?

Kama hawana nia ya kuvamia wao wanafanya nini mpakani mwa Ukraine? au Tuseme wanalinda mpaka wao tu.

Earlier Russia walisema ni vita vita vita tu lakini kwa nini wamebaki mpakani wansubiri nini?

Nafkiri wadau hemu tujikiteni hapa kidogo tupate dondoo zenu katika hili
 
Mbona kama Russia yuko ndani ya Ukraine akivisaidia vikosi vya waasi katika majimbo ya Donbas na Luhansik tangu 2014?

Kwa sasa anatafakari majibu ya US na NATO kwa maombi yake ya kutaka Ukrane isijiunge na NATO na kuhakikishiwa usalama wake! US na NATO wameyakataa maombi yake! Hapo ndipo dunia inasubiri Putin atafanyaje.
 
Tusubiri muda ndio utaamua kama zipigwe ama. Kwa sasa nadhani pande zote mbili zimetoa fursa ya majadiliano ya kidiplomasia kwanza.
 
Mkuu,Hio yenyewe ni VITA.

Kama majeshi yao yako mpakani hio ni VITA na kama NATO wako UKRAINE hi ni VITA.Swala la kushinda au kushindwa ni swala mkakati zaidi kwani katika Vita kuna mambo mengi zaidi ya kufyatua RISASI.

Kwa ufupi RUSSIA ameshashinda hii VITA kipropaganda na kimkakati na kinachofanyika hapo ni Military Diplomacy vs Military Propaganda ila kile walichotaka kutoka UKRAINE tayari wanakipata.
 
Hii sio kama Crimea
Nam admire sana Putin ila kwenye ukweli tuseme
Russia hawatavamia kwa sababu nyingi tu
Uchumi pande zote utaporomoka ila kwa Mrusi utakuwa zaidi maana sanctions watakazomuwekea ni hatari na kesho jumatatu ndio watasema waya Fanta nini
Huku Boris ametoa Amri kwa Jeshi waweke full force na kuipa nguvu NATO

Kuwekewa vikwazo tunajua wamemfanyia sana Putin ila ni mbaya sana kwao
Tusubiri tuone
 
Back
Top Bottom