Hivi Robert Kisena ni nani?

Hawa mafisadi walitesa mno kwa wizi acha wanyooshwe hafu walijifanya miungu watu hawagusiki kabisa
Acha kabisaa wanasema ukimcheki Ruge na Singasinga walivyonyooka+ zile ndevu+kanzu zao unaweza kudhani ni wale manabii wa enzi za yesu.

Ninachokiona UDA inarudi serikalini kwa 100% kama ambavyo yule Zakaria wa Mwz aliwekwa ndani na mkewe mpk akarudisha yale Maghorofa+mali nyingine za chama cha ushirika Mwz.

Hii ni good Move.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja mkuu.

Kuna kipindi jamaa alisema ameleta ma bus 400 ila yamezuiliwa na TRA pale bandarini,sijui alimalizana nao vipi.
Mwendokasi ziko chache usimamizi mubovu nilifanikiwa kupanda Mara chache ila ule usafiri ni kero nawahurumia watumiaji wake bora daladala. Sasa nikiona ni hujuma za kifisadi acha tu anyooshwe aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kuna maeneo kule Vietnam wamezidi kwa kupiga dili.
Tangu awamu ya kwanza wanaongoza kwa kutoa mawaziri na wanasheria wengi na wafalme wawili sasa.
Hawafanyi biashara za maduka au umachinga Bali ni dili za serikali.
Wameua vyama vingi sana vya ushirika.
Kuna awamu waligawana vyeo vikubwa vya kila wizara mpaka Hazina.
Wamejipanga kula kodi za Wavietinam.
Wamezidi kuitafuna nchi kisayansi huku wakiwa wamejaliwa uwezo wa kujionyesha na kujisifia kuwa ni wapiga kazi na wazaleno ,kumbe wanatumikia maslahi yao.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukitaka kuwa mpigaji mwenye mafanikio nchi hii basi hatua ya kwanza ni kuchukua kadi ya CCM, hata serikali iwe kali vipi bado wana ka 'soft spot' linapokuja suala la ma kada. nadhani dogo ni mwanachama mtiifu
True, wakati wa kampeni mabsi ya uda yote yanaacha biashara na kubeba watu, bure
 
Kisena jamaa tapeli sana huyu bwana mdogo.Aliichukua ile Nyanza na NewEra Ginnery.Ameibia sana wakulima wa Pamba kuanzia Meatu huko mpaka Maswa.

Ni tapeli ambaye anakudhurumu,ukimfuata unaweza mpiga kwa blabla zake...ukimpiga anajifuta anasema basi tumeshamalizana.Kajamaa fulani kasanii sana,na kwa kweli kalikuwa hakagusiki.

Mara ya mwisho alikuwa akikaa Flat moja hivi pale Upanga,nilionana naye last time 2014 nikiwa Tz.Utapeli wake mpaka kwa Wamama wenye hela,kawaliza sana.

Uchaguzi Mkuu 2010 alienda na mtoto wa Rais mmoja mstaafu kwenye kura za maoni jimbo la Maswa kwa Shibuda,akashinda kwa nguvu kura za maoni.Huyu ndio alifanya Shibuda apigwe chini 2010 na akahamia CHADEMA akapewa jimbo.Kosa lake Shibuda ni kutangaza nia ya kugombea Urais 2010,wenye chama wakamuwekea Kisena.

Alimtapeli Muhindi wa Eicha na Tata alipoziingiza kwenye daladala za UDA.Huyu ndio anaivuruga UDART mpaka sasa haieleweki.Kifupi haka ni kahuni fulani kalikoharibu sana sekta ya pamba na Usafiri wa UDA.

Kwa hili,mimi nipo nyuma ya Amri Jeshi Mkuu John Joseph Pombe Magufuli.Hawa kina Kisena wameiba sana.
Mkuu barafu subiri kesho uone akina Salary Slip na rafiki zake watakavyokuwa wanadai kaonewa
 
Ni ngosha mjanja mjanja tatizo shule hana.Raha ya kuwa mjanja mjanja ni kuwa na shule pia kama mzee baba Chenge.
chenge nyoka mwenye makengeza ulishawahi kumuona ? ndiyo huyo baba kila skendo yumo tena zile kubwa lakini hakamatiki ni mjanja sana kwenye mikataba yake anakuwemo lakini hakuna pa kumkamatia
 
chenge nyoka mwenye makengeza ulishawahi kumuona ? ndiyo huyo baba kila skendo yumo tena zile kubwa lakini hakamatiki ni mjanja sana kwenye mikataba yake anakuwemo lakini hakuna pa kumkamatia
Sasa mkuu ukimgusa chenge si utaamsha mambo makubwa sana Yule atabaki vile mpaka kifo kimkute tu tofauti na hapo hakuna wa kumgusa hata kidogo
 
Sasa mkuu ukimgusa chenge si utaamsha mambo makubwa sana Yule atabaki vile mpaka kifo kimkute tu tofauti na hapo hakuna wa kumgusa hata kidogo
da aisee huyu msukuma sijui sheria aliisomea nchi gani maana ni mjanja balaa yaani skendo zote yumo na mnaona kabisa lakini hata pakumuanzia hampaoni alishawajhi kuitwa akahojiwe akakataa wenziew walienda na hakufanywa kitu na bungeni ni MHESHIMIWA MWENYEKITI
 
Back
Top Bottom