Hivi rushwa ya Mil 90 inaweza kuwapa ushindi Kalenga?

Recipient

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
425
345
Wakuu,

Ukweli ni kwamba hali ya siasa ya nchi yetu ni ya kusikitisha kama si kustaajabisha kwa chama cha siasa ambacho kimekosa hoja zinazoweza kuwashawishi wapiga kura wakakiamini. Imefikia mahali hawana kete nyingine ya kuicheza ili kupata ushindi kwenye sanduku la kura zaidi ya kuwaza kuhonga wapiga kura.

Hivi tunavyozungumza ni kwamba yule mkuu wa Green Guards Tanzania na China mchana huu ame draw fedha taslim na halali za kitanzania Mil 90 na kwenda nazo na gari lake Kalenga. Tunajiuliza Kalenga kuna uchaguzi, na imebaki masaa takriban chini ya 40 kwenda kupiga kura sasa hizo hela ni za kwenda kufanyia nini? Akili kichwani.

Hii hapa chini ni taarifa za kiintelijensia kutoka kwa Mtanganyika mwenzetu aliyeko kwenye viwanja vya ukombozi Kalenga;

Barabara ya Dodoma au Uhuru Avenue, Benki ya NMB Tawi la Iringa

Yule mpangaji mipango mmuaji na gaidi wa CCM, majira ya saa 6 mchana leo, ame-draw milioni 90... Je mnataka kujua ni za kazi gani? Wakati mnajua kuna uchaguzi Kalenga na wamezidiwa!
 
Hatari sana kwakweli.... Hizo hela angeenda kununulia madawati watoto wakaacha kukaa chini angebarikiwa sana
 
Wakuu,

Ukweli ni kwamba hali ya siasa ya nchi yetu ni ya kusikitisha kama si kustaajabisha kwa chama cha siasa ambacho kimekosa hoja zinazoweza kuwashawishi wapiga kura wakakiamini. Imefikia mahali hawana kete nyingine ya kuicheza ili kupata ushindi kwenye sanduku la kura zaidi ya kuwaza kuhonga wapiga kura.

Hivi tunavyozungumza ni kwamba yule mkuu wa Green Guards Tanzania na China mchana huu ame draw fedha taslim na halali za kitanzania Mil 90 na kwenda nazo na gari lake Kalenga. Tunajiuliza Kalenga kuna uchaguzi, na imebaki masaa takriban chini ya 40 kwenda kupiga kura sasa hizo hela ni za kwenda kufanyia nini? Akili kichwani.

Hii hapa chini ni taarifa za kiintelijensia kutoka kwa Mtanganyika mwenzetu aliyeko kwenye viwanja vya ukombozi Kalenga;

Barabara ya Dodoma au Uhuru Avenue, Benki ya NMB Tawi la Iringa

Yule mpangaji mipango mmuaji na gaidi wa CCM, majira ya saa 6 mchana leo, ame-draw milioni 90... Je mnataka kujua ni za kazi gani? Wakati mnajua kuna uchaguzi Kalenga na wamezidiwa!

Mwigulu unajidai mzalendo huku unaipindisha haki??
 
Wana WA kalenga msife moyo Bado bwana yupo upande wetu msivunjike moyo
 
kwa nchi maskini kama inavyojulikana leo hii wanatoa million 90 ili kununua shahada na kuwaonga watu wawapigie kura jamani hizi pesa si zingeenda kwa watoto yatima na wajane duuh ccm mtakufa kifo kibaya
 
Kweli wana pesa ila hakika hawana Mungu

Wanatakiwa kujiuliza kama kweli ccm wanadhani watanzania wa kununuliwa, bali wanahitaji maendeleo. Ni ajabu kuwanunua wapiga kura wakati wao wanahitaji maendeleo siyo pesa yako.
 
Huyo ni mhasibu wa chama na ni waziri kwenye wizara ya Hela,sasa unatarajia nini?
Sehemu ya hizo hela kesho anaingiza kwenye akaunti yake binafsi,na kiasi kuhongea wapiga kura.
Kila mshika mkoba lazima akate kidogo.Maana wengi wananeemeka vipindi hivi vya uchaguzi
 
kwa nchi maskini kama inavyojulikana leo hii wanatoa million 90 ili kununua shahada na kuwaonga watu wawapigie kura jamani hizi pesa si zingeenda kwa watoto yatima na wajane duuh ccm mtakufa kifo kibaya

Chakushangaza ni kwamba wanamajimbo mengi nchi hii, sasa kwanini wanataka kuipata kalenga kwa njia isiyo halali? Wana dhambi gani mpaka wanahisi watapoteza hilo jimbo? Wao wanajigamba kuwa ccm ni nambari one na inakubalika kila mahali, sasa kwanini watumie rushwa? Watulie, waache kuwachanganya wananchi masikini wa kalenga, wawaache waamue kwa mapenzi yao
 
Hela hazisaidii kitu kwa siasa za zama hizi,hizi ni mbinu za zamani za akina kingunge.

Angalizo..
Kuweni macho na Mwigulu huko kalenga
Ni mtu hatari.
 
Hivi Jamani huyu mtu si kafiwa na kaka yake hata wiki haijaisha?

Badala ya kukaa na ndugu msibani anahangaika kugawa hela Kalenga?

Ama tujiulize:Kafurahia kifo cha kaka yake ??
 
Huyo ni mhasibu wa chama na ni waziri kwenye wizara ya Hela,sasa unatarajia nini?
Sehemu ya hizo hela kesho anaingiza kwenye akaunti yake binafsi,na kiasi kuhongea wapiga kura.
Kila mshika mkoba lazima akate kidogo.Maana wengi wananeemeka vipindi hivi vya uchaguzi

Aisee wana dhambi sana hawa watu, wanafunzi hawana vitabu mashuleni, wagonjwa hawana vitanda mahospitalini, kuna watu mlo mmoja kwa siku ni tabu kuupata.... Kwanini wanawaza kuhonga tu mda wote? Mimi naamini kama watafanya mazuri kwa watanzania wala hawatahitaji kuhonga kwa chochote manake siku zote chema huwa kinajiuza chenyewe... Waache dhambi na kujitengenezea laana wao na vizazi vyao
 
Hela hazisaidii kitu kwa siasa za zama hizi,hizi ni mbinu za zamani za akina kingunge.

Angalizo..
Kuweni macho na Mwigulu huko kalenga
Ni mtu hatari.

Tena wawe macho haswaaaa kwa siku kama ya kesho ya kuhitimisha kampeni... Mungu aepushe hila zote za huyu mtu, arusha bado tunamkumbuka na tutamkumbuka daima
 
Ni matusi kuhisi wanakalenga wananunulika kwa pesa na hizo dharau ndizo zinawagharimu Chadema
 
Back
Top Bottom