Hivi rasimu ya katiba mpya ilianzishwa na upinzani maana CCM hawakumbuki

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hakika moto wa katiba mpya umekuwa moto

Mchakato wa rasimu ya katiba mpya unaonekana ni suala geni sana hapa tanzania na mwanzilishi wake inaonekana ni cuf au chadema kwani ccm inaonekana haimjui aliyeanzisha rasimu ya katiba mpya.

Ikumbukwe mchakato wa katiba mpya ni maono ya rais mstaafu jakaya kikwete aliona ni vema tanzania ikapata katiba mpya kutokana na katiba iliyopo kupitwa na wakati na mambo mengi yamebadilika na viraka vimekuwa vingi.Lakini wanufaika na katiba iliyopo mahafidhina waliuvuruga mchakato mzima wa ile katiba.

Mwaka 2015 ilani ya CCM ilikuwa na suala la katiba mpya lakini wanufaika wa katiba iliyopo wakasema wanajenga uchumi na uchumi wenyewe umeshuka na katiba

Hawakuishughulikia.

Kaja rais mwingine nae akasema anajenga uchumi na polisi wameanza kuzuia wananchi wasikusanyike hata kwenye mikutano ya ndani iliyoruhusiwa ili mradi kuwazuia wasijadili suala la katiba mpya najiuliza

Kwanini CCM inaogopa katiba mpya?

Miaka 60 CCM imekuwa madarakani inahangaika kujenga uchumi na bado haijafanikiwa kwa sababu ya katiba iliyopo leo itawezaje kujenga uchumi kwa katiba

Ile ile iliyoshindwa miaka 60 iliyopita?

Tusidanganyane uchumi utajengeka kwa katiba mpya katiba iliyopo ina mapungufu mengi sana.

Sent from my sm-j600f using jamiiforums mobile app
 
Uoga wa Katiba mpya kwa CCM unaleta maswali mengi sana. Kama CCM wangekuwa wanashinda uchaguzi na kutawala kwa haki, wasingekuwa wanaogopa Katiba mpya kiasi hiki
 
Mama anaposema wanaodai Katiba Mpya wanaleta chokochoko je wakati ule alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la kuleta chokochoko katika nchi?
 
Back
Top Bottom