Hivi Ripoti ya CAG pekee haitoshi kupeleka watuhumiwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Ripoti ya CAG pekee haitoshi kupeleka watuhumiwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, May 22, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Baada ya Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kueleza madudu ya baadhi ya Wizara kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma.

  Kamati zote na bunge na ile ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali (POAC) ambayo Mwenyekiti wake Zitto Kabwe, na kamati ya bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mwenyekiti wake James Lembeli, zilionyesha namna mawaziri walivyoshindwa kuwajibika na kusababishia taifa hasara kubwa.

  Hivi (Takukuru) na (DCI) wanachunguza nini wakati (CAG) na ripoti za kamati tatu za bunge zote ziko wazi na wote tumeona hasara iliyotokea, kazi ya Takukuru ni kuchunguza rushwa sijui wanahusika vipi kwenye hili sakata.

  Wanasheria tusaidieni ni nani mwenye mamlaka yenye uwezo wa kufungua kesi dhidi ya hawa wahusika.
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kama unataka wanasheria wakusaidie peleka jukwaa la sheria.
   
 3. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ritz niwewe kweli unaetaka kujua haya? Sisi inabidi tukuulize wewe na Nnauye Jr mtuambie serikali yenu inawajibika vip katika hili?mi nashangaa kama wewe lakin wewe usishangae kama sisi kwakua siri unaijua
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hii ndiyo njia pekee ya kuendeleza ufisadi mtakatifu, maana yake hapo inaundwa kamati na posho maalum juu. Kwa hiyo hamna jipya, pia ni njia za kuchelewesha ili watu wasahau maana sisi watanzania kwa kusahau haraka tumejaliwa.
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Audit report ndiyo uthibitisho pekee wa wizi uliotokea au ubadhirifu, kwa kawaida watuhumiwa walipaswa kupelekwa polisi na baadae jalada kufunguliwa.Audit report ndiyo kielelezo kikuuu katika kesi ile maana ndiyo itaonyesha jinsi wizi ulivyofanyika na CAG atakuwa shahidi no1, wanasheria wasaidie mimi najua kidogo sana uhasibu an ukaguzi
   
 6. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Katika nchi ya kifisadi kama Tanzania ambayo inatekeleza zile sera za kulindana haitoshi hata kidogo..by the way Ritz we si unajua kwamba nyie CCM na serikali yenu huu ndio utaratibu wenu,au umeanzisha thread kutu joke mwanakwetu?
   
 7. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  naona sasa M4C imefika pazuri, kama na wewe mkuu ritz umeweza kuyaona haya ngoja tumsubiri tu Nepi kujua msimamo wake

   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ushaidi ni report za kamati na report ya CAG what else do we need to place these culprit in the house they deserve 'Segerea"
  No wonder wanataka kutupotezea issue ipoe watu waendelee kupeta mtaani!
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ripoti ya mkaguzi ni tofauti na jalada la uchunguzi. ripoti haiongei mahakamani inabidi watafutwe mashahidi wa kuipresent na wachukuliwe
  maelezo kwa mujibu wa kanuni za mwenendo wa mashtaka na sheria ya ushahidi.
   
Loading...